Pressure ya kushuka kwa mama mjamzito

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
47,407
40,475
Poleni na majukumu, nimekuja kwenu kuomba msaada juu ya jambo hili.

Mke wangu ni mjamzito wa miezi mitano kwenda wa sita sasa, katika kuhudhuria clinic hii ni mara ya pili vipimo vinaonyesha pressure yake ipo chini.

Je hii ina athari gani kwa mama na mtoto aliye tumboni? Maana ni ujauzito wake wa kwanza na kwa jinsi alivyopitia changamoto nyingi tokea kuubeba itakua uchungu mkubwa kwetu sote mimi na mke wangu endapo tatizo hili litasababisha tatizo lolote kiafya kwa mama na mtoto.

Pia kama ipo njia nyingine ya kuipandisha pressure yake ikae sawa tofauti na kuchanganya Oral na glucose kama alivyoshauriwa clinic, nitafurahi kuifahamu.

Natanguliza shukrani, pia samahani kama mada hii imejirudia.
 
Athari kubwa ni mtoto kukosa hewa ya kkutosha sababu pressure ndogo hufaanya damu kidogo imfikie. Nakushauri apime hospitali kubwa kujua shida nini. Kutokula vizuri au kutapika huchangia hiyo shida.
 
Pressure iki chini unamaanisha nini mkuu. Go deep eleza kwa makini zaidi fafanua kwa unit ipo ngapi kwa ngapi pressure ina kipimo chake by unit acha kueleza kwa mazoea hio ni afya ya mtoto na mkeo utakuja kupewa ushauri wa hovyo humu ndani iwagharimu familia kwa ujumla
 
Poleni na majukumu, nimekuja kwenu kuomba msaada juu ya jambo hili.

Mke wangu ni mjamzito wa miezi mitano kwenda wa sita sasa, katika kuhudhuria clinic hii ni mara ya pili vipimo vinaonyesha pressure yake ipo chini...

This info may help:-
 

Attachments

  • CAUSES AND REMEDIES FOR LOW BLOOD PRESSURE DURING PREGNANCY.pdf
    276.3 KB · Views: 30
Walimuambia achanganye Oral na glucose kwenye maji anywe
Wiki 24 za mwanzo ambazo ni kama hiyo miezi 5, mtoto hukua kwa haraka sana na wakati mwingine mfumo wa kuzungusha damu wa mama huwa unalemewa kidooogo. Hivyo BP kushuka huwa sio kitu cha ajabu ndani ya muda huo.

LAKINI,
Daktari anatakiwa atafute chanzo cha BP kushuka KAMA sio sababu ya ujauzito.
Je anatumia dawa zinazoathiri BP?
Anakunywa maji na kula matunda( vyanzo vya maji kiasi gani?)
Anapoteza maji toka mwilini sana kwa mfano kwa kukojoa koja sana kuliko anavyokunywa maji? Kama ndio kwanini? Ana infection? figo zake ziko sawa?
Ana Anaemia? etc

Unless kama wamempima salt balance yake wakasema kapungukiwa na Sodiumchloride. Na kama kapungukiwa nayo walitakiwa wampe drip sio waseme akanywe glucose. Glucose ni sukari na kuna Gestational Diabetes (aina ya kisukari inayowapata wajawazito) ni hatari sana.

Kwakifupi,
BP ni ile nguvu au kasi ya damu inavyojisukuma ndani ya mishipa ya damu, dhidi ya hiyo mishipa ya damu. Kwahiyo wahusika wakuu hapo ni ;
1.) wingi (volume) na uzito wa damu na uwepo wa (majimaji), ambavyo vinaamua kwa asilimia kubwa kiasi cha pressure.
2.) hali ya mishipa ya damu yenyewe (huku hatutakwenda maana tutachanganyana tu).

Glucose au chumvi (sodiumchloride) ikiwa ndani ya mishipa ya damu inavuta na kushikilia maji ndani na hivyo kuongeza volume ya damu na kama mishipa iko powa, pressure inaongezeka.
Lakini Kunywa Glucose au Sodiumchloride haisaidii kama ana Anaemia ambayo ni kupungukiwa kwa zile red blood cells (zile chembe ziatengeneza damu). Ndo maana lazima kujua chanzo hasa cha Pressure kushuka.

Samahani kwa jibu reefu ninalojaribu kutafasiri uelewa niliokaririshwa kwa kikoloni kuja kwenye lugha ya mama.

Kifupi:
Mboga za kijani kwa wingi zile tumefunzwa na mabibi zetu kuwa zinaongeza damu. Msibane matumizi ya chumvi lakini pia msipitilize.
Maji, matunda na maziwa kama yote.

Sukari sio powa, ndo chanzo kikuu cha magonjwa kadhaa kama ya figo na watanzania wengi wanakisukari bila kujijua. Sio lazima uwe mnene. Vifo vingi vya mama na mtoto husababishwa na sukari kuwa juu na preeclampsia (kupanda kwa BP gafla) ambavyo vinaweza kuzuilika.

Mpende na mthamini mkeo

Kubeba mimba na kuzaa japo wazee wetu walikuwa wanafanya enzi hizo bila hata wakunga, lakini sio ishu ya mchezomchezo. Ni hatari sana kwa maisha ya mwanamke.

Nawatakia kila lenye heri.
 
Back
Top Bottom