Process za Kujenga Majengo Marefu

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,531
1,133
Wana JF nataka kufahamu na mnijuze maana JF ni jungu kuu lisilokosa ukoko!!
Nataka kufahamu kabla mradi wa ghorofa refu huwa vitu gani vya msingi vifanyike kwa hapa nchini? Je kuna sheria inayokataza sehem fulani hapa dar zisiwe na maghorofa na sehemu zingine yawepo? Je udongo pia ni kikwazo cha kutokuwa na majengo marefu hapa Dar ,achilia mbali pesa za kuanzisha mradi ?
Nawasilisha
 
Kujenga jengo refu kuna hatua unazopitia ambazo unaweza kuziweka katika mafungu matatu.
1. Washauri wa mradi
2. Vibali vya serikali
3. Ujenzi wa mradi
WASHAURI WA MRADI hawa ni wataalan wanaohusika katika design ya jengo husika Architect, structural engineer, service engineer, quantity surveyor.
Hawa wote huwa wanahusika katika design ya jengo na wanakupa documents muhimu za kuombea vibali vya Ujenzi.

VIBALI VYA UJENZI kabla haujaanza Ujenzi sharti upate vibali husika kutoka manispaa na kama eneo husika linahitaji kubadilishwa matumizi basi inabidi vibali kutoka wizara ya Ujenzi vipatikane.

UJENZI WA MRADI hii ndio hatua ya kuanza Ujenzi ambayo mhusika mkuu ni contractor. Hapa mkishakubaliana na contractor yeye anaenda kutafuta vibali CRB kwa ajili ya kuanza Ujenzi.

Kuhusu swali lako la je kama kuna maeneo ambayo hayaruhusu Ujenzi wa ghorofa refu ni kweli kuna baadhi ya maeneo huruhusiwi kujenga majengo marefu kama maeneo ya ufukwe masaki, oysterbay ili uweze kufahamu zaidi kuna mwongozo unaoonyesha limitations za Ujenzi.

Kuhusu aina ya udongo mara nyingi aina ya udongo huwa inasaidia kujua ni aina gani ya msingi utumike lakini sio kuzuia urefu wa jengo. Kwani hata baharini watu huwa wanajenga majengo marefu.

Ukitaka maelezo zaidi na msaada ni PM tu nitakusaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom