prince bagenda,shankupe wa mafisadi;tuwe makini nae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

prince bagenda,shankupe wa mafisadi;tuwe makini nae

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Mar 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa habari 13 wa vyombo mbalimbali, wametangaza kumpeleka mahakamani Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, huku wakidai anahujumu vyombo vya habari vichanga visijiendeshe.

  Wanahabari hao ambao Mengi alitangaza hivi karibuni kuwafungulia mashitaka akidai wanamchafua, wao pia waliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kwamba watafungua kesi Machi 23 mwaka huu, ambayo pamoja na mambo mengine, wanataka athibitishe kama wao ni mafisadi kama alivyodai kwenye magazeti yake.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Waandishi hao, Prince Bagenda, alisema nia ya Mengi kuwaburuta mahakamani ni kutaka kuwadidimiza kimauzo. Pia walisema watamshitaki Mwanasheria Michael Ngalo wa Kampuni ya Uwakili ya Ngalo &Company kwa kuwaita mafisadi wakati akitangaza azma ya mteja wake (Mengi).

  Alisema hivi sasa wanashindwa kupata matangazo kutoka kwa watu mbalimbali baada ya magazeti yao kutajwa kuwa yanamilikiwa na mafisadi, jambo ambalo alisema si kweli. “Hii ni vita ya kibiashara, soko linaingiliwa na hatupendi vyombo vya habari vichanga viingiliwe, hivyo tunamtaka athibitishe kama kweli sisi ni mafisadi.

  “Kama ilivyokuwa awali, ingawa ametushitaki kwa kumchafua na sisi tunamshitaki kwa kutuita mafisadi nasi pia atulipe fidia,” alisema Bagenda. Bagenda alikishutumu Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) kuwa hakiwafai wao kama wamiliki wa vyombo vidogo vya habari na hivyo wameamua kuanzisha chao.

  Kwa mujibu wa waandishi hao, katika kesi ambayo wanaendelea kushughulikia mchakato wake, wanataka walipwe Sh bilioni 100 kwa maana ya Sh bilioni 50 kwa magazeti matano kila moja Sh bilioni 10. Lakini pia Sh bilioni 50 zingine kwa waandishi, wahariri na wamiliki ambao wanamlalamikia. Magazeti hayo ni Tazama, Taifa Tanzania, Nyundo, Sauti Huru na Umma Tanzania.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  amekuwa akihongwa na mafisadi kuandika mambo yaanayowachafua wale wanaoshughulika na mafisadi........
   
 3. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bagenda tamaa sana yule mzee.Anapenda sana pesa kuliko utu wake.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Mar 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mr. Impossible unao ushahidi wa hizo hongo alizokuwa akuipewa huyu Bagenda kama usemavyo?. usijeingizwa kwenye kesi mkuu
   
 5. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  baadhi ya waandishi ni Vigeugeu,PB na kasanga tumbo walikuwa wapinzani wa kweli lakini ufisadi umeshawapofusha
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani ni hatua nzuri kwani itatoa fursa kwa wanaotuhumu kuthibitisha ukuwadi wa ufisadi wanaoutuhumu kwa watu hawa
   
 7. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Hivi kila anayemsema Mengi amehongwa na ni fisadi? Hivi Mengi yeye anaowasema huwa hawajisikii vibaya kama yeye? Please acheni kumdekeza huyo mzee ambaye anataka aonekane kama serikali kwa Tanzania.
   
 8. r

  rizikius New Member

  #8
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusema ni rahisi lakini kuthibitisha mara nyingi huwa ni vigumu sana,sasa ni muhimu kufanya utafiti zaidi ili kujua ukweli wa mada yetu.
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  jamani huyu mzee inawezekana simsemei,lakini sikuhizi siku nzima anashinda kwenye ofisi za karamagi pale oppossite na crdb bank holland karibu na british caounsel akitafuta umbea,haya ndio maisha ya kutotengeneza maisha mapema mwisho unafia kwenye mikono ya dhambi...kumchafua mwenzio sio dili

  wewe unaesema mengi tunamtetea anavyowasema wenzake;na wewe unao ushahidi...ama

  1/))JE KARAMAGI AZIIDI KUWADANDIA WAKE ZA WATU!!SI KWELI

  2)JE MASHA AKUKUTANA NA WALE WAHUNI WENZAKE GINIVA??

  3))KWANI SIRI WE UJUI WAZIRI ANAEMFANYA MWENZIO UNYUMBA

  JIBU THEN TUENDELEE
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Prince Bagenda alikuwa mpambanaji mzuru lakini pesa imendhalilisha mpaka amekuwa kibarua wa wezi kama alivyo Kaborou pia; tumuombe mwenyezi amnusuru Zitto Kabwe kwani nae pesa imemroga na hiyo inajionesha kwani siku hizi anavaa designer Shirts na tie zake ; ahsante Dowans kulalek wallahih!!
   
  Last edited: Mar 18, 2009
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Zitto Kabwe kwani nae pesa imemroga na hiyo inajionesha kwani siku hizi anavaa designer Shirts na tie zake ; ahsante Dowans kulalek wallahih!!

  huyo alishaanza kunuliwa na chadema/sisiemu tangu akiwa chuo;na ndio maana mgomo wowote chanzo zitto basi atakaeumaliza yeye mwenyewe na wote wanafyata
  hili la dowans lisikushangaze ndugu yangu; .....kila sehemu """"WIZI MTUPU"""
   
 12. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MZee hii ya tatu sijaijua kidogo,Naomba uni PM
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Huyu Bagenda alinunuliwa tangu miaka ya nyuma.
  Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, huyu bwana alikuwa mwandishi katika gazeti la Rai enzi hizo (sina uhakika kama bado anaadikia huko) ambalo lilitumika sana kuwapamba wanamtandao na kuwachafua wasio wanamtandao wakati wa kampeni mwaka 2005. Baadaye akaandika kitabu kumpamba JK. Kwa miaka hiyo, waandishi ambao walikuwa pro mtandao kutoka katika magazeti hayo walikuwa ni Bagenda, Salva (aliyepo ikulu sasa) na bw John Bwire. Ikumbukwe kwamba magazeti hayo yalitumika sana kumchafua waziri mkuu wa wakati huo ndugu Sumaye, kwamba kanyang'anya wakulima mashamba kule Morogoro, na Malecela, kwamba ni Mzee hafai kwa urais.Kwa hiyo kazi ya kuchafua wenzao hawajaanza hivi karibuni.


  Hapana.

  Hakuna anayemdekeza Mengi wala kumuonea huruma. Kuna makala zipo hapa JF ambazo zimechambua mema na mabaya yake yote, pekua katika search hapo juu na usome jinsi Mengi alivyo. Hapa JF hakuna kitu kinafichwa.


  Huwa wanajisikia vibaya, kwa sababu nao ni binadamu wenye mapungufu kama alivyo Mengi, lakini kama wanafanya mambo yasiyoleta maendeleo unataka Watanzania wakae kimya!
  Please wake up!
   
Loading...