Private detective/investigator (Mpelelezi binafsi) kwa sasa ni Fursa. Tuitumie!

klementos

Senior Member
Aug 29, 2017
105
753
Private detective/investigator (Mpelelezi binafsi) ni mtu ambae anaweza kukodishwa na mtu binafsi ,watu au taasisi kwa ajili ya kufanya upelelezi wa kesi fulani. Private detective/investigator(Mpelelezi Binafsi) mara nyingi huwa anafanya upelelezi kwa kesi za mtu kibinfsi na si za serikali.

Wajibu wao ni kukusanya taarifa mbalimbali kama vile upigaji wa picha,kudurufu nyaraka, kurekodi video/sauti za wahusika ambao wamepewa kazi za kufuatilia mienendo yao kwa siri ili kuziwakilikilisha kama ushahidi kwa watu waliowapa kazi au kutumika mahakamani, ila hawana mamlaka ya kukamata au kuwafungulia watuhumiwa kesi.

Kwenye mataifa ya wenzetu wapelelezi binafsi(private investigator) wapo kwa mujibu wa sheria. Sheria zimeainishaa utaratibu wa kupata vibali,miiko yao ya kazi na mipaka ya kufanya kazi zao.

Kuna vigezo vifuatavyo vinamwezesha baadhi ya nchi mtu kupata leseni ya kuwa mpelelezi binafsi ;-

· Raia wa nchi

· Miaka isipungue 25

· Ushawai kupata mafunzo ya kipolisi au polisi mstaafu

· Polisi

· Ujuzi usiopungua miaka mitatu

· Kutokuwa na historia ya uharifu

Kwa mataifa yalioendelea wapelelezi binafisi wapo na watambulika na Serikali na pia wanalipa kodi kwa ajili ya shughuli zao. Mwaka 1953 jimbo la Marekani -Pennsylvania lilitunga sheria ‘PRIVATE DETECTIVE ACT OF 1953,The Act of Aug. 21, 1953’’ Sheria hii iliweka utaratibu wa upatikanaji leseni, vigezo vya kupata leseni na sifa mwombaji.

Kwa upande wa Africa Afrika kusini wana makampuni mengi ya Private investigator (wapelelezi binafsi) kama Jackson's Private Investigations Unlimited, Cheaters Investigations Cc, na Lesward Private Investigations(Zimbambwe)

Wapelelezi binafsi wanaweza kuchunguza vitu vifuatavyo;-

Upelelezi maswala ya Bima

Makampuni ya bima huwa yana ajiri wapelelezi binafisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kubaini kama walalamikaji wenye bima waliounguziwa nyumba, magari au matukio ya wizi ili kujiridhisha kama madai yao ni sahihi au si sahihi, ili kuepusha udanganyifu.

Upelelezi maswala ya mahusiano/talaka

Wana ndoa baadhi huwa wanaajili wapelelezi binafsi kwa ajili ya kupeleleza mienendo ya wake/ waume zao kujua kama ni waminifu au lah, kwenye mahusiano yao na kutumia taarifa hizo kama ushahidi mahakani kwenye maswala ya talaka. Mara nyingi wapelelezi hawa utumia tekinojia aidha ya mobile surveillance,kuweka tracker kwenye magari au kutumia remote ca,mera kufanikisha upelelelzi wao.

Upelelezi maswala ya kifamilia

Wapelelezi binafisi wanafanya kazi ya kupeleleza wazazi wanaokimbia majukumu yao ya kulea watoto na kukimbilia Miji tofauti ili wasiweze toa mahitaji muhimu kwa watoto (Child support).Mama mzazi anaweza kuwatumia hawa ili Baba aweze patikana na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwani ni vigumu polisi wa serikali kufanikisha jukumu hilo kwani wanakuwa na majukumu mengi .

Upelelezi wa taarifa za mtu

Baadhi ya makampuni huwa yanaajiri wapelelezi binafsi kupeleleza taarifa za wafanyakazi wao ambao wamewaajiri au wanategemea kuwaajiri kwenye nafasi za juu ili kujua taarifa zao na mienendo yao kama sehemu walizofanyia kazi awali,walipozaliwa, mahusiano, taarifa zao za kibenki,kama wana matukio ya kiuhalifu awali na mali wananzomiliki lengo kuu ni kupata mtu sahihi na usalama wa makampuni yao tofauti na serikalini ambao wanakuwa na vitengo vya usalama kwa ajili ya vetting.

Upelelezi wa mali zilizopotea

Watu hawa pia huwa wanapewa kazi ya uchunguzi wa mali zilizopotea na kampuni/mtu binafsi ili kukusanya ushahidi utakaosaidia kupatikana. Zoezi la utafutaji wa mali zilizo potea mara nyingi ufanywa na askari ila baadhi ya watu kwa ajili ya usiri (privacy) huwa wanawatumia wapelelezi binafsi.

MIIKO YA KAZI ZA WAPELELEZI BINAFSI(PRIVATE INVESTIGATOR)

Sheria zimeanisha taratibu za kufanya kazi zao za kipelelezi ila kuna vitu ambavyo wanakatazwa kufanya ili kulinda haki za yule wanamchunguza kama vile udukuzi wa komputa,simu na taarifa za kibenki mpaka wafuatae taratibu za kisheria(subpoena).

Lazima wawe wamepata mafunzo ya kuweza kupambana na changamoto yeyote inayoweza kutokea wakati anapofanya majukumu yake ya upelelezi na kumlinda mteja wake.

Hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa kazi yao tu ni kupelelelza na kupata taarifa za mtuhumiwa, wenye mamalaka ya kukamata ni polisi.

