Prisons FC yapewa ushindi wa mezani baada ya Ruvu Shooting kushindwa kuleta Ambulance Uwanjani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Timu ya Tanzania Prisons imepewa ushindi wa alama tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliokuwa ufanyike February 11, 2020 baada ya timu ya Ruvu Shooting ambao ni wenyeji wa mchezo kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani.

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la soka la TFF imeeleza kuwa uamuzi huo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14 (2|) jambo lililosababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri dakika 30 bila gari hilo kutokea.

Mchezo huo ulikuwa wa ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), namba 205, kati ya Tanzania Prisons FC na Ruvu Shooting.
FB_IMG_1581692074340.jpeg
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Alichosema Masau Bwire akihojiwa na radio moja nchini;

"Ambulance ilikuwepo, lakini dakika chache kabla mchezo kuanza iliondoka kwenda kumbeba mgonjwa na kumpeleka Hospitali ya Lugalo ambapo ilirudi tena uwanjani saa 10: 34".

Ikiwa ni dakika 4 baada kusubiriwa 30 kwa mujibu wa kanuni, ambapo mwamuzi alivyunja mchezo.
 

ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
4,214
2,000
Timu ya Tanzania Prisons imepewa ushindi wa alama tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliokuwa ufanyike February 11, 2020 baada ya timu ya Ruvu Shooting ambao ni wenyeji wa mchezo kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani.

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la soka la TFF imeeleza kuwa uamuzi huo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14 (2|) jambo lililosababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri dakika 30 bila gari hilo kutokea.

Mchezo huo ulikuwa wa ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), namba 205, kati ya Tanzania Prisons FC na Ruvu Shooting. View attachment 1357589
Taratibu zifatwe piga nyundo kenge hao
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,650
2,000
Mikia wataanza kuhonga madreva wa Ambulance. Hawashindwi kitu. Ya marefa imebuma.
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,164
2,000
Kwa mwendo huu subirieni timu za Kariakoo zikianza kuleta figisu na kupata point za mezan ndio mtajua chungu yake hii kanuni
 

Mkale

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
1,136
2,000
mechi haikuchezwa so hasara imeenda kwa mzamini mkuu w ligi ,hasara kwa wazamini wa redio n TV zilizo plan kurusha matangazo y mechi husika.. next time no uzamini kwnye ligi n vilabu vitaanza kulia njaa.
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,650
2,000
Wakati mwingine tunazidisha ujuaji.

Hii ni kanuni na imekubaliwa na timu zote. Kikubwa nimeshukuru tukio halikuzihusu vigogo wa Kariakoo.

Sababu za Masau Bwire zimejaa uswahili. Eti emergence, ubinadamu. Wakiruhusu hizo emergency, zitakuwepo kila mechi. Sisemi yule mgonjwa asingekimbizwa kupata huduma. Mipango yao mibovu, full stop.

Vigogo wa Kariakoo wakicheza mikoani, timu mwenyeji wanavuna mpunga wote. Nayo ni kanuni kama hii kanuni ya Ambulance. Zamani kila timu ilikuwa inajitafutia. Yanga ilisaidia wa Mikoani kuitumia. Sasa imekuwa kanuni. Kila mwenyeji afanye hivyo.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,658
2,000
Atakua nayo matatu mkuu wakati anasubiri jamaa wengine wazingue afunge tena kupitia TFF.

macson
Na ntafunga sana tu, maana timu itakayotaka kupanga tokeo hawaleti ambulance uwanjani refa anafuta game mimi naenda kuchukua magoli wengine wachukue point
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom