Prof. Adelardus Kilangi aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rais Magufuli kutofanya mabadiliko watendaji wa Serikali, Mawaziri kubadilishwa

Naona watendaji wamepewa 'security' ya nafasi zao.
Ilikua wazi kwamba asingewabadili kwakua wametekeleza alicho waelekeza kuhakikisha wapinzani hawarudi Bungeni au kupata nafac za uwakilishi, kwahiyo ni vigumu kuwatupa walio shikilia siri nzito nyuma ya ushindi wake.

Tatizo ni sisi tulio kuwa tunafanya yote tuliyo yafanya tukitrajia uteuzi, hapo ndipo pana shida .Viti maalum vimetoka ,hakuna nafac ,uteuzi wa ma Dc na ma ded hakuna nafac, kazi itakua ni kupiga majungu tu!
 
Baraza la Mawaziri pendwa ni hili hapa
1. Waziri Mkuu -Kasimu Majaliwa
2. Tamisemi-Jafo
3. Ujenzi na Mawasiliano-Nditiye
4. Fedha-Mpango
5. Uwekezaji-Kimei
6. Mambo ya Nje-Kabudi
7. Madini-Doto Biteko
8. Kilimo- Bashe
9. Elimu-Dr Ndalichako
10. Sheria-
11. Mambo ya Ndani-simbachawene
 
Afanye mabadiliko asifanye huo ni utashi wake ila tra, wizara ya fedha na biashara kuna tatizo; mainly communication issues.

Kuna malalamiko mengi sana ya watu kubambikiwa kodi not necessary huo ndio uhalisia. Ukiniuliza mimi nitakwambia asilimia kubwa ya malalamiko as to do with VAT.

Sheria ya mwongozo ipo ila kila mwaka kuna financial act ambayo inakuja na mabadiliko yake. Kinachoonekana asilimia kubwa ya walipa kodi hawapo up to date na sheria za kodi ya VAT wala awaelewi obligations zao.

Walipaji awajui muda wa kutunza record zao hizi ndio sababu TRA wakifika na kuwakadiria kodi za miaka mitatu nyuma pengine awajui kama wanajukumu la kutunza kumbukumbu labda kwa miaka sita just incase TRA ikiamua kwenda kukagua. Na kama hawana TRA itaawaamulia.

Wafanya biashara wengi awaelewi VAT accounting schemes za TRA na majukumu yao how often they have to pay their periodic advances.

In short hii TRA ni tatizo na wizara zinazo husika na hiyo sector hazina msaada kwenye kuwasaidia walipa kodi, technocrats ni makatibu wakuu wa wizara wakurugenzi wao na management za TRA.

There is a serious problem kwenye administration za VAT not necessary kwa sababu ya utendaji, bali uelewa wa wajibu wao kwa upande wa walipa kodi. Something needs to be done.
 
Rais magufuli hasisitiza kuwaacha baadhi ya mawaziri waliokuwemo kwenye baraza la mawaziri lillilopita, kutokana na spidi na perfomance kutoendana.

NB: mwananchi unapendekeza mawaziri gani, waachwe awamu hii kutokana na kutokuwa na spidi na perfomance mbovu
 
Naomba kujuzwa huyu mwanasheria aliyekula kiapo leo ni mzaliwa wa wapi? Au anatokea mkoa gani?: pia usiamini sana kauli za wanasiasa uapishaji ndo umeanza wengine waweza kuenguliwa tu.
 
Prof. Adelardus Lubango Kilangi amekuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na Rais John Magufuli kwa kipindi cha muhula wa pili wa Uongozi wa Rias Magufuli.

Prof. Kilangi ameteuliwa na kuapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo amesema hii imeonesha Rais ana imani naye kwa hivyo ameahidi kutumikia kwa uadilifu.

Katika hotuba yake Prof. Kilangi amesema kazi kubwa ya mwanasheria sio kuwa mahiri wa kufahamu sheria na vifungu mbalimbali bali kufahamu muktadha wa sheria ambapo sheria hutumika.

=============

Kwa sasa anaeongea ni Rais John Magufuli

MAGUFULI: Pamekuwa na tabia kila serikali mpya inapoingia au awamu nyingine inapoingia watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya serikali kwamba panatokea mabadiliko. Na kwa sasa hivi naona wana hofu sana wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na ninawashangaa kwanini wanakuwa na hofu, kwasababu kama ni mafanikio ya serikali ni pamoja na wao, kama ni ushindi wa asilimia 84 ni pamoja na wao ndio wameuwezesha ushindi huu kupatikana kwa kufanya kazi nzuri kwenye maeneo yao.

Wanasiasa ambao tumeguswa na hili ni mimi ambae ilibidi nikawaombe tena kura kwa miaka mitano pamoja na makamu wangu, mwingine alieguswa ni Waziri Mkuu kwa sababu lazima tuteue Waziri Mkuu tena pamoja na mawaziri, wengine nashangaa kwanini wanakaa.

Sasa wachaguliwa wengine wameisha, mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani? Unless kama performance yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vi messege vingine, mheshimiwa Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana nilimwambia kipindi chake kinaisha baada ya mimi kuapishwa. Msiwe na wasiwasi na kunawezekana kusitokee mabadiliko hata moja labda kwa mtu atakaestaafu au kufanya mambo ya hovyo.

Kuchaguliwa kwetu haina maana sasa tunakuja kubadilisha, Gavana Luoga maana yake nibadilishe tena Gavana? Kwanini? Kwa hiyo watu wachape kazi katika nafasi zao, kwa maana nyingine hakuna mabadiliko, tulianza wote tutamaliza wote. Mabadiliko yatakayokuwepo ni kwenye nafasi tu zile za uwaziri ambazo zenyewe tulienda kuomba upya. Wapo watakaorudi, wapo hawatarudi tena siku hizi option ni kubwa, nina wabunge 264 kwa hiyo uchaguzi ni mkubwa zaidi, hili sitaki kusema uongo.

Nikishamaliza hivyo basi, wengine wachape kazi tu, kwahiyo ndugu zangu viongozi niliona nilizungumze hili kwamba watendaji ndani ya serikali chapeni kazi zenu, mpo na mtaendelea kuwepo labda ikishafika miaka ya kustaafu hilo ni suala lingine au umeamua mwenyewe kuacha hilo ni suala lingine au performance yako imekuwa haiendani na speed tunaiyoitaka ya ilani ya uchaguzi hilo ni sula lingine lakini nionavyo sasahivi kila mtendaji katika kila mahali, RC, makatibu tawala, maDC, wakurugenzi, MaDas, makatibu tarafa, watendaji wa kata mpaka wenyeviti wa vijiji mpaka nyumba kumi kumi na wengine katika maendeo mbalimbali wachape kazi, hakuna cha kuwa na wasiwasi.

Yani kila mwaka ukiingia unaanza kuapisha! Hata kuapisha kunachosha, nianze tena kuapisha wakuu wa mikoa 26! Niende maRas 26, niingie maDC, siwezi. Tumeshamaliza, wachape kazi ila atakaejiondoa yeye mwenyewe ndio ntaapisha, AG kafanye kazi. Yale mawazo mazuri uliyopewa hapa kayafanyie kazi.
Kadanganya kwa mfumo wa mind game kama kicha wa simba,but atawafukuza wengi sana
 
Mambo yote hayo hayana mvuto. Ngoja summons za ICC.
 
Tusitarajie kuona sura mpya sana itampasa kuwarudisha walewale sababu wameshiriki kusaidia kutenda dhambi ya dhuluma na udanganyifu.
 
Watendaji walikua matumbo joto...

Ila kwenye uapishaji sura za watendaji waliyokuwepo hapo zilikua kama hazina furaha kabisa...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom