Pro magembe ana hisa na serikali ya rais jk kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pro magembe ana hisa na serikali ya rais jk kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jun 25, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Rais JK aliwahi kutamka hadharani wakati anazindua bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.Kauli yake ya kutokuwa na hisa na mtu yeyote ndani ya serikali yake imkwenda wapi,mbona waziri wake Pro Maghembe amekua anaingia kwenye tuhuma mbalimbali na serikali yake imekaa kimya?

  Kulikuwa na tuhuma za vocha za pembejeo za wakulima ambazo ziliitingisha wizara ya kilimo lakini hakuna hatua zilizo chukuliwa dhidi ya utendaji wake,limekuja suala la kumsimamisha mkurugenzi wa bodi ya pamba nchini lakini mpaka ameingia waziri Christopher Chiza ndiye aliyethubutu kutumia dhamana yake kumsimamisha mkurugenzi huyo.Leo tena anatuhumiwa kuteua wajumbe wa bodi ya kahawa wakiwa hawana sifa za kuwa member wa bodi akiwa wizara hiyo hiyo ya kilimo,maneno haya yanazungumzwa bungeni,hansard ipo tunasubiri nini mpaka kumbeba mtu asiyebebeka kama kweli hana hisa na serikali hii ya awamu ya nne.Rais wetu msikivu tekeleza basi yale tuliyokutuma na kutoa dhana ya watu kuwa na hisa na serikali yako.
   
Loading...