Primary school!! Ilikuwa burudani kwangu

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,585
5,758
Salaam wana Jf.
Wakati tukiwa primary, ilikuwa kila siku asubuhi tunakimbia mchakamchaka, tunaimba nyimbo za umoja na mshikamano. Ilipendeza sana,.
Je wewe unakumbuka tukio gani wakat ukiwa primary level?

Mimi nakumbuka kabla ya kumwamkia Mwalim, tunasema haya
''Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Shikamoooooo mwaaalim!!!

Mimi nakumbuka kabla ya kumwamkia Mwalim, tunasema haya

''Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora. Shikamoooooo mwaaalim!!!

sisi tulianza hivi "kazi ni kipimo cha uhai Shikamoo Mwalimu"
ilipendeza sana.

Siku ya kufanya mtihani wa Darasa la saba kama siku ya leo terehe 7/9/2011 lakini mimi nilifanya tarehe 23/9/198.Na mara nying ilikuwa inakuwa siku ya jumatano tu.Ilikuwa ni siku moja masomo matatu yaani Hisabati,Lugha na Maarifa ya Jamii.

namkumbuka mwalimu wangu wa hesabu. NIliamini hakuna mtu mwingine anayejua hesabu kama yeye zile za kipenyo, nusu kipenyo, Pie -3.14 Alikuwa anazishuka mno hasa akivuta ganja. Alinifanya nisiogope hesabu kabisa katika maisha yangu!! I will never forget him.

mi nakumbuka mdingi alikuwa na hotel kwa hiyo kila siku nilikuwa naenda na kiloba cha halfkeki shuleni mpaka wakanipachika jina la ringo maafkekii,
nilikuwa nahonga kuanzia namba asubuhi,kufanya usafi kikosini mpaka mwalimu wa darasa.
hahahaha.. nakumbuka mbali kweli.

mie primary nimemiss ugomvi na boys,nilikuwa mwembamba but i had mikwara na uchokozi mpaka basi!na walimu walikuwa wananipenda,so hata nikisemewa walikuwa hawaamini.

Nakumbuka shule ya msingi, choo kilikua cha shimo na mlango ni gunia..... si unajua vijijini kuchambia ni magunzi enzi hizo au mlango wenyewe kwa maana ya gunia. Ukiingia chooni ule mlango wetu (gunia) kila sehemu lina kinyesi.... lakini utajidai kuna sehemu ambayo ni safi na utachambia hapo..... Najiulizaga kungekua na magonjwa km siku hz sijui ingekuwaje........ I still have those sensational memories.......

Mi nakumbuka enzi zile pale Meru primary, tulivyokuwa tunatoroka vipindi kwenda kuvua samaki feki pale Mto wa Naura, vipindi tulivyokuwa tunaescape zaidi ni, Siasa, Sayansi kimu na Hesabu teh teh te te te teee

Nakumbuka hukooo Buhangija primary, maeneo ya Shinyanga, mwalimu wa darasa anakuwa hajaingia darasani siku kadhaa kucheck mahudhurio, saa ya kuita majina kama ulihudhuria siku zote unatakiwa kuitika JUZI, JANA na LEO.

Tehe tehe tehe..................................

Mie nilikuwa Mughanga Singida. Nilimtongozaga mwanafunzi mwenzangu kwa barua ya kiingereza, ile nampa tu, ticha kaona, akamfuata demu na kuichukua ile barua. Akaisoma kisha akatoka zake. Dak 15 baadaye akaja kiranja mkuu akanambia naitwa kwa mwalimu Mkuu. Nikajua leo nimekwisha, kumbe walifurahi mtoto wa darasa la nne anajua kiingereza. Nikapewa daftari 12 na kompasi. Daftali sita nilimpa yule demu, ila nakumbuka nilirudi nyumbani na bikari tu, teh teh teh

Mi nakumbuka enzi zile pale Meru primary, tulivyokuwa tunatoroka vipindi kwenda kuvua samaki feki pale Mto wa Naura, vipindi tulivyokuwa tunaescape zaidi ni, Siasa, Sayansi kimu na Hesabu teh teh te te te teee

duh ninakumbuka walimu waliokuwa wametoka JKT walikuwa wakali na wanatupigisha kwata,nakumbuka jina la utani nililopewa TESHA kwakuwa mfupi kuliko wote darasani,ninakumbuka kushika namba mtihani wa kata,ninakumbuka marafiki zangu wengi wakike akina Editha,Ade,Koku etc mbaya zaidi ni kufungiwa shule yetu kushindisha drs la saba kwenda sekondari miaka mitano.Duuh tuliumia sana kwa uwamuzi wa kikatili huo.Gov abonded some bright guyz.sitasahau hiyo kitu.SHULE YA MSINGI ITAHWA KATA KARABAGAINE KYAMTWARA BUKOBA VIJIJINI KAGERA.

Nakumbuka mara ya kwanza naingia darasan, ticha akanambia niandike jina langu, nikawa sijuw cha kuandika, nikachukua kitabu cha hesabati nikacopy jina la juu ya kitabu HESABATI uwez amin ticha alicheka kufa bt aliamin ndo jina langu.... Duh kweli tunatoka mbali...

mi nakumbuka mdingi alikuwa na hotel kwa hiyo kila siku nilikuwa naenda na kiloba cha halfkeki shuleni mpaka wakanipachika jina la ringo maafkekii,

nilikuwa nahonga kuanzia namba asubuhi,kufanya usafi kikosini mpaka mwalimu wa darasa.

hahahaha.. nakumbuka mbali kweli.

Mkuu wewe ukiwa contractor huwezi kukosa tenda.

Siku ya kufanya mtihani wa Darasa la saba kama siku ya leo terehe 7/9/2011 lakini mimi nilifanya tarehe 23/9/198.Na mara nying ilikuwa inakuwa siku ya jumatano tu.Ilikuwa ni siku moja masomo matatu yaani Hisabati,Lugha na Maarifa ya Jamii.

siku hiyo lazima ukaazime shati kama lako limechoka. Ilipendeza sana.

nakumbuka siku ya kwanza kuanza std one pale jangwani pr school swanga siku iliahirishwa kesho yake tukaja anza rasmi, kitendo cha kuahirishwa kwa siku ya ufunguzi wa shule kimeishi kwenye mind yangu kila shule niliyopita nilitamani hiyo kitu irudie. nikiwa std four Songea huko tulikuwa na mtindo wa kuwakatia viuno watoto wa kike darasani hasa wakiinama basi unakimbilia nyuma yake unamkatikia km mambo flani hivi. mbaya zaidi mwl alituchanganya kila dawati mnakaa msichana na mvulana basi mie nakimbiia kukaa mwanzoni mwa desk naacha demu akae upande wa ukuta na nahakikisha nawahi kukaa kabla yake, anapokuja yeye si atapita mbele yangu basi namvuta ananikalia basi namkatikia darasa zima linashangilia huo ulikuwa mtindo wa wavulana wote. kuna demu alikuwa mbaya na mchafu wavulana wote walikuwa hawamkatikii hata iweje, ktk kutafuta kuchekesha darasa, kuna siku nilimnyang'anya eni yake nikaitupa chini mbele ya darasa yeye hakujua nachotaka kufanya alipokwenda kuokota hakujua nipo nyuma yake ile kainama tu nikakamata kiuno style ya mbuzi kagoma kwenda katiiiiiiika mtoto darasa zima linashangilia. cha ajabu hakuna hata siku moja mtoto wa kike alishtaki kwa mwl. nikikumbuka namuomba tu mungu anuisamehe!

hakika mlilaaniwa!

Mi namkumbuka mwalimu wangu wa sayansi alikuwa anapenda sifa huyo,basi anaingia darasani anaandika ubaoni,SAYANSI,halafu anasema kwa wale watakaoenda sekondari,somo hili linaitwa SCIENCE,TUNGAMO mtaita MASS,UZITO mtaita WEIGHT n.k,yaani alikuwa anajifanya anajua sana!

Nakumbuka kibaoni primary Hai nlikuwa nakula chakula cha waalimu,tunaenda kulima mashamba ya waalim na wazazi wetu walikuwa wanaturuhusu!nayakumbuka sana mashindano ya umitashumta ili kuwa raha sana jamani!waalim wangu tunaheshimiana sana mpaka leo!

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom