Prof. Adelardus Kilangi aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rais Magufuli kutofanya mabadiliko watendaji wa Serikali, Mawaziri kubadilishwa

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,161
2,000
Jiwe amepambana sana na CHADEMA Lakini hajui maadui wa nchi kuwa ni.

Umasikini.
Ujinga.
Maradhi

MWAMBIE UPINZANI UKO MIOYONI MWA WATU.HATUMPENDI.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
5,634
2,000
Hana jipya.

ANACHOWEZA NI KUPAMBANA NA WAPINZANI,
HAJUI KUWA MWALIMU NYERERE ALIAINISHA MAADUI WA TANZANIA NI UMASIKINI, UKINGA NA MARADHI.

Jiwe anajua maadui wa Tanzania ni wapinzani.

Tumemchoka.
Kwa sababu wapinzani baadhi ndio wanaongoza kwa "UKINGA" huo. Mtu anataka kuuza nchi na kuifanya koloni tena; akili kweli, au???
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
5,634
2,000
Jiwe amepambana sana na CHADEMA Lakini hajui maadui wa nchi kuwa ni.

Umasikini.
Ujinga.
Maradhi

MWAMBIE UPINZANI UKO MIOYONI MWA WATU.HATUMPENDI.
Tunajua upinzani uko mioyoni ndiyo sababu huo upinzani usingeweza kutoka huko mioyoni kwenda kuandamana barabarani kwa mujibu wa wito wa Mr Mzungu. Na kwa vile hakuna aonaye kilichomo mioyoni, nani ajuaye, pengine ulishajistaafia wenyewe kitambo tu.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
5,634
2,000
Jiwe amepambana sana na CHADEMA Lakini hajui maadui wa nchi kuwa ni.

Umasikini.
Ujinga.
Maradhi

MWAMBIE UPINZANI UKO MIOYONI MWA WATU.HATUMPENDI.
Tunajua upinzani uko mioyoni ndiyo sababu usingeweza kutoka huko mioyoni kwenda kuandamana barabarani kwa mujibu wa wito wa Mr Mzungu. Na kwa vile hakuna aonaye kilichomo mioyoni, nani ajuaye, pengine ulishajistaafia wenyewe kitambo tu.
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
15,354
2,000
“Pamekuwa na tabia kila Serikali mpya inapoingia Watu wanakuwa na hofu hasa Watendaji ndani ya Serikali kwamba panatokea mabadiliko na kwa sasa Wakuu wa Mikoa na Wilaya naona wanakuwa na hofu na nawashangaa kwanini wanapata hofu maana kama mafanikio ya Serikali ni pamoja nao”-JPM baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu Kilangi Dodoma leo.

“Wakuu wa Mikoa na Wilaya naona wanakuwa na hofu na nawashangaa kwanini wanapata hofu maana kama mafanikio ya Serikali ni pamoja na wao, kama ushindi wangu wa 84.4% umechangiwa pia na wao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa miaka 5, wasiwasi wanini?, naona meseji za baadhi ooh Mheshimiwa Mimi nimefanya kazi sana” - JPM.

“Narudia Watendaji wa Serikali wachape kazi wasiwe na wasiwasi, hakuna mabadiliko tulianza wote tunamaliza wote, yaani nianze kuapisha tena Wakuu wa Mikoa 26 siwezi, hata kuapisha kunachosha, Watu wachape kazi waliokuwepo watabaki walewale labda watakaostaafu au kuwa na utendaji mbovu” -JPM.

“Mabadiliko yatakuepo kwenye uwaziri, kuna watakaotoka na watakaoingia ” -JPM.
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,213
2,000
Mh lazaro NYALANDU amezuiliwa namanga akiwa anaelekea Kenya kutafuta hifadhi. Amezuiliwa namanga. Kufika mwakani tutabaki mimi na wewe
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,213
2,000
Madiliko ya uongozi ni gharama sana haswa kiutendaji

Heri waendelee waliopo kama mabadiliko abadilishe pale inapohitajika
DED wanaomba kuhamishwa vituo vyao, madudu waliyoyafanya kipindi Cha uchaguzi mazingira yanawasuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom