Prof. Anna Tibaijuka ni dalali wa ardhi Kigamboni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Anna Tibaijuka ni dalali wa ardhi Kigamboni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Jul 25, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Jul 25/07/2012

  Na,

  Nyaronyo Kicheere

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alishangiliwa sana pale alipoteuliwa kushika wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Kapteni Mstaafu, John Chiligati. Bahati mbaya ushabiki kwa uwaziri wa Tibaijuka haukudumu muda mrefu kwa sababu wananchi wamemgundua mapema kuwa si mkweli, mbaguzi na asiyefuata sheria za nchi kama zilivyotungwa na Bunge la Jamhuri.

  Kabla ya kwenda mbali, tumtendee haki Profesa wetu kwa kutaja bayana uwongo wake, ubaguzi wake na kutotii sheria kwake kunakomfanya asifae hata kushika wadhifa wa uwaziri anaoushikilia kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachojinasibu kutetea wanyonge.

  Kuhusu uongo;

  Tarehe 30 Machi, 2012 Profesa Tibaijuka aliwaahidi na kuwahakikishia wananchi wa Kigamboni kunakotajwa kujengwa Mji Mpya kuwa atafanya kazi na kamati ya wananchi wa Kigamboni lakini kinachotokea sasa ni profesa huyo kufanya kazi na kamati ya madiwani isiyo rasmi!

  Wiki iliyopita Mbunge wa Kigamboni, alimpa mama huyo alama ya sifuri katika utendaji wake, akimtuhumu Profesa Tibaijuka kuwahonga madiwani wanne wa Kigamboni, madiwani Juma Mkumbi wa Kibada, Selemani Mathew wa Vijibweni, Dotto Masawa wa Kigamboni na Kanali mstaafu Lwambano wa Tungi, kwenda kuhudhuria Bunge mjini Dodoma kwa kuwalipia nauli, chakula na malazi.
  Kama inavyoonyesha katika kundi la wananchi wa Kigamboni walioalikwa na profesa wetu hayumo hata mjumbe mmoja kutoka kamati ya wananchi inayoongozwa na Mwenyekiti Stewart Swai, Makamu Mwenyekiti Kassim Abdallah, Katibu Deogratius Charles Mayala na Naibu Katibu Christian Methew.

  Tatizo kubwa hapa ni aina ya madiwani walioteuliwa na Profesa wetu kuhudhuria kikao cha Bunge wakati wa hotuba ya makadirio ya wizara yake kama ushahidi kuwa umma wa wakazi wa Kigamboni wanauunga mkono mradi wa Mji Mpya Kigamboni. Kateua madiwani wote kutoka eneo la mradi pekee siyo eneo lingine la temeke! Kwa nini?

  Diwani wa kwanza Juma Mkumbi, maarufu Juma Viwanja, huyu amepata umaarufu wa kuitwa Juma Viwanja kwa sababu ni dalali wa viwanja vya raia na hakosi kuwepo jengo la Ardhi kwa wiki mara mbili au tatu. Bila kuongeza chumvi mtu wa namna hii anafahamika kwa nini anafurahia mradi wa mji mpya Kigamboni.

  Juma Viwanja anasubiri kuvuna. Kwake yeye mradi huu ni wakati wake wa kuvuna na haitarajiwi kuwa atawakilisha wananchi wapate haki yao kwenye ardhi na majengo yao. Hivi mradi haujaanza na anashinda wizarani mara mbili au tatu kwa wiki siku mradi ukianza ataondoka wizarani kweli?

  Diwani wa pili Dotto Masawa Huyu hana rekodi nzuri hata kidogo. Dotto ni mtuhumiwa wa wizi wa magari. Nimeambiwa kuwa gari aina ya Land Cruiser mali ya mkuu wa Majeshi wa Kenya lililoibwa na kutangazwa Afrika Mashariki yote, lilikutwa kwenye yadi yake ya kuuzia magari katikati ya jiji.

  Si hilo tu, majuzi wakati wa mbio za mwenge, Dotto Masawa aliteremshwa kwenye gari na polisi ambao hatukujua walitumwa na nani wala walitokea wapi na siku mbili baadaye tukasikia kuwa alipelekwa Morogoro, Mji kasoro bahari, kujibu tuhuma za wizi wa gari!
  Hatuna uhakika kama kesi hiyo imekwisha, bado inatajwa au imemalizwa nje ya mahakama kwa kusuluhishwa kati ya walalamikaji na walalamikiwa.

  Sasa diwani wa aina hii ndiye anamfaa Profesa Tibaijuka katika kusimamia haki ya wananchi au atasimamia kuiba viwanja vya wananchi? Ni raia gani, mwananchi gani au mfuasi gani wa Tibaijuka ataridhika kuwakilishwa na Juma Viwanja na au Dotto Masawa (mtuhumiwa wa wizi wa magari) katika kusimamia haki yake ya ardhi, viwanja na fidia? Yaani hawakuonekana madiwani wengine ila Juma Viwanja na Dotto Masawa? Kweli ni sawa hii?

  Diwani wa tatu Kanali Mastaafu Lwambano wa Tungi. Huyu ni mwanajeshi mstaafu aliyestaafu akiwa na cheo cha Kanali; huyu alisikika siku ya tarehe 11/6/2012 kwenye mkutano wa mbunge akimfokea raia aliyesema hataki mradi na akamwamrisha akae chini.
  Kwa hasira raia waliokuwepo pale walikuja juu na kumnyamazisha yeye diwani na kumtaka kama hataki kusikiliza mawazo yao ya kupinga mradi basi aondoke mkutanoni. Yeye diwani keshakubali na anautaka mradi na bila kuwasikiliiza wananchi wanataka nini anawafokea halafu huyu ndiye awawakilishe? Kweli?

  Kwanza diwani huyu aliingia CCM lini? Yeye si mwanajeshi na amestaafu mwaka juzi tu huku tukiambiwa na kuaminishwa kuwa jeshi halina chama! Je, alikuwa CCM tangu jeshini, aliingia CCM na kukata kadi kwenye geti la kambi wakati anatoka siku alipostaafu au aliingia CCM siku alipoomba kugombea udiwani?


  Pili, diwani huyu anamwakilisha nani? Mbona wananchi wa kata ya Tungi anaodai kuwawakilisha wanapinga mradi na wanajeshi wastaafu kama yeye wametamka kwenye umoja wao kuwa kamati yao ipo pamoja na kamati ya wananchi wa Kigamboni ambayo Tibaijuka hataki kushirikiana nayo?


  Diwani wa nne Selemani Mathew maarufu kama Big Man tangu enzi ya uchezaji wake wa mpira katika Simba na timu ya taifa. Mathew alishinda uchaguzi wa udiwani katika uchaguzi mdogo hivi karibuni na hana uzoefu wowote na nadhani kaingizwa kundini mahususi kusaidia kufanikisha mipango ya wakubwa.

  Nia mbaya ya madiwani hawa aliowalipia Tibaijuka kwenda kushuhudia hotuba yake ikisomwa ni dhahiri na hawana sifa ya kuwawakilisha wananchi na hawastahili kusimamia haki za wananchi katika fidia, katika kupewa maeneo mengine wala kusimamia wananchi katika utambuzi wa nani ana haki na nani hana.

  Hoja za ubaguzi na kutofuata sheria hazina maelezo marefu na nitazijadili kwa pamoja. Profesa Tibaijuka ni mkazi wa Dar es Salaam na ana hekalu lake pale Makongo Juu ambako wasomi wengi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamejenga mahekalu yao, nadhani (sina uhakika) kutokana na pesa wanazopata za utafiti, posho za safari na hongo za wanafunzi wasiojiamini. La muhimu hapa ni kwamba Profesa Tibaijuka kaanzisha mradi mwingine wa mji mpya Makongo Juu na amemteua mtu yule yule aliyeboronga maandalizi ya ujenzi wa Mji Mpya Kigamboni, Lameck Mtui, kuusimamia, lakini tofauti na Kigamboni kwa Tibaijuka (Makongo Juu) sheria inafuatwa!

  Tumewasikia wakazi wa Makongo Juu wakihojiwa na kushiriki kujadili mpango wa uanzishwaji mradi kabambe wa ujenzi wa mji mpya Makongo kitu kinachoitwa kitaalamu Public Hearing. Kwa nini Kigamboni hakukufanyika Public Hearing kama inayofanyika Makongo Juu? Hatusikilizwi kwa nini? Public Hearing haitufai Kigamboni? Kwa vile sisi si wasomi eh? Kwa vile sisi tu maskini eh? Kwa vile sisi hatujui Kingereza eh? Na je, haya ndiyo Profesa Tibaijuka aliyojifunza huko UN na Habitat? Tibaijuka kaja kuwafukarisha watu mskini ili wawe maskini zaidi? Sasa hatutaki mpaka na sisi tupatiwe nafasi ya Public Hearing kama Makongo; ubaguzi wa nini?

  Na hapa tuseme wazi kuwa sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007 haikufuatwa na hao walioandaa, wanaoushabikia, wanaong'ang'ania na wanaolazimisha kutekelezwa mradi wa ujenzi wa Mji Mpya Kigamboni. Kamati ya wananchi inadai na inataka sheria hii ifuatwe.

  Kamati ya wananchi na wananchi wa Kigamboni wanahoji kuwa kuna tatizo gani hata waache kufuata sheria ya Mipango Miji waliyotunga wenyewe. Wananchi wa Kigamboni hawataki zaidi ya kile kilichotajwa ndani ya sheria hii. Serikali na Tibaijuka wasiwe madalali wa ardhi ya Kigamboni bali watekeleze matakwa ya sheria tu. Hakuna cha ziada wala pungufu ya hili.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nilicheka sana nilipomsikia akisema "Nimekuja kupambana na Umasikini, sikuja kupambana na Masikini" Sijaona tija yake huyu mama!!!!!!
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kuwa CCM kote kumeoza kwa hiyo hata mtu mzuri akiwa huko huoza pia, ndio maana kila anayeonekana mzuri akiwa ccm huchafuka.
   
 4. S

  Sessy Senior Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ardhi tanzania ni bomu ambalo ipo siku tu litalipuka.....
   
 5. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Makala ni nzuri,,,, ina mashiko,,, hongera advocate,,nyaronyo kicheree, MaMA TIBAIJUKA ANA KESI ZA KUJIBU HAPO,,,
   
 6. Dr F. Ndugulile

  Dr F. Ndugulile MP Kigamboni

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 248
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Ardhi ndio mtaji pekee wa mwananchi maskini. Utaratibu huu Mpya wa kuwapokonya maskini na kuwapa matajiri kwa kisingizio cha uwekezaji kinaweza kutuletea shida mbele ya safari. Ni muhimu Serikali ikawashirikisha wananchi katika maamuzi.
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mheshimiwa nakuunga mkono100%tuko pamoja na wewe na sisi ni wakazi wa kigamboni ingawa tuko nje ya nchi lakini unatufariji sana kwa msimamo wako ila usife moyo na hao madiani we know leve yao ya kuona mambo inaishia kwenye kulazwa holi kubwa na kulishw chakula cha bei but not give up we will fight together mpaka kigamboni wajue ina wenyewe mama tibaijuka apeleke hizo politics muleba kuna ardhi kubwa kuliko kigamboni atapata wawekezaji wengi tu
   
 8. a

  andrews JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​kigamboni ni yetu tibaijuka ubabe hautakusaidia jaribu kufuata taratibu kigamboni kuna wasomi kama wewe usijisahau sana hata kwenu muleba kuna walala hoi lakini respect ni muhimu plz
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  S/N:
  2.Mark Mwandosya
  7.Abbas Mtemvu
  24.A.F Luambano-M/kit wa mtaa CCM
  30.A.Kitwana Kondo
  31.Aggrey Mwamri
  87.Asha Meck Sadiki
  147.Dotto Msawa--Diwan CCM
  218.Dr Faustine Ndungulile
  242.George Mkuchika
  258.Hawa Ghasia
  288.Hasheem Thabeet(Hashim Thabit)
  304.Idd Azan
  344.John M. Cheyo--CCM D
  389.Khalfan Kikwete
  458.Michael Pombe Magufuli
  553.Yusuf Mzee
  580.Pindi Chana
  583.Ramadhan Dau
  619.Said Meck Sadiki
  672.Sitti Abbas Mtemvu
  675.Sophia Simba
  7O1.Victor Geogre Mkuchika
  715.William mhando
  724.Yusuf Mustafa Yakub

  YALE YALEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280

  Kwa nini uandikie mate wakati wino hupo
  ???? Diwani wa CCM Dotto Masawani Akamatwa kwa wizi wa gari
   
 11. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safiiiiiii
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Huu mradi wa mji mpya ni batiri,kigamboni kuna wanajeshi wengi sana wana ardhi kule kwhyo mama tibaijuka asiforce watu awadalalie kama anataka kua dalali akadalalie hekalu lake la makongo kwanza,pili kama ukanda wa bahari waende bagamoyo na goba kwa kikwete wachukue yale maeneo wajenge miradi yao! Tatu Dr Faustine Ndungulile kama mb wa kigamboni tunaomba ulifikishe ili swala kwa rafiki yako tibaijuka kuna watu wanafuga mapori tu kigamboni kuanzia kisalawe hadi mwasonga kuna watu wamechukua ardhi kubwa bila kuiendeleza anzeni na Hussein mwinyi na heka zake 65 kisalawe pili muanze na muhindi wa mwasonga yule anafuga mapori tu na bila kumsahau Chacha rafiki wa sumaye naye anafuga mapori tu!! Mimi eneo langu lipo jirani na rafiki yako aliyejenga kisalawe kigogo
   
 13. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mh. pole kwa hayo yote ndani ya chama chako, ukienda kinyume ndani ya CCM Tayari ww unaitwa msaliti, eti ilani za chama ni lazima zitekelezeke... very wonderfull, hata kama hazina tija kwa mtanzania?
   
 14. Imany John

  Imany John Verified User

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Investors are our new Gods~lissu.

  Anasema hao ukiwagusa tu polisi wameshatia timu na mabomu kuja kutawanya wanyang'anyi ambao ndio wapokonywa ardhi ambao kimsingi ni watanzania masikini.
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  posti ya chuki binafsi
   
 16. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wakati wao huu.
   
 17. M

  Mindi JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni kwamba mfumo unaotawala katika nchi yetu sasa hivi ni wa kunyonya masikini kutajirisha wachache. matajiri wanakuwa matajiri zaidi. Profesa Tibaijuka anasimamia mfumo huo. kimsingi huo si mfumo unaoweza kupambana na umaskini. hata kama angekuwa na nia nzuri kiasi gani, bado anasimamia mfumo kandamizi na kama ana uadilifu, utatumika kutekeleza mfumo huo. Sera zetu sio za kujali mkulima mdogo kijijini wala mlalahoi wa mjini. kama Profesa Tibaijuka ni mkweli, ajiuzulu tu hiyo nafasi. akitaka kulazimisha mambo yaende itabidi afanye hayo anayofanya. hapo hamsaidii mlalahoi na kama ni mtu safi, atakuja kujuta sana hapo baadae
   
Loading...