Prof. Assad: Kudhibiti wizi wa mali za umma Baraza la mawaziri lisiwe na siri

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,865
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Musa Assad amesema ubadhirifu unaotokea kwenye baadhi ya wizara huwa hauna maelezo zaidi ya kusema 'Ni maamuzi ya Baraza'

Amesema suala hilo linafanya kuwepo kwa mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma, hivyo ni vizuri kuwa na uwazi katika baraza la mawaziri.

Ametolea mfano nchi zilizoendelea kama Dernmark ambapo taarifa zote za baraza la mawaziri huwekwa wazi ili wananchi wajue kinachoendelea.

Amesisitiza kuwa namna bora ya kupambana na rushwa na ubadhirifu katika ofisi za umma ni kuwa na uwazi.

Naungana naye Yuko sahihi ila CCM hawawezi kukubali Hilo na hata upinzani nao wakipewa nchi hawatalikubali Hili..tuna tatizo Kama taifa
Alichomaanisha yeye ni kwamba ubadilishwe mfumo wa sasa wa uendeshaji wa vikao vya Baraza la Mawaziri.

Nchi ikiwa na Mifumo Imara haiwezi kuyumbishwa na wanasiasa kupitia vyama vyao.
 
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Musa Assad amesema ubadhirifu unaotokea kwenye baadhi ya wizara huwa hauna maelezo zaidi ya kusema 'Ni maamuzi ya Baraza'

Amesema suala hilo linafanya kuwepo kwa mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma, hivyo ni vizuri kuwa na uwazi katika baraza la mawaziri.

Ametolea mfano nchi zilizoendelea kama Dernmark ambapo taarifa zote za baraza la mawaziri huwekwa wazi ili wananchi wajue kinachoendelea.

Amesisitiza kuwa namna bora ya kupambana na rushwa na ubadhirifu katika ofisi za umma ni kuwa na uwazi.

Wewe ndio unafaa kuwa waziri wa feza
 
Huyu ndiye anafaa kuliongoza Taifa hili
Mwenye masikio asikie Roho aliambia Taifa
Walaji wengi mnoooooooo
Haki mtalipa hii dhuluma
Mshahara wa dhambi ni ....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Amepata mwanya wa kuongea na anasema ukweli... akina ndugai wamepata mwanya wa kuongea na wanaongea u afiki tuu..
Uzur Asad aliongea ukweli hata enzi za mwenda zake
 
Ndiyo kila kitu kiwe kinafanywa kwa uwazi, siyo kwa kufichaficha gizani. Giza siyo zuri mara zote. Kongole Prof. Assad kwa kutoa ushauri huu adhimu.
 
Back
Top Bottom