#COVID19 President Uhuru Kenyatta orders new lockdown to battle COVID-19 infections wave

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
53,876
2,000
Mama SUluhu is 61 years Old, she never wear mask
She wqnt us to ho back to square one
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,480
2,000
Mkuu ulimwengu huu ni hadaa.....the way u navyoona vitu si kama vilivyo....
Jombaa, mimi nazungumza kuhusu uhalisia wa mambo kama yalivyo. NATO wakiongozwa na Ujerumani, ambao waliitumia China 'invoice' ya €130Billion, tayari walianza kujadili mbinu za kuilazimisha China ilipe. Kisa utepetevu wao kwenye response yao dhidi ya kirusi cha COVID-19.

UK pia wamesema wazi kwamba wanaidai China hela nyingi na kwamba nchi hiyo haitaepuka lawama zinazohusu maambukizi ya COVID-19. Kuna nchi zingine tano ambazo zimeungana kudai kwa sauti moja, kwamba lawama zote zipo kwenye mlango wa China na kwamba lazima watachukuliwa hatua. Iran ni kati ya nchi hizo na Kazakhstan pia.

China gets 130-billion-pound bill from Germany for corona damages - ET HealthWorld
 
Richard spencer

JF-Expert Member
Feb 22, 2021
716
1,000
Wewe fikiria Ebola, kirusi ambacho ni hatari zaidi ya COVID, kisambae kwa kasi kutoka DRC ambao hawana mifumo dhabiti kama China na nchi zingine '1st World'. Kisha kifike kwenye nchi hizo na kisababishe maafa na hasara kama janga hili. Hapa Afrika kutakalika kweli? Si wanaweza wakawavamia hadi wengine ukanda huu kwa kisingizio kwamba ni marafiki wa Kinshasa?

Jambo ambalo ni la kujiliwaza nalo na ambalo ni baraka kiana ni kwamba janga hili halijawaathiri waafrika kama walivotabiri au kama kilivowaathiri wao. Ila sio kisingizio cha kutoibua hoja kama hii na bara hili linafaa liwe kwenye mstari wa mbele. Maanake ukizingatia kwamba nchi za Afrika bado hazijakomaa kiuchumi, athari za janga hili zitabaki kuwa donda sugu kwa bara hili kwa muda mrefu ujao.

Mwisho wa siku 'responsibility' ya hasara kama ya janga hili na mengine mengi ambayo huwa yanaiathiri zaidi bara la Afrika(kwa mfano 'climate change'), huwa ipo kwa nchi kama China na wenzake.
Juzi Marekani na Umoja wa ulaya walikuwa Alaska wanajadili vikwazo vya kumuwekea kutokana uvunjifu wa haki za binadamu kwa waislam wa uighurs. Bila shaka hiyo ni hatua moja wameanza kukabiliana na china hivyo tegemea vitakuja vikwazo vingine zaidi ikiwepo na hilo suala la corona. Na uzuri sasa hivi Marekani wanadeal na China kimkakati ndomaana ameamua kuhusisha washirika wake hivyo vikwazo vya sasa vitakuwa vigumu zaidi kwa China tofauti na vya Trump.
 
Richard spencer

JF-Expert Member
Feb 22, 2021
716
1,000
Mama SUluhu is 61 years Old, she never wear mask
She wqnt us to ho back to square one
Wanadiplomasia na madaktari wetu hapa wanachemka sana. Hata kama hataki ilitakiwe avae kuhamasisha watu wajikinge zaidi lakini pia alete chanjo, lockdown na curfew asiweke. Atakuwa ameua ndege watatu kwa jiwe moja lakini hichi kiburi tunacholeta kwenye hili janga sijui kama tutafika.
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
823
1,000
Hivi hadi sasa hivi hakuna mtu hata mmoja duniani ambaye ameibuka na charter, strategy, memorandum au jambo lolote lile? Ambalo litashirikisha mataifa yote duniani kuhakikisha kwamba China watalipa, kufidia au kuwekewa vikwazo vya aina yeyoye ile? Kama 'response' ya kimataifa dhidi yao kwa kuisababishia dunia usumbufu, dhiki, majonzi na hasara chungu nzima kupitia hii Kung-Flu virus yao?

