Prof. Anna Tibaijuka atolea Ufafanuzi sakata la Escrow, agoma Kujiuzulu

ongozi vijiji 2708
mitaa 644
vitongoji 26,300

Tarehe rasmi ya uchaguzi 14/dec/2014
Mitaa inayoshindaniwa 3741
vijiji 12443
Vitongoji 64,616

Mapingamizi na ccm kujitwalia u

Viongozi waliojitwalia uongozi kwa mapingamizi aslimia 33%

Viongozi walioshinda kwenye uchaguzi siku ya 14/dec/2014= ccm47% ukawa 53%

ccm wanajivunia ushindi wa 80% wakijumuisha na 33% ya mapingamizi
 
tumsubiri mzee wa tezi dume.nae akileta mzaha kama alivyozoea lazima itafune upande wao.
 
Anamjua Mr Dhaifu! hawezi kumfanya lolote.
Hapo tumeliwa kidogo tusubiri labda nasi tutakula.
Ahaa aha ahaaaaaa!.
 
Mama Tibaijuka tayari umeshachafuka na usione nafasi ya uwaziri kama ya mzazi na mtoto ambayo haiwezi kutenganishwa. Fedha ulilipwa wewe, kama ulikuwa na nia nzuri ya kuijenga hiyo shule yako ili iaminike na wafadhili wengine fedha zingekwenda huko moja kwa moja. Kwa maana nyepesi ni kuwa wewe ndio hiyo shule na shule ndio wewe. Inawezekana baada ya shule kulipa deni la Bank M, sasa wewe ndio unaidai shule kwa vile fedha zilizolipa deni zilitoka kwako.
 
ongozi vijiji 2708
mitaa 644
vitongoji 26,300

Tarehe rasmi ya uchaguzi 14/dec/2014
Mitaa inayoshindaniwa 3741
vijiji 12443
Vitongoji 64,616

Mapingamizi na ccm kujitwalia u

Viongozi waliojitwalia uongozi kwa mapingamizi aslimia 33%

Viongozi walioshinda kwenye uchaguzi siku ya 14/dec/2014= ccm47% ukawa 53%

ccm wanajivunia ushindi wa 80% wakijumuisha na 33% ya mapingamizi

Baada ya kujumlisha hizo 47% na 33% wianisha na ukawa.
Haziwezi kuwa 80% lazima itakuwa 76.86.......%. Kwa hesabu yangu ya kiKayumba.
Ni hilo tu, tusubirie na matokeo ya J'pili mmojawapo atapanda au kushuka.
 
Kwa ufupi alichoonyesha Bi. Tibaijuka ni jinsi gani alivyo mbishi na anavyowachukulia Watanzania hawana akili. Hii inanikumbusha ile kauli ya kejeli ya Basil Mramba, "Bora Watanzania mle majani lakini ndege ya rais itanunuliwa". Huku ndiko kunakoitwa ulevi wa madaraka. Pesa za escrow zilikuwa ni za wizi kwa kwa sababu PAP haikuwa na Deed of Assignment (hati ya kupewa dhamana ya kumiliki hisa za mbia mkuu wa IPTL ambaye alikuwa amefilisika) bali iko mikononi mwa Standard Chartered Bank ya HK. Hivyo huu ulikuwa wizi sawa na wa EPA. Kauli ya Bi Tibaijuka kuwa ripoti ya CAG haimtaji ni ya upotoshaji mkubwa. Siyo kazi ya CAG kuchunguza makosa ya jinai; hiyo ni kazi ya PCCB na police. Kanuni ya msingi (rule of thumb) hapa ni: mwizi na mpokea mali ya wizi wote ni wezi. Halafu I'm deafened by Tibaijuka's monotonous cries, "Shule! Shule!" Huu ni utovu wa nidhamu na maadili.Tumemkabidhi ofisi ya umma ili afanye majukumu ya hiyo ofisi na siyo kutumia muda na rasilimali za umma kwa biashara zake binafsi. Huu ni ufisadi.
 
Since last week anatumia STK .....na sio kibao cha WZR AR kwenye gari anayozunguka nayo town NDIO kilishanuka?

No anaogopa wananchi watampiga mawe..seriously..huyu ni prof gani asiyejua ethics za kiuongozi ..alipewa mabilioni..then hakuyatolea hata maelezo..its real shame..halafu anakuwa mbishi..utafikiri yuko right na alichokifanya...majanga kama kweli hawa ni viongozi wetu tunaowategemea.Tena ni maprof!
 
Katika utetezi wake Prof. Tibaijuka hajatoa hoja inayofanana na uprofesa wake; amezungumza kama mwanasiasa wa kawaida tu; tena mbumbumbu asiyejua nini maana ya dhamana ya ofisi ya umma. Huwezi kutumia ofisi ya umma kukusanyia mtaji wa kuendesha miradi yako binafsi halafu ukabaki salama. Ukweli ni kwamba Prof. Tibaijuka amekula rushwa kwani kuna kitu kikubwa zaidi ambacho Rugemalira ameshapata ama anatarajia kupata kutokana na dhamana aliyonayo Tibaijuka kama Waziri wa Serikali. Swali, je hiyo ndiyo kazi tuliyomtuma Tibaijuka tulipomkabidhi dhamana ya Wizara ya Ardhi? Baadhi yetu tulitarajia angalau Prof. Tibaijuka katika utetezi wake atuambie aliomba fedha kwa ajili ya Sekondari za Kata katika Jimbo lake la Muleba Kusini na siyo shule yake binafsi iliyoko Dar. Shule hizo za kata zina matatizo lukuki ambayo kwa hakika sh. 1.6/= zingesaidia sana kupunguza. Pamoja na usomi wake, Prof Tibaijuka ameonyesha kuwa hana uwezo wa uongozi wa umma.
 
Prof. Kasoma alama za nyakati kuwa maji yamemwagika hayawezi kuzoleka!.
Ubunge tayari uko rehani sasa na uwaziri nao aupoteze! Potelea mbali kuliko kufulia zaidi!.

Grafu yake inayoyoma kwenda negative. Toka UN, Ubunge (Waziri) hadi kuwa mtuhumiwa wa kula sahani moja na mwizi!.

Dah njaa kali (njala likoko ikoma na Tibaijuka!)
 
Wanajamvi,

Prof. Tibaijuka amesisitiza kuwa hana hatia na fedha alizopewa na kaka yake Ruge, hivyo haoni sababu ya kujihudhuru.

Kwa upande wangu kwa kuwa naona JK aelekei kumwajibisha , bora arudishe zile fedha 1.6b ili tusitoke bure.

Fedha hizo zinaweza kupangiwa kitu kingine kuliko kupoteza vyote, hivyo ajiandaa kumsindikiza kuakikisha anazikabidhi kwa JK au kampuni itakayokuwa imepangiwa kuzipokea, lakini wasiwasi wangu ni kwamba zisije kuwa kama zile za EPA ambzo mpaka leo hatujui zimepokelewa na nani na zilitumikaje, je kuna ambazo bado hawajaleta na ni kwa sababu gani?
 
wa kabisa na kauli
ya Anna Tibaijuka kuwa
hawezi kujiuzulu kwa kuwa
yeye na Mhongo ni majembe
ya JK. Kauli hii inakuja wakati raisi
anataka kulihutubia taifa
jumatatu baada ya kutoka
kwenye matibabu.
Anakwenda kuzungumza
mambo mazito yanayohusu nchi yetu. Kabla ya kuja
kuhutubia nafikiri atakuwa
ameshafanya vikao na cabinet
ya mawaziri ikiwa na maana
kuwa baraza la mawaziri ndilo
linalomshauri Raisi. Inawezekana kwenye baraza
la mawaziri wamekubaliana
kuwa mawaziri
waliotuhumiwa wasijiuzulu.
Kwa hiyo maneno aliyoyatoa
Tibaijuka ni kama briefing ya kikao cha mawaziri na raisi.
Kwa hiyo maneno hayo moja
kwa moja yanaenda kuathiri
hotuba ya Raisi jumatatu kwa
namna moja au nyingine. Huyu mama alikuwa hana haja
ya kupigana vijembe na
watanzania, Ni kweli alipewa
fedha na Rugemalila iwe ni
halali au si halali sioni sababu
ya kubishana na watanzania eti sijiuzulu. Mimi mwenyewe
sitaki ajiuzulu bila kufanyika
uchunguzi wa kina kama
kweli wanahusika ila maneno
aliyoyatoa ni KIBURI na
upungufu wa elimu ya uongozi. Katika wakati kama huu
ambao watanzania wengi
wanaishi chini ya dola moja
unaibuka ukiwa na bilioni 1.6
bank ni kuamsha hasira zao
kuwa eti sijiuzulu. Kaa kimya Raisi ndiye mwenye kauli ya
mwisho utoke au usitoke
unavuruga hotuba ya raisi ya
Jumatatu.
 
tibaijuka_clip-564x272.jpg


Waziri wa ardhi na makazi Profesa Anna Tibaijuka

Thursday, December 18, 2014


Na Peter Edson

Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.


Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.
“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwenye sakata hili la Escrow” anasema Profesa Anna Tibaijuka.


TIBAIJUKA ASISITIZA KUPOKEA MCHANGO WA SHULE NA SI VINGINEVYO(KUPOKEA ZAWADI)
Bonyeza vidio
https://www.youtube.com/watch?v=nMNU_sPj00o
Via mwananchi.co.tz
 
Nasikitishwa kabisa na kauli
ya Anna Tibaijuka kuwa
hawezi kujiuzulu kwa kuwa yeye na Mhongo ni majembe
ya JK. Kauli hii inakuja wakati
raisi
anataka kulihutubia taifa
jumatatu baada ya kutoka
kwenye matibabu. Anakwenda kuzungumza
mambo mazito yanayohusu
nchi yetu. Kabla ya kuja
kuhutubia nafikiri atakuwa
ameshafanya vikao na cabinet
ya mawaziri ikiwa na maana kuwa baraza la mawaziri ndilo
linalomshauri Raisi.
Inawezekana kwenye baraza
la mawaziri wamekubaliana
kuwa mawaziri
waliotuhumiwa wasijiuzulu. Kwa hiyo maneno aliyoyatoa
Tibaijuka ni kama briefing ya
kikao cha mawaziri na raisi.
Kwa hiyo maneno hayo moja
kwa moja yanaenda kuathiri
hotuba ya Raisi jumatatu kwa namna moja au nyingine. Huyu
mama alikuwa hana haja
ya kupigana vijembe na
watanzania, Ni kweli alipewa
fedha na Rugemalila iwe ni
halali au si halali sioni sababu ya kubishana na watanzania
eti sijiuzulu. Mimi mwenyewe
sitaki ajiuzulu bila kufanyika
uchunguzi wa kina kama
kweli wanahusika ila maneno
aliyoyatoa ni KIBURI na upungufu wa elimu ya
uongozi. Katika wakati kama
huu
ambao watanzania wengi
wanaishi chini ya dola moja
unaibuka ukiwa na bilioni 1.6 bank ni kuamsha hasira zao
kuwa eti sijiuzulu. Kaa kimya
Raisi ndiye mwenye kauli ya
mwisho utoke au usitoke
unavuruga hotuba ya raisi ya
Jumatatu.
 
Hakuna ulevi mbaya kama wa madaraka hatari zaidi ya kiroba au gongo!
 
Back
Top Bottom