Process ili utambulike na "TFDA" kama mzalishaji wa vyakula anaefahamu , anisaidie !!!

Emmadogo

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,140
2,000
Lazima uwe na Food Inspector....ni graduate yoyote wa Food sience
eneo lako liwe katika hali ya usafi sana/ pamoja na wafanyakzi wako.
nadhani pia wanataka wafanyakzi wako wafanyiwe medical check ups kila mwaka....i think.

all in all nenda pale TFDA victoria
 
WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,291
2,000
Nataka kuanzisha bakery January, but Cjui process Za "TFDA" kunitambua, Msaada please anayejua process,????
Mkuu
Hongera sana kwa kuwa na wazo zuri la kuweza kujiajiri ama kuajiri.TFDA ni taasisi inayohakikisha unazalisha chakula salama kwa afya ya walaji,TBS inahakikisha unazalisha chakula chenye kiwango na ubora unaotakiwa.
Mimi kidogo ni mdau kuhusu hili basi nitakupa njia za kufuata.
1.KUANDIKISHA ENEO LA UZALISHAJI (PREMISES REGISTRATION)
Unatakiwa ufanye vitu vifuatavyo
a.Uwe na mchoro wa eneo lako la uzalishaji(factory layout) inavyoonesha mzunguko wa malighafi na bidhaa kutoka kupokea malighafi(raw materials,ingredients etc),uzalishaji(production),packaging(kufungasha) na despatching.
Tafadhari ramani/mchoro unatakiwa uoneshe unidirectional flow ili kuzuia cross contamination
2.Unatakiwa mazingira ya uzalisha yawe masafi
3.Unatakiwa uwe na msimamizi wa taaluma ya sayansi ya kula (Food science) ataandika barua (commitment letter) itaunganishwa na form za maombi yako kwenda TFDA,pia aambatanishe na cheti chake.Ili kupunguza gharama unaweza mtafuta huyo mtaalam mkaelewana akakupa chetu na barua yake (malipo inaweza kuanzia 200K) na kuendelea.
4.Download form za premisea registration kutoka kwenye wavuti yao na ujaze,pia kuna malipo ya kuandikisha,hii inategemea na mtaji wako wa kuanzia.
5.Wafanyakazi wako wote lazima wapimwe afya zao kutoka hospitali inayotambulika na serikali.Mfanyakazi aliye na ugonjwa unaweza kuambukiza kupitia bidhaa kamwe haruhusiwi kufanya uzalishaji,labda atibiwe mpaka apone.
5.Baada ya kutimiza maandalizi yako,nenda ofisi yoyote ya halmashauri kitengo cha afya,mkaguzi utapata kupitia pale,zamani walikua wanadai rushwa sana lakini siku hizi wanaogopa hata ukitaka kumpa ya maji.
6.Baada ya ukaguzi,ukipata marks kuanzia 75% utaruhusiwa kuendelea na uzalishaji lakini utahimizwa ufanye maboresho ya hapa na pale,chini ya 60% hawatakuruhusu km sikosei.
Kila la heri mkuu,ukishindwa niPM nitakusaidia mkuu.
BAADA YA KUANDIKISHA ENEO LAKO hatua ya pili ni kusajiri bidhaa zako (product registration)
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,077

Hizi hatua zote zinachukua miaka mingapi kukamilika??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom