Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,480
- 5,506
Sina Takwimu za uhakika za idadi ya Wafungwa Nchini ila nina imani kabisa katika Magereza yetu tunaweza kuwa na idadi ya Wafungwa ambao wanaweza kuzalisha bidhaa mbalimbali na kuchangia katika ujenzi wa uchumi.Natambua kwamba mtu anapokuwa kifungoni anakuwa anatumikia adhabu kwa kosa alilofanya lakini hii haimaanishi kwamba maisha yake hayana maana na kwamba hawezi kufanya shughuli za uzalishaji.
Kama taifa tunaweza kuwa na Mfumo ambao unawawezesha wafungwa kupata malipo kabisa kwa kazi za uzalishaji wanazofanya wanapokuwa gerezani.Kipato hiki kinaweza kutumika kuwasaidi wafungwa pindi wamalizapo kifungo na pia kinaweza kusaidia katika kuwapatia mahitaji wategemezi wao pindi wawapo kifungoni.
Baadhi ya Shughuli zinazoweza kufanywa na wafungwa ni pamoja na shughuli za KILIMO na UFUGAJI,Uchimbaji wa Kokoto na Mchanga,Uzalishaji wa Nguo,viatu na bidhaa za aina hio.Katika kuamua mfumo wa malipo inaweza kutumika kanuni ya minimum wage ya sekta husika.
Ni muhimu sana Walipwe kwa kazi wanazofanya ili kuwajengea utu,hadhi na nidhamu.
Tukifanikiwa katika hili tutajenga jamii ya kipekee sana ambayo inathamini utu na tunaweza kuchangia kushusha kiwango cha uhalifu hapa nchini.
Tujadili hapa kwa kina namna ambavyo tunaweza kuboresha mfumo wetu wa Magereza na kuongeza uzalishaji wenye Tija.