Maanake kila mtu anajua kwamba huu ni mwanzo tu na kirusi hiki hakitakuwa cha mwisho. Inamaana kwamba duniani tunaishi mambumbumbu tu ambao hawana ubunifu wowote wala ujasiri? Nimekuwa nikiwaza kuhusu suala hili kwa muda na ninayo draft ambayo nimekuwa nikiiandaa kwa wiki mbili sasa.

UN wajiandae kusoma azimio langu kwenye kikao chao kijao. Haingii akilini kwamba Mjerumani alilipia vita vya pili vya dunia ambavyo vilisababishwa na mwendawazimu wao mmoja. Alafu eti janga hili la COVID-19 ndio tutalisahau tu bila kumlaumu wala kumnyoosha mchina ambaye kwa usiri na ukanjanja wake aliamua tufe wote pamoja.
Kama wakibainika lazima walipie kwa kweli hali tete dunia nzima kwa tatizo lao wenyewe upo sahihi kabisa
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,555
2,000
Juzi Marekani na Umoja wa ulaya walikuwa Alaska wanajadili vikwazo vya kumuwekea kutokana uvunjifu wa haki za binadamu kwa waislam wa uighurs. Bila shaka hiyo ni hatua moja wameanza kukabiliana na china hivyo tegemea vitakuja vikwazo vingine zaidi ikiwepo na hilo suala la corona. Na uzuri sasa hivi Marekani wanadeal na China kimkakati ndomaana ameamua kuhusisha washirika wake hivyo vikwazo vya sasa vitakuwa vigumu zaidi kwa China tofauti na vya Trump.
Wachina wanajiona ni nchi kubwa yaweza jitegemea ndio maana licha ya vikwazo sahi ati wameamua kukata kufanya biashara yoyote na makampuni ya Ulaya, hawataki kuambiwa ukweli kuwa hawatii haki za kibinadamu huko kwao, wanawatesa wenye dini ya kiislamu kwenye detention camps. Ulaya wanamcheki tu, vikwazo vinazidi kuongezeka na nchi nyingi na kampuni kutoka bara ulaya zinajitenga na business with China. Lakini lawama ni kwao, leo hata kesho.
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,555
2,000
Wanadiplomasia na madaktari wetu hapa wanachemka sana. Hata kama hataki ilitakiwe avae kuhamasisha watu wajikinge zaidi lakini pia alete chanjo, lockdown na curfew asiweke. Atakuwa ameua ndege watatu kwa jiwe moja lakini hichi kiburi tunacholeta kwenye hili janga sijui kama tutafika.
Mh. Samia anafaa aweke mikakati dhabiti kuanzia sasa ili kuzuia hasara baadaye na lawama pia. Hivi si kutokee madaktari wakuu wajasiri wampatie facts ya huu ugonjwa, upo jamani. Mh. Kenyatta leo amekubali kudungwa chanjo yeye na timu yake ya state house baada ya hotuba, nikajua kweli hapa kazi ipo na hili wimbi la tatu, kila mtu mwoga aisee, sisi wenyewe raia hata hatujui tutafikiwa mwaka gani, ni Mungu tu asaidie sasa.
 
nomasana

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
1,619
2,000
I have been thinking of the same ...China needs to be held responsible.
Should certain countries in africa be held responsible for ebola? Should brazil be held responsible for zika?! C'mon people sometimes shit happens and punishing china gets you nowhere. Plus, who the hell has enough power to punish china?
 
Richard spencer

JF-Expert Member
Feb 22, 2021
716
1,000
Wachina wanajiona ni nchi kubwa yaweza jitegemea ndio maana licha ya vikwazo sahi ati wameamua kukata kufanya biashara yoyote na makampuni ya Ulaya, hawataki kuambiwa ukweli kuwa wanatii haki za kibinadamu huko kwao, wanawatesa wenye dini ya kiislamu kwenye detention camps. Ulaya wanamcheki tu, vikwazo vinazidi kuongezeka na nchi nyingi na kampuni kutoka bara ulaya zinajitenga na business with China. Lakini lawama ni kwao, leo hata kesho.
China hawezi kuwa super power kwa kutegemea biashara ya ndani tu, kwanza haya makampuni ya nje yakiondoka na purchasing power yao inashuka. China imejengwa na bado inajengwa na makampuni vya marekani na ulaya, yakiondoka china hawezi kuzalisha chochote cha maana sababu hana patents za kutosha. Sasa hivi wanamvumilia wizi wake wa intellectual properties sababu bado wanafanya biashara ila wakitoka tu bidhaa za china zilizotengenezwa kwa wizi wataziwekea vikwazo.

Naamini wazungu hivi vikwazo wanavyotaka kuweka ni vya kibiashara zaidi ili kumpunguza moto mchina kiuchumi. waislamu na hii corona vinatumika tu kama njia ya kufanikisha agenda yao.
 
Richard spencer

JF-Expert Member
Feb 22, 2021
716
1,000
Mh. Samia anafaa aweke mikakati dhabiti kuanzia sasa ili kuzuia hasara baadaye na lawama pia. Hivi si kutokee madaktari wakuu wajasiri wampatie facts ya huu ugonjwa, upo jamani. Mh. Kenyatta leo amekubali kudungwa chanjo yeye na timu yake ya state house baada ya hotuba, nikajua kweli hapa kazi ipo na hili wimbi la tatu, kila mtu mwoga aisee, sisi wenyewe raia hata hatujui tutafikiwa mwaka gani, ni Mungu tu asaidie sasa.
Anajua hatari na athari za huu ugonjwa lakini anapuuza. Ni ukweli usiopingika ugonjwa haujafikia kuwa na madhara kama yaliyopo ulaya ila kama wao wanachukua tahadhari alafu sisi huku tunaonekana hatufanyi chochote kuudhibiti tunakaribisha kutengwa na pengine vikwazo. Ni lazima tujue kucheza siasa za kimataifa pia sio kweli mataifa yote yanayochukua tahadhari ni wajinga ila sisi tu ndio tuna akili.
 
Mkikuyu- Akili timamu

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
4,310
2,000
Wewe fikiria Ebola, kirusi ambacho ni hatari zaidi ya COVID, kisambae kwa kasi kutoka DRC ambao hawana mifumo dhabiti kama China na nchi zingine '1st World'. Kisha kifike kwenye nchi hizo na kisababishe maafa na hasara kama janga hili. Hapa Afrika kutakalika kweli? Si wanaweza wakawavamia hadi wengine ukanda huu kwa kisingizio kwamba ni marafiki wa Kinshasa?

Jambo ambalo ni la kujiliwaza nalo na ambalo ni baraka kiana ni kwamba janga hili halijawaathiri waafrika kama walivotabiri au kama lilovowaathiri wao. Ila sio kisingizio cha kutoibua hoja kama hii na bara hili linafaa liwe kwenye mstari wa mbele. Maanake ukizingatia kwamba nchi za Afrika bado hazijakomaa kiuchumi, athari za janga hili zitabaki kuwa donda sugu kwa bara hili kwa muda mrefu ujao.

Mwisho wa siku 'responsibility' ya hasara kama ya janga hili na mengine mengi ambayo huwa yanaiathiri zaidi bara la Afrika(kwa mfano 'climate change'), huwa ipo kwa nchi kama China na wenzake.
Good. Hii ndio michango tunataka kuona hapa jukwaani
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,555
2,000
Anajua hatari na athari za huu ugonjwa lakini anapuuza. Ni ukweli usiopingika ugonjwa haujafikia kuwa na madhara kama yaliyopo ulaya ila kama wao wanachukua tahadhari alafu sisi huku tunaonekana hatufanyi chochote kuudhibiti tunakaribisha kutengwa na pengine vikwazo. Ni lazima tujue kucheza siasa za kimataifa pia sio kweli mataifa yote yanayochukua tahadhari ni wajinga ila sisi tu ndio tuna akili.
Hapo kweli mkuu, hii kitu si ya kutania kabisa, Italy na Spain Hata huko America, na pesa zote walilizwa vibaya na virusi. Sasa nikiona ati nchi kadhaa Afrika hatuna hata haraka ya kununua hizi chanjo, duh nasikitika sana maana hawatakuja kutusaidia tukizidiwa, sababu walitupea offer na tunaringa.
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,555
2,000
Should certain countries in africa be held responsible for ebola? Should brazil be held responsible for zika?! C'mon people sometimes shit happens and punishing china gets you nowhere. Plus, who the hell has enough power to punish china?
Ebola haijasambaa dunia nzima, na pia China wana makosa ya kutochukua rapid & immediate measures to combat virusi vya Covid-19 ilhali walijulishwa mapema na madaktari wao wakuu na wakapuuzia. Since day one yule daktari alipogundua virusi vipo Wuhan, wangelichukua tahadhari na kuweka Lockdown kali sana China nzima na kuitisha hata usaidizi kwa majirani. Hakuna kuingia wala kutoka China ndio ingekuwa kazi, nina uhakika sahi tungekuwa hatuongelei hatari iliopo.
 
Richard spencer

JF-Expert Member
Feb 22, 2021
716
1,000
Hapo kweli mkuu, hii kitu si ya kutania kabisa, Italy na Spain Hata huko America, na pesa zote walilizwa vibaya na virusi. Sasa nikiona ati nchi kadhaa Afrika hatuna hata haraka ya kununua hizi chanjo, duh nasikitika sana maana hawatakuja kutusaidia tukizidiwa, sababu walitupea offer na tunaringa.
Hapo tutaanza kusema wazungu hawatupendi, wanataka kupunguza watu Afrika wakati sisi wenyewe tunachukulia mambo poa. Imagine mtu unaambiwa kabisa huu ugonjwa ukifika stage ya 3 hakuna malimao wala tangawizi zitakazokusaidia lakini sisi hatujali wala nini bado tunaona chanjo kama sumu.
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,555
2,000
Hapo tutaanza kusema wazungu hawatupendi, wanataka kupunguza watu Afrika wakati sisi wenyewe tunachukulia mambo poa. Imagine mtu unaambiwa kabisa huu ugonjwa ukifika stage ya 3 hakuna malimao wala tangawizi zitakazokusaidia lakini sisi hatujali wala nini bado tunaona chanjo kama sumu.
Hapa ni kujilinda kivyako, sasa ata virus vyenyewe vina mutate kwa kasi, jana naona kirusi mutant kimejiongeza kwa kingine mutant yaani hadi vyashangaza. Malimau na tangawizi yaweza hata yasisaidie kitu kule tuendako. Mungu mbele tu
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,272
2,000
Hapo tutaanza kusema wazungu hawatupendi, wanataka kupunguza watu Afrika wakati sisi wenyewe tunachukulia mambo poa. Imagine mtu unaambiwa kabisa huu ugonjwa ukifika stage ya 3 hakuna malimao wala tangawizi zitakazokusaidia lakini sisi hatujali wala nini bado tunaona chanjo kama sumu.

Nani kakwambia malimao na tangawizi hazitibu stage 3. Got evidences?
 
Greg50

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
1,653
2,000
Anajua hatari na athari za huu ugonjwa lakini anapuuza. Ni ukweli usiopingika ugonjwa haujafikia kuwa na madhara kama yaliyopo ulaya ila kama wao wanachukua tahadhari alafu sisi huku tunaonekana hatufanyi chochote kuudhibiti tunakaribisha kutengwa na pengine vikwazo. Ni lazima tujue kucheza siasa za kimataifa pia sio kweli mataifa yote yanayochukua tahadhari ni wajinga ila sisi tu ndio tuna akili.
Unataka kuwekwa lockdown kisiasa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom