Prof. Adelardus Kilangi aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rais Magufuli kutofanya mabadiliko watendaji wa Serikali, Mawaziri kubadilishwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,533
8,323
Kilangi.jpg
Prof. Adelardus Lubango Kilangi amekuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na Rais John Magufuli kwa kipindi cha muhula wa pili wa Uongozi wa Rias Magufuli.

Prof. Kilangi ameteuliwa na kuapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo amesema hii imeonesha Rais ana imani naye kwa hivyo ameahidi kutumikia kwa uadilifu.

Katika hotuba yake Prof. Kilangi amesema kazi kubwa ya mwanasheria sio kuwa mahiri wa kufahamu sheria na vifungu mbalimbali bali kufahamu muktadha wa sheria ambapo sheria hutumika.

=============

Kwa sasa anaeongea ni Rais John Magufuli

12.jpeg

MAGUFULI: Pamekuwa na tabia kila serikali mpya inapoingia au awamu nyingine inapoingia watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya serikali kwamba panatokea mabadiliko. Na kwa sasa hivi naona wana hofu sana wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na ninawashangaa kwanini wanakuwa na hofu, kwasababu kama ni mafanikio ya serikali ni pamoja na wao, kama ni ushindi wa asilimia 84 ni pamoja na wao ndio wameuwezesha ushindi huu kupatikana kwa kufanya kazi nzuri kwenye maeneo yao.

Wanasiasa ambao tumeguswa na hili ni mimi ambae ilibidi nikawaombe tena kura kwa miaka mitano pamoja na makamu wangu, mwingine alieguswa ni Waziri Mkuu kwa sababu lazima tuteue Waziri Mkuu tena pamoja na mawaziri, wengine nashangaa kwanini wanakaa.

Sasa wachaguliwa wengine wameisha, mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani? Unless kama performance yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vi messege vingine, mheshimiwa Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana nilimwambia kipindi chake kinaisha baada ya mimi kuapishwa. Msiwe na wasiwasi na kunawezekana kusitokee mabadiliko hata moja labda kwa mtu atakaestaafu au kufanya mambo ya hovyo.

Kuchaguliwa kwetu haina maana sasa tunakuja kubadilisha, Gavana Luoga maana yake nibadilishe tena Gavana? Kwanini? Kwa hiyo watu wachape kazi katika nafasi zao, kwa maana nyingine hakuna mabadiliko, tulianza wote tutamaliza wote. Mabadiliko yatakayokuwepo ni kwenye nafasi tu zile za uwaziri ambazo zenyewe tulienda kuomba upya. Wapo watakaorudi, wapo hawatarudi tena siku hizi option ni kubwa, nina wabunge 264 kwa hiyo uchaguzi ni mkubwa zaidi, hili sitaki kusema uongo.

Nikishamaliza hivyo basi, wengine wachape kazi tu, kwahiyo ndugu zangu viongozi niliona nilizungumze hili kwamba watendaji ndani ya serikali chapeni kazi zenu, mpo na mtaendelea kuwepo labda ikishafika miaka ya kustaafu hilo ni suala lingine au umeamua mwenyewe kuacha hilo ni suala lingine au performance yako imekuwa haiendani na speed tunaiyoitaka ya ilani ya uchaguzi hilo ni sula lingine lakini nionavyo sasahivi kila mtendaji katika kila mahali, RC, makatibu tawala, maDC, wakurugenzi, MaDas, makatibu tarafa, watendaji wa kata mpaka wenyeviti wa vijiji mpaka nyumba kumi kumi na wengine katika maendeo mbalimbali wachape kazi, hakuna cha kuwa na wasiwasi.

Yani kila mwaka ukiingia unaanza kuapisha! Hata kuapisha kunachosha, nianze tena kuapisha wakuu wa mikoa 26! Niende maRas 26, niingie maDC, siwezi. Tumeshamaliza, wachape kazi ila atakaejiondoa yeye mwenyewe ndio ntaapisha, AG kafanye kazi. Yale mawazo mazuri uliyopewa hapa kayafanyie kazi.
 

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
969
3,791
Rais Magufuli kwenye hafla ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kwamba hana mpango wowote wa kubadili watendaji katika awamu yake ya pili. Hili limekuja baada ya kudai kwamba ameanza kupokea jumbe za watendaji wanaodai kwamba awamu ya kwanza walifanya kazi nzuri.

Rais Magufuli amesema kwamba watendaji watakaobalishwa ni wale waliofikia umri wa kustaafu, watakaoamua wenyewe kuacha kazi au wale wazembe watakaoshindwa kufanya kazi.

Pamekuwa na tabia kila Serikali mpya inapoingia watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya serikali, kwamba yanatokea mabadiliko na sasa hivi naona wenye hofu sana ni wakuu wa mikoa na wilaya na nawashangaa kwanini wanakuwa na hofu

Nashangaa napokea vimeseji vingine, Mhe Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa, niliona hili nilizungumze wakuu wa mikoa wakuu wa Wilaya msiwe na wasiwasi, na inawezekana wala yasitokee mabadiliko

Wakuu wa Mikoa na Wilaya naona wanakuwa na hofu na nawashangaa kwanini wanapata hofu maana kama mafanikio ya Serikali ni pamoja na wao, kama ushindi wangu wa 84.4% umechangiwa pia na wao, wasiwasi wanini?, naona meseji za baadhi ooh Mheshimiwa Mimi nimefanya kazi sana

Narudia Watendaji wa Serikali wachape kazi wasiwe na wasiwasi, hakuna mabadiliko tulianza wote tunamaliza wote, yaani nianze kuapisha tena Wakuu wa Mikoa 26 siwezi, hata kuapisha kunachosha, Watu wachape kazi waliokuwepo watabaki walewale

Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wengine wachape kazi, hakuna mabadiliko, tulianza pamoja, tutamaliza pamoja, Mwanasheria Mkuu yuleyule, huenda Spika na Naibu Spika watabaki walewale, labda atakayestaafu au ambaye atalegalega kiutendaji

Mabadiliko yatakuwepo labda kwenye Uwaziri tu huko wapo watakaoingia na kutoka, tena sasa hivi nina Wabunge wengi mabadiliko yatuwepo tu, lakini Watendaji wengine kama Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya watabaki walewale
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
59,332
87,772
Rais Magufuli amemwapisha mwanasheria mkuu wa serikali Prof Kilagi na kumtaka akamtangulize Mungu mbele katika utendaji wake wa kila siku.

Rais Magufuli amemtaka Prof Kilagi kama mwanasheria mbobezi akahakikishe serikali haipotezi kesi hasa zile zenye maslahi ya nchi.

Source: Upendo tv

Maendeleo hayana vyama!
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,663
3,308
Kwa hii "tulianza pamoja na tutamaliza pamoja" sioni Waziri mkuu akibadilishwa
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,319
16,903
Eboo, sasa hapa huyu ndio kasema nini? Kwamba alifikiri tulitarajia abadilishe wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi, makatibu wakuu na kina Dotto waondolewe nk kwa kuwa ameshinda uchaguzi awamu ya pili? Naona nikigundua chujio ya maneno nitakuwa tajiri sana!
 

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,366
35,136
Kwa hii "tulianza pamoja na tutamaliza pamoja" sioni Waziri mkuu akibadilishwa
Kwahiyo ulitegemea kuwa Majaliwa aondoke? Mbona tulishasema wazi kuwa huu utawala kitakachobadilika ni uteuzi tu wa baraza ambapo kina Kamwelwa, Shonza, Hasunga, Kigwangalla hawatakuwepo!
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
46,732
79,702
Nakubaliana nae Rais Dk. Magufuli kwa 100% kuwa hama haja ya Kufanya 'Mabadiliko' makubwa kwani waliokuwepo 'Utendaji' wao ulikuwa mzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

5 Reactions
Reply
Top Bottom