Process unayoweza kuitumia kujitwalia wateja zaidi na mapato zaidi katika biashara

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
1. Andaa orodha ya watu na taasisi ambazo unadhani zaweza kuhitaji huduma yako. Kwa mfano kama wewe ni mtengenezeji wa websites basi tafuta makampuni yote ambayo hayana website ama yana websites zisizokuwa relevant kwao.

Kwa huduma ama bidhaa yoyote kuna orodha kubwa sana unaweza tengeneza ya wale unaodhani wanaweza kuwa wateja wako. Hakikisha unaongeza nyama katika orodha yako.

Kwa mfano umeorodhesha makampuni 100 ambayo yanaweza kuhitaji bidhaa yako unapaswa kuongeza details kwa kila kampuni ikiwemo mahali ilipo, mtu unaeweza kuwasiliana nae na mawasiliano yake, etc

2. Andaa ratiba ya kutembelea ama kutuma mtu atembelee kila kampuni katika orodha yako. Matembezi yawe na nia ya kupata maelezo ya ziada ambayo hukuwa nayo awali.

Pia tumia fursa hiyo kufanya research kwenye hizo kampuni. Kwa ule mfano wa mtengeneza website unaweza fika na kujifanya kama mteja ila ukadadisi mbona kampuni haina website na kadhalika.

3. Chuja orodha yako na ubakiwe na wale ambao unahisi uwezekano wa kufanya nao biashara ni mkubwa zaidi.

4. Andaa proposal kwa kila mmoja na uhakikishe inakuwa imeshiba nyama na ina ushawishi mkubwa. Hakikisha unaonesha kuwa kweli unajua unachotaka kukifanya. Zifikishe hizo proposal kwa wahusika ukihakikisha zinafika kwa watu sahihi.

5. Fanya follow up katika kila baada ya kipindi cha muda maalum.

6. Hakikisha una bidhaa ama una timu ya kutosha ongezeko la wateja.

ALL THE BEST
 
Ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom