Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado hatujawa na tekinolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.
Kwa upande wake Prince Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na pia Prince William amemualika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.
Makamu wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.
Chanzo: Mpekuzi
Pia soma >Makamu wa Rais kumwakilisha Rais Magufuli kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola