Product za shine and lovely si salama kwa matumizi ya binadamu

mjingamjanja

New Member
Dec 19, 2018
1
3
salute wanajamvi

kwa takriban miaka kama miwili hivi sasa nimekua nikikutana na bidhaa za kampuni moja iitwayo MIKU INVESTMENT LTD wanazalisha vipodozi kwa ajiri ya ngozi, nywere na kucha.

nimekua ni mtumiaji mzuri sana lakin baada ya kuona utofauti nikaamua kufuatilia chini chini

nilikua natumia vitu kama lotion zao, zikanitoa vipere vya kufa mtu. mafuta ya nywele nikawa ninamba za kutosha. hivi vitu vikanisababisha nifuatilie

kwenye kufuatilia nikakutana na majibu ya ajabu sana lakni kikubwa mtu alienipa majibu alikua ni mmoja ya wafanyakazi wa kampuni hilo

na haya ndio alioniambia

1) Kwamba lile ni kampuni la mtanzania na lina miaka kama mitatu sasa linafanya kazi
2) Wana product almost 50 na ni mbili tu zimethibitishwa na shirika la viwango tanzania yaani TBS (niliambiwa ni shampoo na lotion aina moja tu). nyingine huwa zina fail kwenye viwango

3) Kwamba kampuni lina products zenye nembo za TBS na wakati bidhaa zake hazijakidhi viwango. hili lilinishangaza kidogo, na nilivo fuatilia nikakuta kuna bidhaa zenye stika zilizotobolewa au kupakwa rangi kuificha nembo ya tbs, nikaambiwa walipewa onyo

4)kwamba jamaa huwa anaimport bidhaa za always na pampus. hii ndio ilinishtua sana kiukweli. huwa anakuja kufanya reparking upya, yaani anachukua mzigo ambao ume_expire (niliambiwa ni toka 2015 ndio expire date) then anakuja kufuta na kuprint ilizionekane ni kutoka 2017 na hapo ndipo huzipeleka sokoni.....sasa hapa nikapata hamu ya japo kuziangalia zilizopo sokoni nikaona zimekaa kufutwa futwa hivi...

my take..

ni kweli tunapenda uchumi wa viwanda, lakin ubora wa bidhaa ndio uwe mwongozo wa kila kitu. sijui hata kama huyu mzalishaji anawashauri na wataalam maana nimejaribu kufuatilia hata baadhi ya interviews zake naona anaongea vitu ambavyo havipo kabisa....

najua sio kiwanda hiki tu kuna na vingine, ni vema serikali wakaingilia kati na kuweza kunyoosha sehemu zilizo pinda...

nimeelezwa mengi juu ya unyanyasaji wa wafanyakazi, kufanyishwa kazi bila mikataba, but nilikua conserned na quality kwa muda huo...


nawasilisha bandugu
 
Kama ni kwel mbona wana matangazo ya products zao yapo kwenye TV??
Siwange katazwa

Meshtuka lakin kwakuwa na mm natumia moja ya product zao
 
Kama ni kwel mbona wana matangazo ya products zao yapo kwenye TV??
Siwange katazwa

Meshtuka lakin kwakuwa na mm natumia moja ya product zao
Za kuambiwa changanya na zako mkuu
What if hii ni kuchafuana ? Maana bongo tupo vizuri kwa futna kuanzia jiwe mpaka wananchi
 
Back
Top Bottom