Profesa Anna Tibaijuka: Kumaliza tatizo la machinga kuwe na adhabu iwekwe kwa wanaonunua ovyo barabarani

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Mbunge wa zamani wa jimbo la Muleba Prof Anna Tubaijuka amesema tatizo la machinga halitaisha kwa kutoa amri na kuwafukuza mbali bunge linatakiwa kukaa na kutunga sheria yenye adhabu kwa wateja wanaopenda kununua bidhaa hovyo mabarabarani.

Prof Tibaijuka amesema wamachinga hufuata wateja na kama hamna wateja hutamuona machinga kwenye hilo eneo hivyo serikali lazima ijikite kubadilisha utamaduni wa wanunuzi wawe wananunua kwenye masoko maalumu yalitengwa na siyo kununua hovyo hovyo mabarabarani.

Kauli ya hovyo kabisa! Halafu eti huyo ni professor?!

Wamachinga wengi wako sehemu ambazo watu wanapita mfano maeneo ya “waenda kwa miguu” sasa huyu mama anataka polisi ama mgambo wakae pembeni ya hao machinga kuvizia watu wanaopita na kununua bidhaa za hao wamachinga? Akili ya wapi hii? Tena anasema bunge likae na kutunga sheria.

Kama huyu mama ndiyo yule aliyekana kupewa pesa na Rugemalila, basi nina wasiwasi huenda amechanganyikiwa tayari akili yake haiko sawa.

Huwezi kuwakamata hao endapo wamachinga watakuwa wameondolewa, inaonyesha anataka wabakie halafu wanunuzi ndiyo waanze kuviziwa wakinunua wakamatwe. Duh!
 
Mpingeni Professor kwa hoja sio kwa mhemko, yeye anafikiria katika level ya kidunia sio kipopoma popoma. Na si kila mmoja ana staili kujibizana na professor, ubinafsi wenye ujinga na upumbavu ni bomu baya sana kwa taifa.
 
Nilisikia alienda kumsalimia mzee Ruge baada ya kutoka gerezani akamchunia mazima...nadhani kwasababu ya kujifanya anarudisha pesa aliyopewa na Ruge eti hakujua Kama ni pesa ya umma.

Huo u prof inawasadia tu kupata pesa lakini siyo kuelimika.
 
Tukisema tunamisomi ya ajabu nchi hii watu wanabisha maana huyo ndo profesori moja takataka ambayo haina msaada kwenye jamiii kala mgao wa kodi zetu bado na yuko bungeni ingekua nchi za wengine huyo angekua ananyea debe na kulala saa kumi na mbili
 
Wahenga walisema.

PictureQuotes1637771729.png
 
Huyu mama hajishitukiagi na hizi pumba zake?

Anna siasa zimemuharibu mpaka amesahau basic economics!! Ili kuwa na soko ni lazima kuwa na muuzaji na mnunuzi [ Supply and Demand}! Sasa hao anaosema watungiwe sheria na kukamatwa kwa kununua vitu barabarani utawapataje kama wamachinga watakuwa wameondolewa?

Suluhisho la machinga ni kuwajengea masoko yanayokidhi mahitaji yao karibu na makazi ya watu ambao ndio wateja wao!! Msijenge masoko bila kuwahusisha wafanya biashara wenyewe otherwise mtajenga white elephants kama pale MACHINGA COMPLEX ilala!!!
 
Watu wakiacha kununua barabarani ,machinga atafuata nini barabarani?
 
Mbunge wa zamani wa jimbo la Muleba Prof Anna Tubaijuka amesema tatizo la machinga halitaisha kwa kutoa amri na kuwafukuza mbali bunge linatakiwa kukaa na kutunga sheria yenye adhabu kwa wateja wanaopenda kununua bidhaa hovyo mabarabarani.

Prof Tibaijuka amesema wamachinga hufuata wateja na kama hamna wateja hutamuona machinga kwenye hilo eneo hivyo serikali lazima ijikite kubadilisha utamaduni wa wanunuzi wawe wananunua kwenye masoko maalumu yalitengwa na siyo kununua hovyo hovyo mabarabarani.

Adhabu ni kwa machinga sio mnunuzi. Kwani kuwatoa imeshindia
 
Mtu ukizeeka Kama mama Tibaijuka Ni vizuri kutulia ulee wajukuu Kama huna katafute vituo vya yatima Mungu akusamehe madhambi ya kifisadi uende mbinguni sababu muda uliobakiza duniani ni mchache kuliko maisha ulioishi duniani
Huyu mama hajuwi shida

Sasa kama yeye bln anaiona pesa ya mboga

Unategemea ataongea nini cha maana

Ova
 
Back
Top Bottom