Prof. Abdallah Safari, uzalendo wako ni wa kupigiwa mfano ndani ya CHADEMA

Aiseee baba yangu mwisho wa c c m unakaribia chadema wakae mkao wa kula kuongoza nchii

ngoja niamke nikapate supu na kisusio
 
Sikubaliani na hoja ya mshindi wa pili katika kura za maoni za chama kilichoshinda kimizengwe kwamba ndio awe anachukua nafasi, wakati kuna mshindi wa pili halali aliyechaguliwa na wananchi.
 
Ccm wanajitahidi kushika kila pembe ili wasianguke kwa kuwa wamezoea kufanya michezo michafu. Hizi kwa mtu mwenye akili anaweza kusema kuwa haridhiki na zile hoja zilizo mvua ubunge kafumu? Inahitaji kuwa na akili za maiti aisee.

1. Hoja ya Rage kupanda jukwaani na bastola Nape hajaridhika nayo?

2. Kauli ya magufuli kuwa wana igunga wasipo ichakua ccm hawajengewi daraja, nayo pia Nape haikubali?

3. Ustadhi wetu kuwa elekeza waislamu wenzangu kuto kumchagua mgombea wa chadema kwa kuwa wamemvua hijabu mkristo mwenye jina la kiislamu. Na bado haikuwa hijabu ni mtandio.

4. Kugawa mahindi wakati wa uchaguzi wakati hakukuwa na tishio lolote la njaa na wala hakukuwa hata na dalili ya watu kupoteza uhai kwa njaa.

Ccm inakufa vibaya.
 
Naona maprofesa na madaktari wote wanaotoa maoni juu ya kupunguza gharama za uchaguzi kwa kumkaimisha mshindi wa pili katika kura za maoni za vyama husika wanakosea na pengine hawajafikiria zaidi ya upande mmoja.
1.Washindi wa kura za maoni hupigiwa kura na wanachama na wapenzi wa chama husika.
2.Wagombea ubunge hupigiwa kura na makundi mbalimbali, kuna uwezekano aliyepiga kura akawa kapiga kura kwa sababu ni mwanachama wa chama husika au akawa si mwanachama na vilevile wapo wanaopiga kura kwa kuwa wana imani na mahaba kwa mgombea, mwisho wapo wanaopiga kura kwa kuwa tu wamepewa takrima au chochote kitu.
Kama ukiitafakari hii kauli yangu namba mbili,binafsi ninaamini kabisa, mbunge kama akifariki au akivuliwa ubunge, mwakilishi wa chama kinachoshika nafasi ya pili ndio akaimishwe nafasi iliyoachwa wazi.......

Upo sahihi mkuu kwa kuwa chama husika ndicho kimehusika kwa mfano kufanya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi kama rushwa na matusi.

Sio sahihi kurejesha haki ya kuteua mgombea toka chama husika,hapo hawataona hasara yoyote,
aidha mgombea wa chama kingine ndiye ambaye haki yake imeporwa kwa ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, si haki akose nafasi pengo likiwepo na wengi hawataona sababu ya kupinga ukiukwaji huo mahakamani.
 
Naona maprofesa na madaktari wote wanaotoa maoni juu ya kupunguza gharama za uchaguzi kwa kumkaimisha mshindi wa pili katika kura za maoni za vyama husika wanakosea na pengine hawajafikiria zaidi ya upande mmoja.
1.Washindi wa kura za maoni hupigiwa kura na wanachama na wapenzi wa chama husika.
2.Wagombea ubunge hupigiwa kura na makundi mbalimbali, kuna uwezekano aliyepiga kura akawa kapiga kura kwa sababu ni mwanachama wa chama husika au akawa si mwanachama na vilevile wapo wanaopiga kura kwa kuwa wana imani na mahaba kwa mgombea, mwisho wapo wanaopiga kura kwa kuwa tu wamepewa takrima au chochote kitu.
Kama ukiitafakari hii kauli yangu namba mbili,binafsi ninaamini kabisa, mbunge kama akifariki au akivuliwa ubunge, mwakilishi wa chama kinachoshika nafasi ya pili ndio akaimishwe nafasi iliyoachwa wazi.

hILI NDIYO TATIZO KUBWA LA WASOMI WETU WANFIKIRI KWAMBA WAO PEKE YAO NDIYO WANO uwezo wa kufikiri na kuchambua kumbe wanajidhalilisha.Hivi kweli prof. mzima unadiriki kushauri mshindi wa kura za maoni ashike nafasi, wanafahahamu kwamba mshindi wa kura za maoni maepigiwa na wanachama wa cham chake?????? huyo hajapigiwa kura na wananchi kwa ujumla wao.Kweli wasomi tunao.shame on you academician.Ndiyop maaana kazi yenu ni kufelisha wanafunzi si kwenu ni kufeli wanafunzi wengi ndiyo mnajifariji nayo
 
Sikubaliani na hoja ya mshindi wa pili katika kura za maoni za chama kilichoshinda kimizengwe kwamba ndio awe anachukua nafasi, wakati kuna mshindi wa pili halali aliyechaguliwa na wananchi.

natumia simu mkuu ningekupa like hata hivyo hapa umetoa kitu cha maana kuliko hata hao maprof.
 
Kwa maoni yangu yule aliyetoa rushwa au kukiuka maadili ya uchaguzi wakati wa upigaji kura basi siyo tu kuvuliwa ubunge bali hata chama chake kipigwe faini na kutoshiriki tena kwenye chaguzi za eneo husika.Hili litasaidia hata akina Magufuli wenye dhamana ya serikali kutosema toa rushwa ya maneno (Kujenga daraja mradi tu mkichagua chama tawala)
Na ikibidi chama ndicho kipate hasara ya kulipia chaguzi nyingine,hii itasaidia vyama kuwa makini nakuacha matusi na matumizi ya rushwa.
 
Jamani MWITA MARANYA, MATOLA na MKANDARA mbona mnaenda nje ya mada?. Hebu tujadili maudhui ya uzi husika, msijikite udini tu wakati hilo sio kusudio la mleta mada.

Hatujakwenda nje ya mada mkuu bali kuna issue imejitokeza ndani ya mnakasha huu basi ikaonekana ni muhimu kuiweka sawa.
Na bila shaka mkuu Mkandara ametoa hoja za kueleweka na ameeleweka vizuri sana, bila kusahau angalizo la mkuu Matola. Kwani sisi sote ni watanzania na lazima tujitambue na kama kuna mtu ama kikundi cha watu kinajaribu ama kinaendelea kututenganisha ni lazima tukitambue na kujitenga nacho.

Ni muhimu sana kuyatambua mambo yanayotugawa kwa misingi ya dini zetu ama kabila zetu ama rangi zetu na baada ya hapo tutafute suluhu ya kuondokana na vikwazo hivyo kwa pamoja na kwa umoja wetu. Tukifanikiwa kufanya hivyo sitarajii kuendelea kusikia malalamiko toka dini moja, ama kabila moja.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa napenda niwapongeze CHADEMA kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kufikia ushindi katika kesi hii ya ya kupinga matokeo yaliyowapa CCM ushindi. Hii ni dalili njema kwa CDM na ishara nzuri ya kuelekea kuchukua nchi ifikapo 2015. Hongera sana Prof. Safari na uongozi wote wa CDM.

Nasikitika kusema kuwa baada ya ushindi huu kwa CDM mahakamani tunategemea tena Uchaguzi mwingine mdogo utakaoligharimu Taifa pamoja za na vurugu,mbwembwe,majigambo na hata kupoteza uhai wa raia wasio na hatia. Hii yote ni kwasababu ya sera na sheria mbovu za Uchaguzi zilizoko kwenye katiba yetu ya JMT. Nitaeleza.

Kwa vile sheria ya Uchaguzi inaelekeza kwamba inapotokea Mbunge akashindwa mhakamani au kufariki basi lazima Tume ya Uchaguzi-NEC iitishe uchaguzi katika muda usiozidi 90. Hii sheria mbovu ambayo haipashwi kuendelea na inatakiwa kufutwa mara moja hasa kipindi hiki tunachotoa maoni kuhusu Katiba Mpya.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kwamba ili kuepuka gharama zisizo za lazima kutokana na hizi Chaguzi ndogo ni kwamba kuwe na sheria ambayo itaweka bayana kwamba:

(a).IWAPO MBUNGE ALIYEKO MADARAKANI ITATOKEA KUONDOLEWA MADARAKANI NA MAHAKAMA KWA KUKIUKA SHERIA ZA UCHAGUZI YEYE AU CHAMA CHAKE BASI MGOMBEA WA CHAMA KILICHOPELEKA MALALAMIKO MAHAKAMANI NA KILICHOPATA USHINDI WA PILI NDIYO APEWE NAFASI YA UBUNGE WA JIMBO HUSIKA.

(b).
IWAPO MBUNGE ALIYEKO MADARAKANI ATAONDOKA KWA SABABU YA KUJIUZULU,KUFARIKI DUNIA AU UGONJWA,BASI NAFASI HIYO ITACHUKULIWA NA MTU WA CHAMA KILEKILE KILICHOSHINDA WAKATI WA UCHAGUZI LAKINI AWE AMBAYE ALIKUWA WA PILI KATIKA KURA YA MAONI YA CHAMA AMBACHO MBUNGE WAKE ALIKUWA MADARAKANI.KAMA ALIYEKUWA WA PILI KATIKA KURA ZA MAONI HATAKUWEPO(KIFO,UGONJWA AU KUWA NA MADARAKA MENGINE),BASI ALIYEKUWA WA 3 AU 4 NDIYE ATAKAYECHUKUA NAFASI HIYO WAZI.

Sheria hii itaweka wazi vilevile kwamba yawezekana chama kilichoshika mkia au nafasi ya 3,4,5 n.k kutegemea idadi ya vyama vilivyoshiriki kwenye Uchaguzi ndicho kikaenda mahakamani kupinga matokea ya Uchaguzi na kikawa na ushahidi wa kumfanya Mbunge aliyeshinda aenguliwe basi bado sheria itaangalia chama gani kilifuatia kwa wingi wa kura(mshindi wa 2) kwa Mbunge aliyeshinda na hicho ndicho kipewe ridhaa ya kuongoza jimbo na siyo kile kilichofungua kesi Mahakamani.

Kwa mfano kama Igunga CCM walipata kura 26,000, CHADEMA kura 20,000,CUF kura 8,000,TLP kura 2,000 na UDP kura 800 kama ni swala la kupinga matokeo kwa Uamuzi wa Mahakama mshindi atakuwa ni CHADEMA hata kama CUF,TLP au UDP mmojawapo atakuwa ameenda Mahakamani kupinga matokeo hayo. Lakini kama issue itakuwa ni Kujiuzulu,Kifo au Ugonjwa kwa maana ya kuwa Mbunge wa CCM kajiuzulu,kafariki au hajiwezi kwa ugonjwa basi CCM watachukua mwanachama wao aliyeshika nafasi ya pili au ya tatu kwenye kura za maoni.
 
Ccm wanajitahidi kushika kila pembe ili wasianguke kwa kuwa wamezoea kufanya michezo michafu. Hizi kwa mtu mwenye akili anaweza kusema kuwa haridhiki na zile hoja zilizo mvua ubunge kafumu? Inahitaji kuwa na akili za maiti aisee.

1. Hoja ya Rage kupanda jukwaani na bastola Nape hajaridhika nayo?

2. Kauli ya magufuli kuwa wana igunga wasipo ichakua ccm hawajengewi daraja, nayo pia Nape haikubali?

3. Ustadhi wetu kuwa elekeza waislamu wenzangu kuto kumchagua mgombea wa chadema kwa kuwa wamemvua hijabu mkristo mwenye jina la kiislamu. Na bado haikuwa hijabu ni mtandio.

4. Kugawa mahindi wakati wa uchaguzi wakati hakukuwa na tishio lolote la njaa na wala hakukuwa hata na dalili ya watu kupoteza uhai kwa njaa.

Ccm inakufa vibaya.

Unajua uvivu wa kujadili hukumu kwa kupitia wanasheria wao,inaleta taabu chama kimoja kuwa na mbili gongana.Huyu nape ni mr misifa yeye kawa ndo mlopokaji sana bila kujua nini madhara yake.Vp unategeme nini kwa watawala kama hao zaidi ya kuongeza gharama za maisha.
 
hILI NDIYO TATIZO KUBWA LA WASOMI WETU WANFIKIRI KWAMBA WAO PEKE YAO NDIYO WANO uwezo wa kufikiri na kuchambua kumbe wanajidhalilisha.Hivi kweli prof. mzima unadiriki kushauri mshindi wa kura za maoni ashike nafasi, wanafahahamu kwamba mshindi wa kura za maoni maepigiwa na wanachama wa cham chake?????? huyo hajapigiwa kura na wananchi kwa ujumla wao.Kweli wasomi tunao.shame on you academician.Ndiyop maaana kazi yenu ni kufelisha wanafunzi si kwenu ni kufeli wanafunzi wengi ndiyo mnajifariji nayo

Lu-ma-ga,

Kwa kiasi fulani inaonekana kama una point lakini ukweli ni kwamba point yako haina uzito unless utuambie unataka kuleta hoja ya mgombea binafsi. Kiukweli ni kwamba tunapoenda kwenye kura TUNACHAGUA SERA ZA CHAMA HUSIKA NA SIYO MTU. CHAMA KAMA KIMEMTEUA MGOMBEA IT MEANS ANAWAKILISHA SERA ZA CHAMA NA SIYO YEYE BINAFSI NA KWA MUDA WOTE ATAKAOKUWA MADARAKANI ATATEKELEZA SERA ZA CHAMA SIYO ZA KWAKE.

Kwa hiyo is immaterial kudai kuwa mtu aliyeshika nafasi ya 2 kwenye kura ya maoni hafai kuteuliwa kujaza nafasi ya Ubunge simply eti alichaguliwa na wanachama na siyo Wananchi wa jimbo husika. What I believe hata huyu mshindi wa 2 au 3 akiwekwa kwenye hiyo nafasi ya Ubunge iliyo fall vacant kwa kujiuzulu,kifo au ugonjwa atakuwa akiendeleza na kutekeleza sera za chama siyo za kwake wala za marehemu au aliyejiuzulu!

Get me?
 
Back
Top Bottom