Private car: Je ni salama kusafiri mwenyewe up country

Mimi natoka Igunga via pori la ibembampazi,chunya to mbeya na Land Rover 109(mwarobaini)
Wewe kwenda hapo tu Arusha unajuiliza uliza hivi?tena rav4 model 2004.halaf unakaujuzi kaufundi hata ukipata Pancha unajua kupiga jeki na barabara lami tupu
Mkuu piga machine usiwe MTT wa mama gari ya Mgumu hairudi nyuma
Punda Afe lkn Mzigo,,,,,,,
 
Hakikisha gari haikosi kitambulisho chako,namba yako ya simu,maji ya akiba unaweza ukaweka carton 1 siti ya nyuma,maji ya emergency kama lita 5 hivi,kisu panga au sime,USB cable,Rungu,Tochi,Filimbi,Kiberiti,Pain killer kama Panadol,tairi ya akiba ya maana.Mengine tutakumbushana panapo majaliwa
Duuhh...anaenda kibiti au
 
Hakikisha gari haikosi kitambulisho chako,namba yako ya simu,maji ya akiba unaweza ukaweka carton 1 siti ya nyuma,maji ya emergency kama lita 5 hivi,kisu panga au sime,USB cable,Rungu,Tochi,Filimbi,Kiberiti,Pain killer kama Panadol,tairi ya akiba ya maana.Mengine tutakumbushana panapo majaliwa
Mkuu, huyu bwana kwani anaenda vitani?? :D:D:D
 
Kuna chalii ni fundi magari anatokaga Dar-Arusha kwenye saa 10 alfajiri...
By saa 3 asubuhi yupo Arusha mjini.. Muhimu uwe makini tu barabarani, jamaa anatembeza noah speed 140 hapo ndio wastan wake akipata mnyooko anakandamiza 160km/h
Kwa barabara ZA TANZANIA NA SPEED HIYO UNATAFUTA KABURI
 
Endesha asubuhi mpaka jioni. Malori yaliyoharibika huegeshwa kiholela barabarani bila tahadhari yoyote kwa watumia barabara wengine.
 
Mambo vipi wakuu...

Nimeona nililete hili swali hapa coz mara nyingi limekuwa likinisumbua sana... Na hii inatokana na historia yangu ya huko nyuma mana gari ya kwanza kuimiliki ilkuwa ni spana mkonon/ESCUDO.. Yana niliujua ufundi pasipo kupenda ilifikia kipindi nikakosa kabisa mzuka na gari kwa kero nilizokuwa naexprience...

Zile effects leo zimenifanya nije kuuliza hapa but gari niliyonayo now ni RAV4, 2004, 1750CC, VVTi Mzigo ni wa hivi karibuni..

Safari zangu ni mara 1 either 2 kwa mwezi Dar- Arusha- Mwanza then Dar

Nimezingatia matairi, break, makorokoro ya alama, fire, spana,
Belt, jack n.k yote yapo

Nataka nitoke nikiwa mwenyewe kwa kuanzia Dar Arusha na ndyo long safari yangu ya kwanza... Je kuwa mwenyewe kwa safari yote hiyo ni salama???

Sent using Jamii Forums mobile app

Are you real asking this Question? AU UNATAKA KUTUAMBIA UMENUNUA RAV 4?
 
EN
Kuna chalii ni fundi magari anatokaga Dar-Arusha kwenye saa 10 alfajiri...
By saa 3 asubuhi yupo Arusha mjini.. Muhimu uwe makini tu barabarani, jamaa anatembeza noah speed 140 hapo ndio wastan wake akipata mnyooko anakandamiza 160km/h
Enzi za ujana wangu nilikua natemba 180KM/H nikiwa na SUBARU, nashukuru MUNGU leo hii bado ni mzima
 
Kwa wastani kila baada ya masaa manne Magogo huwekwa njiani .na watu wasiojulikana na kila baada ya masaa 2 tochi za za yangeyange beware of road!
 
Siku moja nilikuwa natoka Dar kwenda mkoani, kufika maeneo ya Mbezi nikajikuta nimeshasinzia na kuanza kuota ndoto nzuuri! Kuja kushtuka nakumbuka kuwa naendesha gari! Ikabidi nipaki pembeni fasta nikalala kidogo. Nahisi kwa muda ambao nilikuwa nimelala, malaika wa Bwana alishika usukani maana isingekuwa hivyo, ningeshajikuta mtaroni!
 
Kitu muhimu kabisa ndg ni kujua uimara wako upo wapi na udhaifu wako upo wapi kuhusu mwili wako, kwa mfano kama unajijua kabisa usingizi wakati wa usiku huwa ni shida kuuzuia kwa hali yoyote ile, basi avoid kusafiri usiku na piga mashine mchana. Kutembe mwenyewe si shida, ila kama unauwezo wa kuwa na company ni bora na salama zaidi. Mengine uliyo andika ya usalama na ubora wa gari, pamoja na kuzingatia sheria na alama za barabarani ni lazima kwa safari salama.
 
Kama hakuna anayekufuatilia nyuma na Toyota Land Cruiser nyeupe au Premio ni salama kabisa kusafiria mwenyewe kwenda huko mashinani / upcountry / mikoani Mkuu.

Haa haa:D:D:D haa....

Sasa wewe wataka kumfanya mwenzio akaanze kupata tiba ya kisaikolojia India kwa mshtuko na woga... !!
 
Ukipatwa na majanga ndio utajua nlioandika hapo kina umuhim gani

Uko sahihi sana mkuu...

Mimi kisu ninacho na natafuta kibali cha kumiliki mkuu wa kuku ama SMG kabisa na itakuwa chini ya siti...

Siko tayari kufanywa kama alivyotendwa Tundu Lissu....

Laiti jamaa angekuwa na hii kitu, angepata nafasi na yeye pengine angeweza kumlaza chini hata mmoja wa majahiri hayo..!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom