Procedures za kusajili Charity Group

Oct 7, 2019
7
0
Guys niko na msukumo wa ndani wa kuanzisha charity group. Naomba maelekezo ya namna gani nitaisajili iwe official.
 
Guys niko na Msukumo wa Ndani wa kuanzisha Charity Group. Naomba maelekezo ya namna gani nitaisajili iwe Official
 
Guys niko na msukumo wa ndani wa kuanzisha charity group. Naomba maelekezo ya namna gani nitaisajili iwe official.
1. Uwe na wanachama waanzilishi wasiopungua 5
2. Muwe na katiba
3. Mkishakuwa na katiba mtaanza mchakato wa usajili mkiwa na
a. Nakala 3 za katiba
b. Nakala 4 za picha passport size
c. Nakala za cv za viongozi wenu
d. Barua kwa Mkuu wa Wilaya ambayo imepitia kwa mtendaji wa mtaa/kata
e. Form ya maombi kwa msajili yenye majina 3 ya waanzilishi ikionesha sahihi, namba za kitambulisho cha utaifa na anwani
f. Barua ya maombi kwa msajili
4. Mtahitaji kukaguliwa na msaidizi wa mkuu wa wilaya (Afisa Tarafa kwa niaba ya DAS) kwa ada ya ukaguzi isiyozidi 100,000 ktk ukaguzi wanachama wote watakuwepo kwenye ofisi yenu kwa mahojiano na huyo Afisa ili kujiridhisha kama wanachama waanzilishi wanaijua katiba, wanakubaliana nayo na wameipitisha.
5. Baada ya kupata barua toka kwa Mkuu wa Wilaya mtapeleka documents Dodoma kwenye usajili na ada ni 115,000 bila gharama za stamp duty ambayo nadhani bado ni 1500

Kila la kheri boss

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom