Press conference ya Mbowe kuhusu Tundu Lissu: Tujikumbushe jinsi 43 milioni za wabunge zilivyochelewa kufika Nairobi

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Inamaana hawakuwa na namba ya mbowe,walanmsigwa kuwauliza hospitali gani na contact zao zikoje kuwapata?
Langi harisi zinaanza kuonekana,hawakutaka mbowe ajue kama hawamtumii yeye.

Kwanini mpaka tarehe 20/09 kwani zilichangwa tarehe 18???Au walikuwa wanazihesabu tena???Wanazihakiki!!!Na huyo aliyejibu mmmhhh km Mimi nisingejibu kwa kuwa nimeshatuma hata kama leo labda nikiitwa kwenye kamat na kuojiwa pesa nimetuma lin??

Nime-quote makusudi hizi post mbili na nikaweka thread nyingine tofauti kwa madhumuni ya hili tu.

Maelezo yanasema kwamba kwanza hazikuchangwa kwa sababu kamati ya Uongozi ilipendekeza kwamba kila mbunge akatwe nusu posho ya siku. Hii maana yake iliwezekana siku ileile bunge halikutoa ile nusu posho likabaki nayo ili iende kwenye matibabu ya Tundu Lissu.

Tundu Lissu kapigwa risasi na watuhumiwa mnamo September 7, 2017 yaani Alhamis. Kufikia Jumatatu iliyofuata yaani September 11, 2017 ni wazi iliwezekana au hata ilikuwa hivyo kwamba fedha ilikuwa tayari.

Kwa maelezo ya leo Mbowe alipigiwa simu na Spika kwamba fedha 43m zilishapatikana na tunanukuu hotuba ya Mbowe,

"na hapa nazugumza kuithibitisha kauli ya kinafiki ya huyu Mwalimu na Spika Ndugai. Kamati ya Uongozi ambayo na mimi ni mjumbe lakini bahati mbaya mimi tayari nilikuwa Nairobi.

Kwa hiyo wakakaa wengi ni wa CCM, wakaamua bwana, serikali haiwezi kutoa hela kupeleka Kenya. Kwa hiyo wabunge wenyewe binafsi wachange.

Haijawahi kutokea mbunge akaugua akachangiwa na wabunge wenzake, analipiwa gharama na bunge kwa sababu ni stahili yake.

Lakini kwa Lissu wakasema hapana, hela ya serikali isitumike, wabunge binafsi wachange, nusu posho ya siku.

Kwa hiyo wakachanga milioni 43. Na Spika akanipigia simu nikiwa Nairobi, akaniambia, Mwenyekiti, MB, tumechanga milioni 43, tunaomba maelekezo tuzipeleke wapi.

Katibu wa Bunge Kashilila, akanipelekea meseji, tuna michangioyenu milioni 43 ya wabunge tuipeleke wapi?

Nikamjibu, chama kimetoa account ya CRDB. Pelekeni pesa kwenye account ya chama ya CRDB ndiyo wanaoratibu makao makuu michango yote, kisha watatuma Nairobi.

Zikapita siku mbili pesa hazikuingia, tunaendelea na matibabu. Wakatoka na kuali, akanipigia Spika tena, sisi hatuwezi kuingiza pesa kwenye account ya chama chenu. Tuko tayari kulipa hospitali moja kwa moja. TUnaomba utupatie particulars za hospitali.

Sikuona shida kwa sababu fedha zinakwenda kwenye matibabu. Nikampelekea kw akupitia email. Mkurugenzi wa fedha wa utawala wa bunge Athuman Nkwima, na hata email address yake naikumbuka, nikampelekea wiki moja imepita , zile fedha hazijatumwa mpaka leo.

Tumeisoma hotuba yote na mlolongo wote wa tangu kuanza kwa fedha hizi hadi hako hiyo sentensi ka mwisho. Tujiulize? Hii maana yake ni nini?

Naona kuna kungangania hii sentensi ya mwisho ili kuonyesha uongo kwamba fedha zilitumwa. Ukweli ni kwamba hakukuwa na haja ya kusema leo kwamba fedha zimetumwa Sept. 20, 2017.

Unaposema hivyo leo saa nane wakati Mbowe katoa madai hayo saa saba kwa ujumla umetengeneza historia kwamba taarifa hiyo hata kama ni kweli imetokana na tuhuma za Mbowe ambazo ni ukweli.

Haina tofauti na wale watu wa Kimara ambao walipata Stop Order mchana, halafu wakakaa nayo na hawakuipeleka TANROADS kesho yake asubuhi TANROADS wakaanza kubomoa nyumba zao ndipo nao wakakurupuka wakidai kuna Stop Order.

Kwa sisi ambao hatuna chama cha siasa mimi nilikuwa mmoja humu JF kupinga utaratibu na nikatetea wabomolewe kwa sababu ya uzembe wa kutjua kutumia kitu kiitwacho "proof of service".

"Proof of service" ni uthibitisho kwamba jambo ulilotuma limefika lakini hata hivyo limefika muda gani. Hapa Mbowe hawezi kulaumiwa kwani taarifa ya zile hela hata kutumwa haimumfikia. Kama ni kweli hela zilitumwa na Bunge kwenye accoutn fulani tu basi wakakaa kimya.

Lakini ukumbuke kwamba wanakaa kimya hivyo wakati hata particulars za hospitali hawakuzitafuta kimyakimya bali hotuba tumeona imesema walipewa na Mbowe.

Tuje upande wa pili, Mbowe kasema pesa zile Mbowe kawapa hospital particulars wiki imepita yaani nina haki ya kusema ni September 15, 2017 yaani Ijumaa iliyopita na nadhani ndiyo siku bunge limeahirishwa pale Dodoma huku spika akiwatahadharisha wabunge usalama wao.

Lakini taarifa kwamba pesa kwamba pesa kiasi cha milioni 43 zimepatikana ni kwenye tumeisikia September 14, 2017 yaani alhamisi iliyopita tena kwa sifa kwamba hizi za wabunge zimepatikana haraka. Kumbuka siku hiyo (September 14, 2017) ndiyo siku Spika aliposema amemsamehe Godbless Lema na magazeti kesho yake yakaandika hivyo.

Hivyo, hadi September 14, 2017 fedha zile zilishakuwa tayari zimepatikana. Leo inapotoka taarifa kwamba zimetumwa September 20, 2017, tena taarifa inatoka nusu saa baada ya mkutano wa Mbowe ni kuiacha dunia nzima kushangaa na kujadili na hivyo kila mmoja kuhitimisha anavyotaka.

Tena imetolewa kana kwamba kuumbua uongo. Mliosikiliza Mbowe tulichambue hili suala. Kuna wakati Mbowe alikuwa anasoma na kuna wakati alikuwa naongea bila kusoma. Mwanzoni kabisa mnakumbuka kwamba alissoma karatasi yake na kusema haya anayoongea ni taarifa ya matibabu hadi September 14, 2017 saa kumi jioni.

Hapa mkanushaji wa bunge hataki kupataja kataja pale ambapo Mbowe alisema hadi leo. ambako Mbowe alitamka vile na alikuw ana haki.

Ni wazi kilichomleta Mbowe anayerudi tena Nairobi ilikuwa ni press conference kuondoa mamilioni ya uvumi wa niz nzuri na nia mbaya. Kama Mbowe kaondoka jana ili aje na taarifa nzito maana yake juzi jioni alikuwa anatakiwa kuwa na taarifa hiyo na nadhani alifanya makusudi kuichukua ya muda muda ule wa saa 10 jioni, ambayo haionyeshi lolote kuhusu fedha milioni 43 kuingizwa pale Hospitalini.

Ni wazi kadiri taarifa zinavyokuja kuumbuliwa kutakuwa ni zaidi. Kama fedha zilipatikana kabla ya September 14, 2017 na juzi tuamini kwamba ndipo zimetumwa basi ni kujiweka katika matatizo ya kutoa sababu zako za kuchelewa kwa kiasi hicho hata kama isingekuwa ni matitabu ya emergency.

Particulars za hospitali umeshapewa na Mbowe na hata hivyo hukutakiwa hata kupewa naye kwa sababu hata wewe ukitaka particulars utazipata. Kenya na hata huko Tanzania kuna kitu kinaitwa Yellow Page na huko unapata kila information unapoihitaji wakati wowote. Directories ziko za kila aina hata wakati miaka ile kuna simu za mezani tu.

Kupata account ya hospitali haichukui masaa mawili kama una sababu genuine za kuipata hata kama ni wewe binafsi.

Sisemi hizi pesa zilichelewa ili ziliwe, ila ninaonyesha jinsi public sector ya Tanzania ilivyo nyuma katika ku-process vitu ambavyo havihitaji hata kutumia siku mbili kukamilika.

Kwa ujumla hili suala la Tundu Lissu taasisi zisipokuwa makini zitabaki kuaibika kila wakati zinapotoa public statement.

Zamani watu walikuwa hawajui mambo ya kutuma vitu kama pesa au registry na file managements. Walikuwa wanayajua walioko ofisi za serikalini tu na makampuni machache.

Siku hizi watu wako mtaani hawako ofisi yoyote na wanayajua kuliko hata wa maofisini. Taasisi zizipobadilika na kukiri kwamba tuna jamii inayojua kila kitu eti ikaendelea na dhana ya zamani kudhani hawajui, zitaishia kugombana ugomvi ambao kila siku zitaishia kuumbuka.
 
Duh.......,tatizo hili suala la huyu mgonjwa linapelekwa kisiasa zaidi kuliko kumsaidia mgonjwa.

Kwa sisi wananchi wa kawaida wenye imani tunatakiwa kuendelea kumuombea bila kutafuta kiki za media nk.

Ila Tundu hatendewi haki na serikali pamoja na chama chake,na inaudhi na inauma ukiwa kama mwanafamilia au mtu mwenye mapenzi mema na mtanzania mwenzako.
 
Kiondoe chama ktk hii lawama mkuu....

Isingekuwa chama chake, likely Tundu Lissu tusingekuwa naye sasa..!!

Kiukweli na kwa nafsi yangu, nimpongeze sana Freeman Mbowe (MB) na M/kiti wa CHADEMA taifa na wenzake ktk chama kwa ku - react kwa wakati ktk kuamua hatima ya mgonjwa huyu...

Hata baada ya serikali kugoma kugharamia matibabu kwa visingizio uchwara, yet, CHADEMA wakabuni utaratibu wa haraka na kuratibu taratibu za michango kwa ajili kugharamia matibabu ya mgonjwa vizuri sana...

They deserve credit for this.......

Ninaamini kabisa wanafamilia hawajatoa chochote ktk kumtibia ndugu yao kwa sbb Tundu Lissu ni mtu wa watu.....

The guy (Mr Mbowe) to me, is a real man and a true leader..., no doubt about it....

Kuwalaumu CHADEMA utakuwa huwatendei haki....

Wamefanya kazi kubwa sana ktk hili na nina hakika kabisa kuwa, hata wanafamilia wa Tundu Lissu wana appreciate efforts za chama ktk kushughulikia suala la ugonjwa wa ndugu yao...

Hatujasikia yeyote akilalamika kuhusu hili na hata wazee wa propaganda kutoka Lumumba, kwa hili wamekamatwa wameshindwa kuingia kwenye familia hii kuwalisha maneno....!!

Kauli zenye elements za usiasa siasa haziupukiki ktk hili kwa sbb Tundu Lissu mwenyewe ni mwanasheria na mwanasiasa vilevile....

Hata jaribio la kutaka kuwawa kwake, liko motivated na sababu za kisiasa kwa 100% .....

Ni wazi usiasa siasa haupukiki kila wakati tunapomjadili huyu bwana aidha iwe kwa nia njema ama kwa malengo mabaya.....

Wasiompenda na waliotaka kumuua, obviousily hawataweza kumjadili positively.....!

Kwao ni wakati wote ni, kwa nini hafi? Kwanini tumeshindwa kumuua huyu hayawani? Kwa vipi na kwa namna gani tupenye tukammalizie?

Namna gani tuwavuruge wanaomshabikia... lakini bahati mbaya kwao ni kuwa, they have failed...!!!
 
Mkuu umechambua vizuri.
 
Nime-quote makusudi hizi post mbili na nikaweka thread nyingine tofauti kwa madhumuni ya hili tu.

Maelezo yanasema kwamba kwanza hazikuchangwa kwa sababu kamati ya Uongozi ilipendekeza kwamba kila mbunge akatwe nusu posho ya siku. Hii maana yake iliwezekana siku ileile bunge halikutoa ile nusu posho likabaki nayo ili iende kwenye matibabu ya Tundu Lissu.

Tundu Lissu kapigwa risasi na watuhumiwa mnamo September 7, 2017 yaani Alhamis. Kufikia Jumatatu iliyofuata yaani September 11, 2017 ni wazi iliwezekana au hata ilikuwa hivyo kwamba fedha ilikuwa tayari.

Kwa maelezo ya leo Mbowe alipigiwa simu na Spika kwamba fedha 43m zilishapatikana na tunanukuu hotuba ya Mbowe,

"na hapa nazugumza kuithibitisha kauli ya kinafiki ya huyu Mwalimu na Spika Ndugai. Kamati ya Uongozi ambayo na mimi ni mjumbe lakini bahati mbaya mimi tayari nilikuwa Nairobi.

Kwa hiyo wakakaa wengi ni wa CCM, wakaamua bwana, serikali haiwezi kutoa hela kupeleka Kenya. Kwa hiyo wabunge wenyewe binafsi wachange.

Haijawahi kutokea mbunge akaugua akachangiwa na wabunge wenzake, analipiwa gharama na bunge kwa sababu ni stahili yake.

Lakini kwa Lissu wakasema hapana, hela ya serikali isitumike, wabunge binafsi wachange, nusu posho ya siku.

Kwa hiyo wakachanga milioni 43. Na Spika akanipigia simu nikiwa Nairobi, akaniambia, Mwenyekiti, MB, tumechanga milioni 43, tunaomba maelekezo tuzipeleke wapi.

Katibu wa Bunge Kashilila, akanipelekea meseji, tuna michangioyenu milioni 43 ya wabunge tuipeleke wapi?

Nikamjibu, chama kimetoa account ya CRDB. Pelekeni pesa kwenye account ya chama ya CRDB ndiyo wanaoratibu makao makuu michango yote, kisha watatuma Nairobi.

Zikapita siku mbili pesa hazikuingia, tunaendelea na matibabu. Wakatoka na kuali, akanipigia Spika tena, sisi hatuwezi kuingiza pesa kwenye account ya chama chenu. Tuko tayari kulipa hospitali moja kwa moja. TUnaomba utupatie particulars za hospitali.

Sikuona shida kwa sababu fedha zinakwenda kwenye matibabu. Nikampelekea kw akupitia email. Mkurugenzi wa fedha wa utawala wa bunge Athuman Nkwima, na hata email address yake naikumbuka, nikampelekea wiki moja imepita , zile fedha hazijatumwa mpaka leo.

Tumeisoma hotuba yote na mlolongo wote wa tangu kuanza kwa fedha hizi hadi hako hiyo sentensi ka mwisho. Tujiulize? Hii maana yake ni nini?

Naona kuna kungangania hii sentensi ya mwisho ili kuonyesha uongo kwamba fedha zilitumwa. Ukweli ni kwamba hakukuwa na haja ya kusema leo kwamba fedha zimetumwa Sept. 20, 2017.

Unaposema hivyo leo saa nane wakati Mbowe katoa madai hayo saa saba kwa ujumla umetengeneza historia kwamba taarifa hiyo hata kama ni kweli imetokana na tuhuma za Mbowe ambazo ni ukweli.

Haina tofauti na wale watu wa Kimara ambao walipata Stop Order mchana, halafu wakakaa nayo na hawakuipeleka TANROADS kesho yake asubuhi TANROADS wakaanza kubomoa nyumba zao ndipo nao wakakurupuka wakidai kuna Stop Order.

Kwa sisi ambao hatuna chama cha siasa mimi nilikuwa mmoja humu JF kupinga utaratibu na nikatetea wabomolewe kwa sababu ya uzembe wa kutjua kutumia kitu kiitwacho "proof of service".

"Proof of service" ni uthibitisho kwamba jambo ulilotuma limefika lakini hata hivyo limefika muda gani. Hapa Mbowe hawezi kulaumiwa kwani taarifa ya zile hela hata kutumwa haimumfikia. Kama ni kweli hela zilitumwa na Bunge kwenye accoutn fulani tu basi wakakaa kimya.

Lakini ukumbuke kwamba wanakaa kimya hivyo wakati hata particulars za hospitali hawakuzitafuta kimyakimya bali hotuba tumeona imesema walipewa na Mbowe.

Tuje upande wa pili, Mbowe kasema pesa zile Mbowe kawapa hospital particulars wiki imepita yaani nina haki ya kusema ni September 15, 2017 yaani Ijumaa iliyopita na nadhani ndiyo siku bunge limeahirishwa pale Dodoma huku spika akiwatahadharisha wabunge usalama wao.

Lakini taarifa kwamba pesa kwamba pesa kiasi cha milioni 43 zimepatikana ni kwenye tumeisikia September 14, 2017 yaani alhamisi iliyopita tena kwa sifa kwamba hizi za wabunge zimepatikana haraka. Kumbuka siku hiyo (September 14, 2017) ndiyo siku Spika aliposema amemsamehe Godbless Lema na magazeti kesho yake yakaandika hivyo.

Hivyo, hadi September 14, 2017 fedha zile zilishakuwa tayari zimepatikana. Leo inapotoka taarifa kwamba zimetumwa September 20, 2017, tena taarifa inatoka nusu saa baada ya mkutano wa Mbowe ni kuiacha dunia nzima kushangaa na kujadili na hivyo kila mmoja kuhitimisha anavyotaka.

Tena imetolewa kana kwamba kuumbua uongo. Mliosikiliza Mbowe tulichambue hili suala. Kuna wakati Mbowe alikuwa anasoma na kuna wakati alikuwa naongea bila kusoma. Mwanzoni kabisa mnakumbuka kwamba alissoma karatasi yake na kusema haya anayoongea ni taarifa ya matibabu hadi September 14, 2017 saa kumi jioni.

Hapa mkanushaji wa bunge hataki kupataja kataja pale ambapo Mbowe alisema hadi leo. ambako Mbowe alitamka vile na alikuw ana haki.

Ni wazi kilichomleta Mbowe anayerudi tena Nairobi ilikuwa ni press conference kuondoa mamilioni ya uvumi wa niz nzuri na nia mbaya. Kama Mbowe kaondoka jana ili aje na taarifa nzito maana yake juzi jioni alikuwa anatakiwa kuwa na taarifa hiyo na nadhani alifanya makusudi kuichukua ya muda muda ule wa saa 10 jioni, ambayo haionyeshi lolote kuhusu fedha milioni 43 kuingizwa pale Hospitalini.

Ni wazi kadiri taarifa zinavyokuja kuumbuliwa kutakuwa ni zaidi. Kama fedha zilipatikana kabla ya September 14, 2017 na juzi tuamini kwamba ndipo zimetumwa basi ni kujiweka katika matatizo ya kutoa sababu zako za kuchelewa kwa kiasi hicho hata kama isingekuwa ni matitabu ya emergency.

Particulars za hospitali umeshapewa na Mbowe na hata hivyo hukutakiwa hata kupewa naye kwa sababu hata wewe ukitaka particulars utazipata. Kenya na hata huko Tanzania kuna kitu kinaitwa Yellow Page na huko unapata kila information unapoihitaji wakati wowote. Directories ziko za kila aina hata wakati miaka ile kuna simu za mezani tu.

Kupata account ya hospitali haichukui masaa mawili kama una sababu genuine za kuipata hata kama ni wewe binafsi.

Sisemi hizi pesa zilichelewa ili ziliwe, ila ninaonyesha jinsi public sector ya Tanzania ilivyo nyuma katika ku-process vitu ambavyo havihitaji hata kutumia siku mbili kukamilika.

Kwa ujumla hili suala la Tundu Lissu taasisi zisipokuwa makini zitabaki kuaibika kila wakati zinapotoa public statement.

Zamani watu walikuwa hawajui mambo ya kutuma vitu kama pesa au registry na file managements. Walikuwa wanayajua walioko ofisi za serikalini tu na makampuni machache.

Siku hizi watu wako mtaani hawako ofisi yoyote na wanayajua kuliko hata wa maofisini. Taasisi zizipobadilika na kukiri kwamba tuna jamii inayojua kila kitu eti ikaendelea na dhana ya zamani kudhani hawajui, zitaishia kugombana ugomvi ambao kila siku zitaishia kuumbuka.
Kawaida sisi wanasheria tunaongea evidence hasa documentally evidence nikisoma speech ya serikali sioni invoice ya malipo, kwa hiyo inaonekana ccm swala hili wanalichukulia kisiasa, ndo maana watanzania wanawajua inawekana watu wasiojulikana wakawa ni ccm. Over
 
Waweke ushahidi hadharani wa pesa hizo kutumwa na pia kuwataarifu Chadema au familia kwamba Bunge limetuma pesa hizo. Vinginevyo wanyamaze tu tumechoshwa na pumba zao.

Mkuu bado pesa iko Dodoma, kama kweli wametuma pesa Nairobi waweke hati ya benki ya kupeleka hizo pesa, vinginevyo tangazo la Bunge ni takataka.
 
Wakuu poleni na majukumu! kuna mtu mwenye link ya press conference ya Mbowe na wanahabari hapo jana! nimejaribu kuitafuta lakini sijaiona.
 
Genge la wajanja wanapasua raha kwa mgongo wa mgonjwa. Tayari wamesharipoti 204M zimeondoka,(zimetumika), wapo first class hotels wanapumua tu.

Tunataka mchanganuo, zipi zimelipwa Hospital na zipi Wandava wameshajikimu.
 
Back
Top Bottom