Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi?

G.25

G.25

JF-Expert Member
1,266
2,000
Alisema kabla hilo ndilo atapenda kuona linafanyika na aliongelea juu ya Chunya yeye na PM. So mpango wanao na labda pesa ndio hizo watatumia, natumaini kiasi umetaja walipojenga cha huko ndicho ambacho kinaendana na sasa.. la sivyo itabidi wasubiri hadi lini kupata zaidi au waendeleze mengine tu.
Samahani Coco we ni MTU wawapi? Halafu naomba unisomee ulichoandika, sijaelewa"
 
D Metakelfin

D Metakelfin

JF-Expert Member
2,884
2,000
Itabidi nipapende ulipotoka mkuu. Km vitu obvious unavikataa na kuwa km vile huoni.Ni wazi huko kwenu nikenda waibia hata aje nani hawezi wabadilisha nia kuwa nawaibia. Sasa hili povu lote nini wakati fact ni kwamba hakuna hela ya fine wala hamna ushindi.Hela ya nia njema ni msaada tuta kwa partner wako km mwezi hauendi, anafulia hovyo hovyo. Theories zote ni ujinga mtupu.
Sijaelewa hata ulichoandika
 
Van persie

Van persie

JF-Expert Member
1,098
2,000
Hizi ni kama 400km za lami.So tujenge Kama 200km na zinazobaki tununue Meli 2 ziwa Victoria.Kama kweli tutalipwa,kwa maana ngoma inaenda kwa kubadilika kwa Kasi.
 
K

kibaravumba

JF-Expert Member
5,359
2,000
Mimi ninachojiuliza kwan serikali haiwezi kuwekeza kwenye hayo machimbo ya dhahabu, tukachimba wenyewe? Mpaka tutegemee mzungu kila kitu?

Kwanini machine wanazotumia Barick serikali isizinunue tukaanza uwekezaji kwenye sehemu.moja moja tukachimba wenyewe kwa faida?

Kama akija mwekezaji.anataka ubia basi tutampa masharti yetu kama tunavyotaka sisi na si kama wanavyotaka wao. Mali yetu.na bado tupelekeshwe?

Tukiwezekeza wenyewe tutachimba taratibu kwa faida na nchi itafaidika tofauti na kuwaachia hawa mabeberu wanapeperushia utajiri wetu nje.

Afadhali tena hata kama ingekuwa ni wazawa wanachimba hata kama hawajalipa kodi lakini hiyo hela ingebakia humu nchini. Ingewekwa bank, watu wangepata mikopo nafuu. Au wangewekeza hata kwenye viwanda na biashara nyingine tofauti ajira zingekuwepo na watu wengi kipato kingeinuka.

Wasitutishe wachape mwendo watuachia madini yetu, tutayafaidi wenyewe na vizazi vijavyo. Period!!
Unaongea kwa hisia sana!Ungeujua tu ukweli sidhani kama ungetoa maoni haya.Kifupi serikali haiwezi kuchimba yenyewe.Kama imeshindwa tu kuchimba mabwawa na kuweka miundombinu ya umwagiliaji,inawezaje kufanya shughuli ya uchimbaji wa dhahabu unaohitaji uwekezaji mkubwa unaolipa baada ya miaka zaidi ya kumi?
Hii biashara si rahisi kama unavyodhani kwani hata hawa wamiliki wanapata faida kwenye uwekezaji wa hisa katika makampuni ambayo wao pia ni wateja wakubwa mf.makampuni ya kutengeneza mitambo mizito n.k
Technolojia,utaalamu na nidhamu ya usimamizi wa uchimbaji hasa kwa kufuata principles za usalama kwanza ni utamaduni mgeni kabisa kwetu.Wao hawakubaliani na misemo kama eti "ajali haina kinga"Wao wanaamini ajali zote zina kinga isipokuwa zinazotokana na majanga ya asili kama tetemeko la ardhi n.k.Kumbuka iwapo watanzania tutachimba wenyewe,ajali zitakuwa nyingi maana akili zetu tunazijua wenyewe!Na kwa hiyo bei ya dhahabu itakuwa chini sana.Wazungu ndio wanunuzi wakubwa wa dhahabu,nao huwa hawanunui dhahabu ya damu!
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
14,379

great
 
L

lebabu11

JF-Expert Member
1,950
2,000
Pascal,

Umechanganya kidogo mambo, au labda nieleweshe vizuri:
Bomba la mafuta toka Uganda tumeweza nini? Lile siyo la kampuni binafsi? Au serikali ina share?
 
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
6,196
2,000
Alisema kabla hilo ndilo atapenda kuona linafanyika na aliongelea juu ya Chunya yeye na PM. So mpango wanao na labda pesa ndio hizo watatumia, natumaini kiasi umetaja walipojenga cha huko ndicho ambacho kinaendana na sasa.. la sivyo itabidi wasubiri hadi lini kupata zaidi au waendeleze mengine tu.
aisee...
 
Mzee wa hat-trick

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
1,737
2,000
Mimi ninachojiuliza kwan serikali haiwezi kuwekeza kwenye hayo machimbo ya dhahabu, tukachimba wenyewe? Mpaka tutegemee mzungu kila kitu?

Kwanini machine wanazotumia Barick serikali isizinunue tukaanza uwekezaji kwenye sehemu.moja moja tukachimba wenyewe kwa faida?

Kama akija mwekezaji.anataka ubia basi tutampa masharti yetu kama tunavyotaka sisi na si kama wanavyotaka wao. Mali yetu.na bado tupelekeshwe?

Tukiwezekeza wenyewe tutachimba taratibu kwa faida na nchi itafaidika tofauti na kuwaachia hawa mabeberu wanapeperushia utajiri wetu nje.

Afadhali tena hata kama ingekuwa ni wazawa wanachimba hata kama hawajalipa kodi lakini hiyo hela ingebakia humu nchini. Ingewekwa bank, watu wangepata mikopo nafuu. Au wangewekeza hata kwenye viwanda na biashara nyingine tofauti ajira zingekuwepo na watu wengi kipato kingeinuka.

Wasitutishe wachape mwendo watuachia madini yetu, tutayafaidi wenyewe na vizazi vijavyo. Period!!
Mbona unaongea pumba mkuu..??? Unatumia nini kufikiri...??

Kwani umeambiwa na nani kwmb hao barrick wanauza mashine zao..??? Na hata kma wanauza, unadhani ni milioni 2 eeh...!!??

Unafikiri kwa uongozi huu na kwa uchumi huu, serikali inaweza ikawa na uwezo wa kununua mashine hizo na mambo mengine ya maendeleo yakaenda sawa..??

Ukichimba huo mchanga utachenjulia wapi?? Na hela ya kununua mashine ya kuchenjulia utaipata wapi wakati utakuwa umetumia gharama kubwa sana kununua hizo mashine..?? Au ndo utausafirisha kwenda nje ya nchi na kulipia gharama za kuchenjulia huko huko..???

Umewaza kuhusu vipuri/ spare parts za hizo mashine..?? Wao kwa kuwa wana hela na uzoefu, ni rahisi kupata hizo spares whenever they're needed, so wat about us..?? Unafikir tutakuwa na uwezo wa kuwalipa wataalam wa hizo mashine na kuzifanya ziweze ku-run kila siku..?? Na ikiharibika tusubir hazina itoe hela ya kuagiza spare kama ni Japan au wapi..?? Au unadhani spare zake zinapatikana dukani kwa mangi mtaa wa pili...??

Hayo ni machache ambayo naamini hukuyafikiria, ila uchimbaji madini sio uwekezaji mdogo. Ni gharama sana na kwa uchumi wetu bado. Ni bora sana hta tusingedai tulichoibiwa kabla ili tuweke terms upya na tuanze upya tukiwa na amani na uhakika wa almost 80% wa kufaidi faida na hasara za mchimbaji.

Tatizo ni kwamba tunaweka kila kitu kisiasa, na kwa sababu watu wa upinzani wametoa angalizo kabla, basi tunawaona sio wazalendo na kuwabeza. Hivyo kinachofanyika ni kama kuwaonesha TUNAWEZA, na ndio maana hata ktk hotuba zake mkuu anaonesha chuki ya waziwazi dhidi ya upinzani. Ni kama waimba taarabu vile wanavyopigana vijembe. Bado tuna safari ndefu sana mkuu.

ACHA KWANZA TUKOMAE NA WANAOFICHA SUKARI NA TUFANYE TU SIASA ZETU ZA MAJITAKA.
 
S

singojr

JF-Expert Member
4,244
2,000
Smelter zinahitaji umeme mkubwa je tunao? Kiwango cha madini kwenye nakinikia kama maprof walikipika kufurahisha umma unadhani watakubali inunuliwe smelter halafu tuchenjue hewa? Serikali sahivi haina hela kabisa yaani imefulia totally unadhani bado smelter ni priority wakati hela ya mishahara hakuna
 
Sigara Kali

Sigara Kali

JF-Expert Member
2,913
2,000
Unaongea kwa hisia sana!Ungeujua tu ukweli sidhani kama ungetoa maoni haya.Kifupi serikali haiwezi kuchimba yenyewe.Kama imeshindwa tu kuchimba mabwawa na kuweka miundombinu ya umwagiliaji,inawezaje kufanya shughuli ya uchimbaji wa dhahabu unaohitaji uwekezaji mkubwa unaolipa baada ya miaka zaidi ya kumi?
Hii biashara si rahisi kama unavyodhani kwani hata hawa wamiliki wanapata faida kwenye uwekezaji wa hisa katika makampuni ambayo wao pia ni wateja wakubwa mf.makampuni ya kutengeneza mitambo mizito n.k
Technolojia,utaalamu na nidhamu ya usimamizi wa uchimbaji hasa kwa kufuata principles za usalama kwanza ni utamaduni mgeni kabisa kwetu.Wao hawakubaliani na misemo kama eti "ajali haina kinga"Wao wanaamini ajali zote zina kinga isipokuwa zinazotokana na majanga ya asili kama tetemeko la ardhi n.k.Kumbuka iwapo watanzania tutachimba wenyewe,ajali zitakuwa nyingi maana akili zetu tunazijua wenyewe!Na kwa hiyo bei ya dhahabu itakuwa chini sana.Wazungu ndio wanunuzi wakubwa wa dhahabu,nao huwa hawanunui dhahabu ya damu!
Umemjibu vizuri sana hilo jinga,bogasi la CCM
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,653
2,000
Paskali, kwa uandushi wako na heshima yako, usishabikie kabla ya uhakika usio na mashaka. Lazima usome watu unao deal nao. Unajua kabisa kuwa watu wanamwogopa boss, hivyo watamwambia analotaka kulisikia kulinda mkate wao. Kuna uongo sana awamu hii, hivyo ingelikuwa mimi ningelisubiri kabla ya kusherehekea/kuandika 300m US$ in the affirmative or negative. Ningeliandika hoja "fikirishi" tu! na si vinginevyo. Sasa wamesema hawana hela ya kulipa, unasemaje sasa? kadagala1
Kwani Acacia wamesema watatulipa hizo dola milioni 300 ?
Tunawezaje kupangia kuzitumia pesa za kishika uchumba, wakati wanaume wenye hizo pesa hawajasema kama watazitoa?
Wakuu Retired na Zanzibar ASP, kishika uchumba ni fedha zozote au zawadi mwanamume anampa mpenzi wake au kupeleka kwa wazazi wa mwanamke kuonyesha interest na sio mahari, hiki kishika uchumba huwa hakirudishwi hata kama utakuta mwali sii wako, ila kishika uchumba kikitolewa kwa solid promise, kinageuka legal kwa kutengeneza a legitimate expectations, hata rais wetu mlimsikia alivyohamasika nazo na kuanza kuzipangia matumizi, hivyo ikitokea wasitoe tunaweza kabisa kuwashitaki kwa kutumia kipengele kinachoitwa 'Promissory Estoppel' ambacho kinasisitiza ukiahidi, hata bila maandishi yoyote, lazima utimize hiyo ahadi.

Paskali
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,653
2,000
Nitarudi kurudi kuja kujadili kwa kina hapo baadae!! Lakini labda nikuulize jambo moja tu Pascally, kwanini suala la bomba la mafuta la Uganda nalo umeona tumeweza wakati ule mradi sio wa kwetu?! Manaka kutokana na mpangilio wako wa hoja, umejikita kwenye suala la vipaumbele na kama ndivyo, suala la bomba la mafuta la Uganda ni kipaumbele cha Uganda na Total; sie wengine hayo yametukuta just by chance!!!

Aidha, wacha niseme kidogo kuhusu hilo la USD 300 Million! Hizo USD 300M naziogopa kama ukoma!!! Hofu yangu isiwe ni janja ya Barrick Gold kutaka hatimae waruhusiwe kuuza makinikia na wakichachukua chao; wafungashe virago na kutuachia maandaki yetu!!!

I hate to say this but there's no way Acacia wanaweza kulipa hata 10% ya kile tunachosema tunawadai; NO WAY! Suala hili nimekujibu kwa kutumia data kwenye ile thread yangu uliyoniambia kwamba hiyo USD 300M ni kishika uchumba!!
Mkuu Chige, I share your concern, kuna mahali nimesema "I fear the Greeks, especially when they bring gifts", watu tunawadai ma trilioni kwa kutuibia, kisha hawazungumzii lolote kuhusu deni letu, bali wanatuletea zawadi ya tujisent, bila kusema ni zawadi ya nini!, halafu wewe unashangilia, kama sio uzuzu ni nini?.

Paskali
 
Upepo wa Pesa

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
14,553
2,000
Wakuu Retired na Zanzibar ASP, kishika uchumba ni fedha zozote au zawadi mwanamume anampa mpenzi wake au kupeleka kwa wazazi wa mwanamke kuonyesha interest na sio mahari, hiki kishika uchumba huwa hakirudishwi hata kama utakuta mwali sii wako, ila kishika uchumba kikitolewa kwa solid promise, kinageuka legal kwa kutengeneza a legitimate expectations, hata rais wetu mlimsikia alivyohamasika nazo na kuanza kuzipangia matumizi, hivyo ikitokea wasitoe tunaweza kabisa kuwashitaki kwa kutumia kipengele kinachoitwa 'Promissory Estoppel' ambacho kinasisitiza ukiahidi, hata bila maandishi yoyote, lazima utimize hiyo ahadi.

Paskali
Kwani ACCACIA wamesema wanatoa ela?

Sasa kama msimamo wao ni ule wa jana kwanin unapanga matumizi kwa pesa ambayo huna??
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,653
2,000
Kwani ACCACIA wamesema wanatoa ela?
Sasa kama msimamo wao ni ule wa jana kwanin unapanga matumizi kwa pesa ambayo huna??
Accacia ni cha mtoto tuu, sisi tunazungumza na baba yake, mwenye mali, ndie aliyeahidi hicho kishika uchumba.

Paskali
 
maonomakuu

maonomakuu

JF-Expert Member
2,522
2,000
Tatizo hilo ni la kifalsafa katika mfumo ambao msingi wake wa kidhana ni kwamba mkubwa hatiliwi shaka, na mambo yalivyo ndivyo yalivyo, na hakuna bora zaidi ya yalivyo.
 
maonomakuu

maonomakuu

JF-Expert Member
2,522
2,000
Tusipoondoa dhana ya kulinda kiti cha Urais kuwa ni CCM tu na watu kupenda vyama vyao kuliko nchi tusubiri Sana many years. Namaanisha hatufanyi kazi kama kuwainua maskini bali kujisifu kwa ajili ya vyama lazima hata ukifanya jema watu wanaona mbaya kwa ajili ya upenzi wa vyama

Hakuna aliye na nia ya dhati kuwakwamua wakulima,Kikwete alijaribu lakini aliyeko hana mwelekeo huo wa wakulima

JPM Nahisi atashindwa zaidi kwa sababu anataka kufanya miradi mikubwa Sana ambayo watu maskini hawatanufaika nao kwa sehemu kubwa.

Makinikia hata sitaki kuyaongelea maana ripoti zote mbili na majadiliano ni full contradiction.
Mungu ibariki Tanzania
 
Forum statistics

Threads
1,424,631

Messages
35,068,801

Members
538,026
Top Bottom