FURSA ZILIZOPO KWA VIJANA WETU WANAOPATA MAFUNZO YA KIPOLISI /KIJESHI ENDAPO MIONGOZO/SERA/SHERIA ZINGEKUWEPO

Kwa Sheria zetu hapa Tanzania kada ya Private investigator haipo kwa mujibu wa sheria zetu. Lengo la kuandika makala hii naona kuna fursa mamalaka husika ikaweka utaratibu wa kuwatumia vijana wanaotoka mafunzo ya kipolisi na Jkt na kukosa kazi kwa kuweka miongozo/sheria, kulingana na ufinyu wa nafasi na bajeti kwa Serikali, wakapata fursa ya kujiajiri na kupunguza mzigo wa kuitegemea serikali au kujiingiza kwenye makundi ya kiharifu na kujiajiri kwenye kada hii.

· Mkampuni ya Bima wanaweza kuwatumia kwa ajili ya upelelezi ili kujiridhisha na madai ya wateja wao ili kupunguza udanganyifu.

· Kuondoa usumbufu wa Mtu binafsi kupeleleza mienendoya mke/mme/kimada badala yake kuajiri mtu kukusaidia kufanya kazi hiyo.

· Makampuni pia yanaweza kuwatumia kupeleleza mienendo ya watumishi wao wanaotaka kuwa promote wafanyakazi wao nafasi kubwa za juu.

· Watu binafsi kusaidia kutafuta wapendwa wao walipotezana siku nyingi

· Kusaidia watu wanaokimbia familia zao kwa kukwepa kuwahudumia na kukimbilia kwenye Majiji kama Dar-es-salaam,Mwanza, Arusha n.k

· Familia kuwatumia kufanya upelelezi wa DNA Kwa wale wazazi wanaokataa watoto wao ili kukusanya ushahidi na kuwabana mahakamani au kujiridhisha kabla ya kufungua kesi.


Klementos
 
Mvunja sheria hawezi kuijenga sheria bali atatunga sheria inayomlinda yeye.Tafakari unaitwa kituo cha polisi ili uisaidie polisi katika kufanikisha kesi zao lakini wewe unawekwa ndani sawa na mahabusu wengine kwa kigezo cha usalama wako hata kama uko salama.Polisi huyo huyo unayemsaidia ndio anampa taarifa mwalifu habari zako!.NADHANI TUNAHITAJI WAPELELEZI BINAFSI LAKINI SIO WAWE MAWAKILI WA KUJALI PESA KULIKO HAKI.
 
Mimi niliibiwa pesa nyumbani na mtu aliyewaleta watu hao nyumbani ni shemeji wa kike yaani dada yake mke wangu. Aliwaleta kama waganga eti wamtibu alikuwa anaumwa tumbo. Walipomaliza kumtibu wakamgeukia mke wangu kwamba awape hela zote na akawapa.
Je mpelelezi binafsi anaweza kunisaidiaje kuwapata watu hao maana shemeji na hao watu walishakimbia na hawajulikani walipo.
Msaada tafadhali.
 
Mimi niliibiwa pesa nyumbani na mtu aliyewaleta watu hao nyumbani ni shemeji wa kike yaani dada yake mke wangu. Aliwaleta kama waganga eti wamtibu alikuwa anaumwa tumbo. Walipomaliza kumtibu wakamgeukia mke wangu kwamba awape hela zote na akawapa.
Je mpelelezi binafsi anaweza kunisaidiaje kuwapata watu hao maana shemeji na hao watu walishakimbia na hawajulikani walipo.
Msaada tafadhali.

Kwa sheria zetu za tanzania, hairuhisiw but unaweza kufanya hvyo kwa siri kwa kumuajir mtu mwenye uwezo kiakili, kufanya ujasus kupepeleza hao wahun, so utampa details ambazo unazijua w kuhusu hao watu
 
Kwa sheria zetu za tanzania, hairuhisiw but unaweza kufanya hvyo kwa siri kwa kumuajir mtu mwenye uwezo kiakili, kufanya ujasus kupepeleza hao wahun, so utampa details ambazo unazijua w kuhusu hao watu
Hawo watu walishakimbia lakini wako hapahapa Tanzania. Ninachohitaji ni kuwapata tu...
 
Utaishia kupigwa risasi kwa Tanzania hii

Waandishi wa habari za uchunguzi wanakiona cha moto ndio itakuwa kwa private detective?
 
Ingekua safi sana kuna watu wamesomea Bachelor ya Law enforcement hapa Tanzania, wangejiajiri.
It's different rafiki sidhani kama wanafundishwa ku work undercover, surveillance na skills za namna hyo. Sijui kama kuna gadgets za kazi hyo wanafundishwa achiliambali silaha.
 
It's different rafiki sidhani kama wanafundishwa ku work undercover, surveillance na skills za namna hyo. Sijui kama kuna gadgets za kazi hyo wanafundishwa achiliambali silaha.
Bachelor ya Law Enforcement wanafundisha mambo ya investigation mfano cyber crime investigation na criminal investigation kwa kiasi fulani
 
  • Thanks
Reactions: vvm
It's different rafiki sidhani kama wanafundishwa ku work undercover, surveillance na skills za namna hyo. Sijui kama kuna gadgets za kazi hyo wanafundishwa achiliambali silaha.
Yes wamesomea hayo mambo and more than that....na weapons management pia.
 
Firm za namba hii zipo Hata Tanzania lakini kujulikana ndio shida. Hawana Uhuru wameaanza na wale kwenye shida za ndoa wanawahangaikia sana hasa wanawake ila shida akilegeza mkeo analiwaaaa
 
Back
Top Bottom