Prof. Adolf Mkenda amsimamisha kazi kaimu mrajisi wa ushirika Lindi kwa kukilazimisha Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) kukodi ghala

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,687
15,106
Waziri wa kilimo prof Adolf Mkenda amekuwa mbogo baada ya kuzungushwa na mrajisi wa ushirika mkoa wa Mtwara na kuamua asimamishwe kazi mara moja na amemtaka katibu mkuu apeleke mrajisi mwingine mkoa wa Mtwara.

Pia waziri wa Mkenda amempa onyo kali mrajisi wa ushirika mkoa wa Kilimanjaro (KCU) na kumuweka kwenye uangalizi kwa muda maalum.

===========

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege ameagizwa kumsimamisha kazi Kaimu Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Lindi Ndg Edmund Masawe. Edmund amesimamishwa kazi kutokana na kukilazimisha Chama cha Ushirika wa mazao (AMCOS) cha Umoja kilichopo Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi kukodi ghala kwa ajili ya kuhifadhia Korosho ilihali chama hicho kina ghala lake la kuhifadhia korosho.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda ametoa agizo hilo tarehe 13 Mei 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dodoma. Mhe Mkenda amemtaka Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt Benson Ndiege kujitathmini kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi ya kutoa ushauri wake alioelekezwa wakati wa kikao cha majadiliano kilichofanyika tarehe 8 Mei 2021.

Waziri Mkenda amebainisha kuwa katika kikao kazi hicho Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini aliagizwa kutoa taarifa ya ushauri wake kuhusu Mradi wa pamoja wa vyama 32 vya msingi vya Ushirika (G32) vya Mkoani kilimanjaro lakini hakufanya hivyo. “Katibu Mkuu Mimi nadhani Mrajis wa Vyama vya Ushirika anafanya mzaha, Anadhani siwezi kumng’oa na pengine mahali pa kuanza kupafumua katika Wizara ya Kilimo ni Tume ya Maendeleo ya Ushirika” Amekaririwa Mhe Mkenda Prof Mkenda amesema kuwa amemuweka Mrajis na mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya ushirika katika uangalizi maalumu huku akimuagiza kufika Jumatatu tarehe 17 Mei 2021 kuwasilisha mapendekezo hayo haraka iwezekanavyo.

Waziri Mkenda amesema kuwa amekabidhiwa kuingoza Wizara ya Kilimo ili kuimarisha sekta ya Ushirika nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima.

Akizungumzia kuhusu kadhia iliyoikumba Tanzania Kuhusu Nzige wa Jangwani amesema kuwa kati ya tarehe 14 Januari, 2021 na 24 Februari, 2020 Tanzania ilipata uvamizi wa Nzige wa Jangwa waliotokea nchi jirani ya Kenya na kuingia katika Wilaya nane (8) za Mwanga, Siha na Moshi (Kilimanjaro), Simanjiro (Manyara); Longido, Monduli na Ngorongoro (Arusha); na Lushoto (Tanga). Kati ya Wiaya hizo, nzige walikuwa wakihama kutoka kwenye maeneo waliokuingia na kulala maeneo mbalimbali ya Wilaya nne (4) Siha (Kilimanjaro), Simanjiro (Manyara); Longido na Monduli (Arusha) wakitanda kwenye eneo la jumla ya hekta 6,441.
======

My take: Viongozi mbalimbali wenye vinasaba na Chadema walidhani kifo cha JPM ndiyo muda wao wa kupiga dili umefika na kuzungusha wananchi lakini sasa kumbe wezi wanaendelea kutumbuliwa kama zama za mwendazake.
 
My take viongozi mbalimbali wenye vinasaba na Chadema walidhani kifo cha JPM ndiyo muda wao wa kupiga dili umefika na kuzungusha wananchi lakini sasa kumbe wezi wanaendelea kutumbuliwa kama zama za mwendazake.
Mimi na Mwendazake ni kitu kimoja
 
Umeleta ujumbe vizuri tena unachomekea CDM, unawapa sifa bila sababu yoyote na unaonyesh uwezo wako ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom