#COVID19 President Samia hires Tony Blair to help in the fight against COVID-19, and rebuild the country's reputation

Hapa ndipo nimeelewa kuwa kama kuwa MISINFORMED, basi ni wote na sipaswi tena kuona kama unajadili hoja kwa dhati ya utaifa ila ushabiki, kwamba ni miongoni mwa wanufaika wa yasiyofaa.

Kwamba hujui kuwa gesi imeuzwa? SONGAS, PANAFRICAN, yote hayo hujui? Unadhani Tanesco anatumia gesi bure bure, unadhani kwanini kabla ya bomba la Mtwara Tanesco ilikuwa inapewa gesi endapo tu ipo ya ziada kwenye pipeline? Unadhani kwanini JPM alikataa kuwaongezea muda wa kuendelea kukaa hapa hao akina SONGAS? 2024 ilikuwa iwe mwisho, ila Msoga theory imerudi kwa nguvu, January na mama wamesema wanenda kuiangalia upya mikataba iliyokwama, ipo 17 sio?

Endelezeni mlipoishia, na nadhani ndio maana halisi ya KAZI IENDELEE. Mtaishi milele sio?
Nimeona posts zako mbili kwangu...

Kwa sasa, wacha nikujibu hii kwanza, na nikipata wasaa, nitakujibu nyingine!!

Man, kwa mara nyingine nasema you're misinformed!!!

Leo hii ukisikia watu wanazungumzia gas boom, wala sio hiyo ya Songas na hao uliowataja!!!

Na hata unaposikia ilipitishwa sheria ya dharula, wala sio kwa ajili ya hiyo gas uliyotaja!

UKWELI UPO KAMA IFUATAVYO....

Tanzania kuna gesi ninazoweza kuita "Za aina mbili"!

Aina ya kwanza, ni gesi ya Songosongo inayowahusisha hao akina SONGAS na aina Gas ya Msimbati/Mnazi Bay iliyojengewa bomba kutoka Mtwara.

Gas zote hizo zimegunduliwa kipindi cha Nyerere, na operesheni zake zilikuwa zinasimamiwa na "Petroleum (Exploration and Production) Act 1980." Reserve ya "gas zote" hizo ni takribani 1.3 Trillion Cubic Feet... kwahiyo sio gas ya kujivunia!!

Gas ya aina ya pili ni ile iliyogunduliwa from 2008 to 2014. Hapa pia kuna za aina mbili, ya kwanza ni ile iliyogundulika nchi kavu (on shore), na nyingine imegundulika baharini (off-shore), and most of it, kama sio yote ni deep sea.

Gas ya nchi kavu ni takribani 10.5 Trillion Cubic Feet, na ile ya baharini ni takribani 47.13 Trillion Cubic Feet. Kwa maana nyingine, total onshore + offshore ni 57.54 Trillion Cubic Feet.

Sasa linganisha hiyo ya 57.54 TCF na ile ya mwanzo na hapo utanielewa kwanini nilisema sio ya kujivunia!!

Sasa ile Sheria ya Gesi ya mwaka 2015 ni kwa ajili ya hizo 57.54 Trillion Cubic Feet, na hii haijachimbwa HATA TONE!! Kama umekuwa ukifuatilia japo kwa uchache, bila shaka umepata kusikia suala la Gas Processing Plant iliyokuwa ijengwe pale Lindi kwa gharama za USD 30 Billion... yaani kwa sasa, bila shaka itakuwa inafika Sh Trillion 70.

Waliofanya exploration ya hiyo gas (57.54 TCF) ni kampuni za Wazungu. Wanaojenga hiyo gas processing plant ya matrilioni yote hayo ni Wazungu lakini bado utawasikia watu wakisema "Gas yote ameuziwa Mchina"!!

And FYI, Wazungu spent billions of USD kufanya exploration!! Na ingawaje watu wanasema sheria mbovu wakati hawajawahi hata kuiona, serikali iliweka wazi kwamba "hatutachangia exploration costs hata senti 5, na hivyo yeyote anayetaka kufanya exploration, will do it at his/her own risk"

Kwanini kulikuwa na huo msimamo wa serikali?

Gas exploration ni very expensive lakini unawekeza pesa kwa kuongozwa na just 2D Seismic Data bila kuwa na uhakika kwamba gas utaikuta! Yaani, data zinasema tu kwamba eneo la Kariakoo kuna uwezekano wa kuwepo gas, lakini data hazikuambia Kariakoo at which particular point!!

Sasa ili kujua at which partcular point, inabidi ufanye drilling kujiridhisha ni wapi hasa kuna gas!! Katika kufanya drilling, unaweza kukuta gas ya kutosha inayoweza kurudisha gharama na kuleta faida, au unaweza kukuta gas ambayo haiwezi kurudisha gharama, au unaweza usikute kabisa!

Sasa kama gas uliyokuta haiwezi kurudisha gharama, au hukukuta gas kabisaa, ina maana hapo inakuwa umezamisha pesa uliyowekeza kwenye drilling ya hicho kisima, na inaweza kufika hata TZS 50 Billion... na ndo hapa Muhongo aliwaambia Wafanya Biashara wa Tanzania kwamba hawana pesa ya kuchimba gas!

Petrobas ay Brazil ilipoteza billions of TZS kwenye exploration!!

Sasa basi, kampuni za so-called Mabeberu wametumia billions halafu leo anatokea mtu anadai "gesi yote kauziwa Mchina", na bado watu wanaamini! Halafu wala hawajiulizi kama gas yote kauziwa Mchina, how come tena hao Mabeberu wanataka kujenga kiwanda cha kuchakata gas pale Lindi kwa matrilioni ya shilingi?!

Na watu wamekuwa wakizungumzia sana kuhusu Sheria mbovu, lakini ukiwaambia waitaje hiyo sheria mbovu, HAWATAJI kwa sababu ni maneno tu ya kusikia, nao wakaamini!! Watu wa karibuni kabisa ni Micho na mbingunikwetu. Wote hawa nimewapa changamoto waniwekee hiyo sheria, na wanieleze JPM kabadili nini, WOTE wameingia mitini!

Ningekuwa home hivi sasa, ningekuwekea hapa hiyo sheria ambayo am sure wengi hawajaisoma lakini wanasema mbovu!! Hata hivyo, angalau tutumie nukuu zifuatazo:-

March 28, 2016, Jarida la The Wall Street Journal lilimnukuu Board Chairman wa Dodsal Group akisema:-
Dodsal has already spent $200 million on its Tanzania project and plans a further $300 million of investments in the next two years to build its exploration and production capabilities there. Mr. Kilachand said, as part of the agreement with the government, profits will be shared “more or less 50-50.
Hiyo ni habari ya March 28, 2016, na kwa kuangalia tarehe bila shaka utapata picha ni sheria ya mwaka gani inayozungumzwa! And to confirm, tafuta source yoyote, na ikukupa profit sharing tofauti na hiyo, NAJIPIGA BAN MWENYEWE!!

Sasa hiyo ndo wanatutangazia kwamba sheria ni mbovu kweli kweli ndo maana Magu kabadili, lakini ukiwauliza Sheria ya Magu inasemaje, HAWASEMI!! Cha ajabu, miaka michache tu iliyopita, hao hao walikuwa wanashangilia Sheria ya Madini ya Magu... sasa sijui na yenyewe inasema profit sharing ni 50/50 less or more!!

And remember, bado hapo kuna kodi yetu!!

And be informed, sheria inasema KILA KITALU, Serikali, kupitia National Oil Company itakuwa inamiliki 50% of the share!!

Sasa nikumegee kwanini sheria ilipitishwa kwa hati ya dharula kuelekea uchaguzi mkuu 2015!!!

Serikali haikuwa na uhakika wa 100% kwamba Magufuli angeshinda!!

Sasa serikali ilikuwa inawaogopa sana Maswahiba wa Lowassa, hususani Rostam Azizi! Hofu ilikuwa kwamba, endapo Magu asingeshinda, halafu Lowassa angeingia madarakani, Rostam Azizi angeingiza influence zake kwenye issue ya gas kwa sababu hawa ni maswahiba wakubwa!!!

Sasa ikaonekana, yeyote atakayeingia madarakani akute tayari sheria imeshapitishwa bungeni, na kusainiwa na rais, akitaka abadili yeye!!

Na nyote mmeshuhudia siku za mwisho mwisho Rostam Azizi alivyoanza kujiweka karibu na Magu, hadi kufikia kumpa shavu la kuzindua mradi wake wa Taifa Gas!!

Na ingawaje watu wanaamini JK alikuwa anamtaka Membe awe rais, nayo sio kweli vile vile! JK tangu hapo alikuwa anamtaka JPM kwa sababu aliamini ndie pekee ambae angeweza kuisimamia Gas & Petroleum Act 2015! Lakini kwavile Membe ni mjanja sana, mambo yake, maongezi yake na matendo yake akawa anawaaminisha watu kwamba yeye ndo chaguo la rais!!!
 
Nakuhakikishia ninamjua mtanzania mmoja tena bado kijana anaweza upiga hodi hapo.
===
Kuhusu maelezo mengine uliyonipa nashukuru. Lakini maswai yaliyojitokeza ngoja niendelee kufuatilia uzi huu.
Nadhani unazungumzia uthubutu... hilo la uthubutu sina shaka nalo!

Sasa kama umenisoma vizuri, hoja yangu sio uthubutu peke yake ingawaje na wenyewe ndo nguzo ya awali na muhimu sana, TENA SANA! Lakini pamoja na uthubutu wa kupiga hodi, je ana exposure ya kumwezesha KUFUNGULIWA MLANGO KWA MIKONO MIWILI?!

Unajua haya mambo ya exposure ni ujinga sana!!! Unaweza kukuta mtu kama Said Fella akaweza kukufikisha kwa January Makamba kirahisi sana kuliko Professor wa Electrical Engineering aliyepo pale CoET!!

Usishangae ukakuta Diamond Platnumz akaweza kukufikisha kirahisi zaidi kwa Uhuru Kenyatta kuliko anayoweza Doto Biteko!!
 
Hivi nyie sio ndo mlikuwa mnaeneza uongo kwamba eti Wachina wameipoka Bandari ya Sri Lanka na kwahiyo hata ya Bagamoyo wataichukua?

Mwenzako mmoja nimemwambia anitajie angalau sheria inasemaje kuhusu umiliki wa gas, AMESHINDWA kutaja kwa sababu hakuna lolote analojua!!

Hata wewe mwenyewe nikikuambia taja hiyo sheria inasemaje, na Magu amebadilisha nini, NINA UHAKIKA KWA 100% huwezi kutaja kwa sababu hujui lolote zaidi ya kusikiliza maneno ya vichochoroni! Na kama nakusingizia, taja hapa sheria ya 2015 inasemaje kuhusu umiliki!!!

Typpical JPM Supporter!!!

Hivi unasoma na kuelewa wapi?

Yaani mradi uliokuwa tayari ku-take off, baada ya mkandarasi na funding kupatikana unaita feasibility study? Hivi unajua hata maana ya feasibility study wewe? Reuters hawa hapa...

Does it sound like it's on feasibility study phase?

Nasema hivi... mlikuwa mnadanganywa kwa sababu you don't know what's going on, na mlikuwa hamjishughulishi kutafuta ukweli.

Halafu unashindwa hata kutumia common sense!! Hivi unajua design inaweza kuchukua muda gani?! Yaani hata design ilikuwa bado but still JPM akaweza kuanza mradi kwa muda alioanza? Ajabu nyingine ni watu wa aina yako mliokuwa mnasema mradi wa reli kwa Mchina ulikuwa wa kifisadi! Sasa ina maana Mchina alipewa tenda ya kujenga kabla ya design?

Sasa kama mimi naweka akili mfukoni, wewe unayeshindwa kufahamu hata jambo dogo kama hili sijui utakuwa unaweka wapi akili yako!!

Wewe mwenyewe umesema JK alikuwa tayari kuanza kujenga pesa iko tayari ameacha mradi feasibility study imekamilika akasema waache sababu anasepa…nikakuuliza feasibility study ikimalizika ndio mradi unaanza kujengwa…

Kabla ya mradi kuanza wanatafuta kampuni yenye ubobezi wa mradi husika…aisee mkuu unanichekesha kweli hizo pesa za mafisadi zitakutafuna km sio wewe kizazi chako unakigugumizi mpaka kwenye maandishi…

Mikataba unayoitetea kwa kifupi yote ilikuwa ina ukakasi…masharti ya hovyo unaeza sikia kichefuchefu ukiambiwa… mikataba mlifanya siri …JPM akaweka uozo wenu hadharini leo mnatafuta maneno yakufunika ukweli ambao haitawezekana kamwe..maji yakishamwagika hayazoleki sasa mdanganyeni mkuu yanazoleka muone hizo pesa mtakavyozitapika nchi hii haina mwenyewe..misingi alioacha Nyerere sio ya kitoto..
 
..hiyo link hapo chini ina maelezo ambayo yanatoa majibu ya maswali yanayotutatiza kuhusu pr / lobbying firms.

Cc TUJITEGEMEE, Chige, Ngungenge, Wacha1
Dah!

Very informative article... nimechelewa kuiona na matokeo yake nikawa natumia nguvu kubwa kumbe kuna mifano ya wazi kabisa!! Na usipofahamu uendeshaji wa mambo kisasa, unaweza kushindwa kuelewa kwa mambo kama haya wakati ni mambo la kawaida sana!
 
Nimeona posts zako mbili kwangu...

Kwa sasa, wacha nikujibu hii kwanza, na nikipata wasaa, nitakujibu nyingine!!

Man, kwa mara nyingine nasema you're misinformed!!!

Leo hii ukisikia watu wanazungumzia gas boom, wala sio hiyo ya Songas na hao uliowataja!!!

Na hata unaposikia ilipitishwa sheria ya dharula, wala sio kwa ajili ya hiyo gas uliyotaja!

UKWELI UPO KAMA IFUATAVYO....

Tanzania kuna gesi ninazoweza kuita "Za aina mbili"!

Aina ya kwanza, ni gesi ya Songosongo inayowahusisha hao akina SONGAS na aina Gas ya Msimbati/Mnazi Bay iliyojengewa bomba kutoka Mtwara.

Gas zote hizo zimegunduliwa kipindi cha Nyerere, na operesheni zake zilikuwa zinasimamiwa na "Petroleum (Exploration and Production) Act 1980." Reserve ya "gas zote" hizo ni takribani 1.3 Trillion Cubic Feet... kwahiyo sio gas ya kujivunia!!

Gas ya aina ya pili ni ile iliyogunduliwa from 2008 to 2014. Hapa pia kuna za aina mbili, ya kwanza ni ile iliyogundulika nchi kavu (on shore), na nyingine imegundulika baharini (off-shore), and most of it, kama sio yote ni deep sea.

Gas ya nchi kavu ni takribani 10.5 Trillion Cubic Feet, na ile ya baharini ni takribani 47.13 Trillion Cubic Feet. Kwa maana nyingine, total onshore + offshore ni 57.54 Trillion Cubic Feet.

Sasa linganisha hiyo ya 57.54 TCF na ile ya mwanzo na hapo utanielewa kwanini nilisema sio ya kujivunia!!

Sasa ile Sheria ya Gesi ya mwaka 2015 ni kwa ajili ya hizo 57.54 Trillion Cubic Feet, na hii haijachimbwa HATA TONE!! Kama umekuwa ukifuatilia japo kwa uchache, bila shaka umepata kusikia suala la Gas Processing Plant iliyokuwa ijengwe pale Lindi kwa gharama za USD 30 Billion... yaani kwa sasa, bila shaka itakuwa inafika Sh Trillion 70.

Waliofanya exploration ya hiyo gas (57.54 TCF) ni kampuni za Wazungu. Wanaojenga hiyo gas processing plant ya matrilioni yote hayo ni Wazungu lakini bado utawasikia watu wakisema "Gas yote ameuziwa Mchina"!!

And FYI, Wazungu spent billions of USD kufanya exploration!! Na ingawaje watu wanasema sheria mbovu wakati hawajawahi hata kuiona, serikali iliweka wazi kwamba "hatutachangia exploration costs hata senti 5, na hivyo yeyote anayetaka kufanya exploration, will do it at his/her own risk"

Kwanini kulikuwa na huo msimamo wa serikali?

Gas exploration ni very expensive lakini unawekeza pesa kwa kuongozwa na just 2D Seismic Data bila kuwa na uhakika kwamba gas utaikuta! Yaani, data zinasema tu kwamba eneo la Kariakoo kuna uwezekano wa kuwepo gas, lakini data hazikuambia Kariakoo at which particular point!!

Sasa ili kujua at which partcular point, inabidi ufanye drilling kujiridhisha ni wapi hasa kuna gas!! Katika kufanya drilling, unaweza kukuta gas ya kutosha inayoweza kurudisha gharama na kuleta faida, au unaweza kukuta gas ambayo haiwezi kurudisha gharama, au unaweza usikute kabisa!

Sasa kama gas uliyokuta haiwezi kurudisha gharama, au hukukuta gas kabisaa, ina maana hapo inakuwa umezamisha pesa uliyowekeza kwenye drilling ya hicho kisima, na inaweza kufika hata TZS 50 Billion... na ndo hapa Muhongo aliwaambia Wafanya Biashara wa Tanzania kwamba hawana pesa ya kuchimba gas!

Petrobas ay Brazil ilipoteza billions of TZS kwenye exploration!!

Sasa basi, kampuni za so-called Mabeberu wametumia billions halafu leo anatokea mtu anadai "gesi yote kauziwa Mchina", na bado watu wanaamini! Halafu wala hawajiulizi kama gas yote kauziwa Mchina, how come tena hao Mabeberu wanataka kujenga kiwanda cha kuchakata gas pale Lindi kwa matrilioni ya shilingi?!

Na watu wamekuwa wakizungumzia sana kuhusu Sheria mbovu, lakini ukiwaambia waitaje hiyo sheria mbovu, HAWATAJI kwa sababu ni maneno tu ya kusikia, nao wakaamini!! Watu wa karibuni kabisa ni Micho na mbingunikwetu. Wote hawa nimewapa changamoto waniwekee hiyo sheria, na wanieleze JPM kabadili nini, WOTE wameingia mitini!

Ningekuwa home hivi sasa, ningekuwekea hapa hiyo sheria ambayo am sure wengi hawajaisoma lakini wanasema mbovu!! Hata hivyo, angalau tutumie nukuu zifuatazo:-

March 28, 2016, Jarida la The Wall Street Journal lilimnukuu Board Chairman wa Dodsal Group akisema:-

Hiyo ni habari ya March 28, 2016, na kwa kuangalia tarehe bila shaka utapata picha ni sheria ya mwaka gani inayozungumzwa! And to confirm, tafuta source yoyote, na ikukupa profit sharing tofauti na hiyo, NAJIPIGA BAN MWENYEWE!!

Sasa hiyo ndo wanatutangazia kwamba sheria ni mbovu kweli kweli ndo maana Magu kabadili, lakini ukiwauliza Sheria ya Magu inasemaje, HAWASEMI!! Cha ajabu, miaka michache tu iliyopita, hao hao walikuwa wanashangilia Sheria ya Madini ya Magu... sasa sijui na yenyewe inasema profit sharing ni 50/50 less or more!!

And remember, bado hapo kuna kodi yetu!!

And be informed, sheria inasema KILA KITALU, Serikali, kupitia National Oil Company itakuwa inamiliki 50% of the share!!

Sasa nikumegee kwanini sheria ilipitishwa kwa hati ya dharula kuelekea uchaguzi mkuu 2015!!!

Serikali haikuwa na uhakika wa 100% kwamba Magufuli angeshinda!!

Sasa serikali ilikuwa inawaogopa sana Maswahiba wa Lowassa, hususani Rostam Azizi! Hofu ilikuwa kwamba, endapo Magu asingeshinda, halafu Lowassa angeingia madarakani, Rostam Azizi angeingiza influence zake kwenye issue ya gas kwa sababu hawa ni maswahiba wakubwa!!!

Sasa ikaonekana, yeyote atakayeingia madarakani akute tayari sheria imeshapitishwa bungeni, na kusainiwa na rais, akitaka abadili yeye!!

Na nyote mmeshuhudia siku za mwisho mwisho Rostam Azizi alivyoanza kujiweka karibu na Magu, hadi kufikia kumpa shavu la kuzindua mradi wake wa Taifa Gas!!

Na ingawaje watu wanaamini JK alikuwa anamtaka Membe awe rais, nayo sio kweli vile vile! JK tangu hapo alikuwa anamtaka JPM kwa sababu aliamini ndie pekee ambae angeweza kuisimamia Gas & Petroleum Act 2015! Lakini kwavile Membe ni mjanja sana, mambo yake, maongezi yake na matendo yake akawa anawaaminisha watu kwamba yeye ndo chaguo la rais!!!

Ok kwa kifupi nashukuru mkuu kwa kumkubali JPM kuwa msimamizi mzuri wa rasilimali zetu..

Kugharamia kuexplore gas haimaanishi ukiipata ni ya kwako…unatulia wenye ardhi wakupe terms…sio unaleta wewe terms JPM alikuwa hatishwi na hizo pesa walizomwga uko baharini…anaangalia maslahi mapana ya nchi…

Nyerere alisema madini yasichimbwe mpaka watanzania wasome wajielewe kwanza waje watumie kwa manufaa yao sasa kilichotokea ni vice versa usaliti wakufa mtu..sasa na kwenye gesi tena ndio maana JPM akapiga pozi..sasa naona mnarudi kupiga ramli hiviii mnachotaka ni nini?!…sifa mabeberu wawaone mnaakili km wao ama ufalme km ule wa Mobutu Seseko…

Watanzania tuko tayari kula makande kuliko hizo chenji zisizo na maana kwetu…
 
Wewe mwenyewe umesema JK alikuwa tayari kuanza kujenga pesa iko tayari ameacha mradi feasibility study imekamilika akasema waache sababu anasepa…nikakuuliza feasibility study ikimalizika ndio mradi unaanza kujengwa…
Hiki ndicho nilisema:-
Tuchukulie SGR kwa mfano... kila kitu kilikamilika mwishoni mwa utawala wa Mzee wa Soga! Feasibility study ilishakamilika, na Mkandarasi alishapatikana!!

Sasa hapo utaita "sasa walishindwa nini kutekeleza"?! Tena niliwahi kumsikia Mzee wa Msoga siku za karibuni akisema "kwavile muda wangu ulikuwa unaelekea kwisha, nikawaagiza wasianze huo mradi kwa sababu unakuja utawala mwingine"

Mfano mwingine, barabara za Dar es salaam! Hadi pesa ilishatolewa tangu May 2015 lakini zikaja kujengwa na Magu!! Hivi hapo utasema "walishindwa nini"?
Na nilichokuambia Mkandarasi na Funding!!
Kabla ya mradi kuanza wanatafuta kampuni yenye ubobezi wa mradi husika…aisee mkuu unanichekesha kweli hizo pesa za mafisadi zitakutafuna km sio wewe kizazi chako unakigugumizi mpaka kwenye maandishi…
Umeshindwa kujibu hoja, unakimbilia viroja... TYPICAL JPM SUPPORTER! Mkishindwa kujibu hoja mnakimbilia kuita wenzenu wanatumika na mafisadi... VERY STUPID

Ina maana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo?!
Mikataba unayoitetea kwa kifupi yote ilikuwa ina ukakasi…masharti ya hovyo unaeza sikia kichefuchefu ukiambiwa… mikataba mlifanya siri …JPM akaweka uozo wenu hadharini leo mnatafuta maneno yakufunika ukweli ambao haitawezekana kamwe..maji yakishamwagika hayazoleki sasa mdanganyeni mkuu yanazoleka muone hizo pesa mtakavyozitapika nchi hii haina mwenyewe..misingi alioacha Nyerere sio ya kitoto..
Wacha maneno na porojo...

Badala ya kuruka rukaruka... jibu swali ambalo nilikuuliza kuhusu hiyo sheria!!!

Lemme guess! Huna huo ubavu wa kuweka kwa sababu kwa sababu hata kuiangalia, HUJAWAI kuiangalia hiyo sheria!!
 
Former British Prime Minister Tony Blair has made two official visits to Tanzania since Samia Suluhu Hassan assumed the presidency in March this year after the sudden death of her predecessor, John Magufuli.

Government officials say that the Tony Blair Institute for Global Change has been hired by President Samia to handle two of her administration’s key projects: the fight against Covid-19 and rebuilding Tanzania’s international reputation.

In July, Blair paid his first courtesy call to Tanzania where he and President Samia discussed how to combat the Covid-19 pandemic.

Blair said his institute is responsible for facilitating the testing and distribution of vaccines, and may help Tanzania to access top vaccine producers.

Credits: The Africa Report
Kandarasi za Blair ni ghali sana na zimejaa usaanii wa kitalaamu sana.baada ya hii kandarasi atatengeneza nyingin.Nadhani serikali iwe unauliza wengine kabla ya kufunga kandarasi na makapuni ya kibepari na kinyonyaji kama haya.ijapo sijui gharama ya hiyo kandarasi ila itakuwa the most top expensive ambayo haitalingana na matokeo yake.hakukuwa na haraka kiasi hicho.
 
Former British Prime Minister Tony Blair has made two official visits to Tanzania since Samia Suluhu Hassan assumed the presidency in March this year after the sudden death of her predecessor, John Magufuli.

Government officials say that the Tony Blair Institute for Global Change has been hired by President Samia to handle two of her administration’s key projects: the fight against Covid-19 and rebuilding Tanzania’s international reputation.

In July, Blair paid his first courtesy call to Tanzania where he and President Samia discussed how to combat the Covid-19 pandemic.

Blair said his institute is responsible for facilitating the testing and distribution of vaccines, and may help Tanzania to access top vaccine producers.

Credits: The Africa Report
 
Ok kwa kifupi nashukuru mkuu kwa kumkubali JPM kuwa msimamizi mzuri wa rasilimali zetu..
Umeelewa nilichoandika?
Kugharamia kuexplore gas haimaanishi ukiipata ni ya kwako…unatulia wenye ardhi wakupe terms…sio unaleta wewe terms JPM alikuwa hatishwi na hizo pesa walizomwga uko baharini…anaangalia maslahi mapana ya nchi…
Tatizo unajifanya unajua wakati hujui chochote...

Kuna mahali niliposema ukigundua gas inakuwa ya kwako?

Again, weka hapa hiyo sheria ya JPM kuhusu gas...
Nyerere alisema madini yasichimbwe mpaka watanzania wasome wajielewe kwanza waje watumie kwa manufaa yao sasa kilichotokea ni vice versa usaliti wakufa mtu..sasa na kwenye gesi tena ndio maana JPM akapiga pozi..sasa naona mnarudi kupiga ramli hiviii mnachotaka ni nini?!…sifa mabeberu wawaone mnaakili km wao ama ufalme km ule wa Mobutu Seseko…

Watanzania tuko tayari kula makande kuliko hizo chenji zisizo na maana kwetu…
Tunazungumzia suala la gas.... weka hapa ile sheria niliyokutaka uweke!!!

Yaani we jamaa unatia aibu sana....

Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015 pamoja na mambo mengine inasema:-
1. Mmiliki wa Vitalu itakuwa serikali kupitia National Oil Company
2. Mwekezaji mwenye mtaji na teknolojia ataingia mkataba na National Oil Company kwa sababu ndie mmiliki wa vitalu
3. Serikali itakuwa ndie Majority Shareholder wa National Oil Company (at least 51%).
4. Profit sharing kati ya National Oil Company na Mwekezaji ni almost 50/50,
5. Kodi
Gas.png

Sheria ya Madini iliyofanyiwa marekebisho 2018 inasema:-
1. Majority Shareholder ni Mwekezaji
2. Serikali inamiliki 16%
3. Kodi

Yaani hapo kwa akili yako wewe, Sheria ya mwaka 2018 ni bora kuliko ya 2015?! Hivi nyie watu mmerogwa, au?

Hakika taifa linaangamia kwa kuwa na viumbe wasiojishughulisha kutafuta ukweli, na badala yake source yao ya taarifa ni wanasiasa na porojo za mitandaoni!!
 
Hiki ndicho nilisema:-

Na nilichokuambia Mkandarasi na Funding!!

Umeshindwa kujibu hoja, unakimbilia viroja... TYPICAL JPM SUPPORTER! Mkishindwa kujibu hoja mnakimbilia kuita wenzenu wanatumika na mafisadi... VERY STUPID

Ina maana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo?!

Wacha maneno na porojo...

Badala ya kuruka rukaruka... jibu swali ambalo nilikuuliza kuhusu hiyo sheria!!!

Lemme guess! Huna huo ubavu wa kuweka kwa sababu kwa sababu hata kuiangalia, HUJAWAI kuiangalia hiyo sheria!!

Sheria zipo tokea Mkapa zimetusaidia nini watanzania…unakimbilia sheria sheria
 
Umeelewa nilichoandika?

Tatizo unajifanya unajua wakati hujui chochote...

Kuna mahali niliposema ukigundua gas inakuwa ya kwako?

Again, weka hapa hiyo sheria ya JPM kuhusu gas...

Tunazungumzia suala la gas.... weka hapa ile sheria niliyokutaka uweke!!!

Yaani we jamaa unatia aibu sana....

Sheria ya Mafuta na Gas ya 2015 pamoja na mambo mengine inasema:-
1. Mmiliki wa Vitalu itakuwa serikali kupitia National Oil Company
2. Mwekezaji mwenye mtaji na teknolojia ataingia mkataba na National Oil Company kwa sababu ndie mmiliki wa vitalu
3. Serikali, kupitia National Oil Company atakuwa ndie Majority Shareholder (at least 51%).
4. Profit sharing kati ya National Oil Company na Mwekezaji ni almost 50/50,
5. Kodi
View attachment 1977534

Sheria ya Madini iliyofanyiwa marekebisho 2018 inasema:-
1. Majority Shareholder ni Mwekezaji
2. Serikali inamiliki 16%
3. Kodi

Yaani hapo kwa akili yako wewe, Sheria ya mwaka 2018 ni bora kuliko ya 2015?! Hivi nyie watu mmerogwa, au?

Hakika taifa linaangamia kwa kuwa na viumbe wasiojishughulisha kutafuta ukweli, na badala yake source yao ya taarifa ni wanasiasa na porojo za mitandaoni!!

Hivi wewe babaaa…kuwa majority share holder ndio kupata pesa nyingi…gesi avune mwingine wewee ukae kusubiria kuambiwa kilichopatikana ndio wakupe cha kwako…

Haya kabla ya sheria ya 2018 ya madini hali ilikuwaje uko nyuma…
 
Gas ya nchi kavu ni takribani 10.5 Trillion Cubic Feet, na ile ya baharini ni takribani 47.13 Trillion Cubic Feet. Kwa maana nyingine, total onshore + offshore ni 57.54 Trillion Cubic Feet.

Sasa linganisha hiyo ya 57.54 TCF na ile ya mwanzo na hapo utanielewa kwanini nilisema sio ya kujivunia!!

Sasa ile Sheria ya Gesi ya mwaka 2015 ni kwa ajili ya hizo 57.54 Trillion Cubic Feet, na hii haijachimbwa HATA TONE!! Kama umekuwa ukifuatilia japo kwa uchache, bila shaka umepata kusikia suala la Gas Processing Plant iliyokuwa ijengwe pale Lindi kwa gharama za USD 30 Billion... yaani kwa sasa, bila shaka itakuwa inafika Sh Trillion 70.
Nashukuru kwa taarifa ulizotupa, kuna la kujifunza pia.

Katika mengi uliyoeleza, napata tabu kuamini ukweli wa taarifa hizi ikiwa unasema huo ujazo wa trilioni 57 haujaguswa hata tone! Sijui kama ni kweli, pengine unisaidie kujua zaidi, ile 1.3t ya Songas, mpaka sasa inafanya kazi gani na hiyo ya Mtwara inatokea wapi? Kisha uniambie Tanesco wanatumia gesi ipi pale ubungo na Kinyerezi.

Pia, unapozungumzia Processing plant ya Lindi, sijui kama umeelewa vizuri ni nini kinaenda kufanyika pale, CNG ndo kinachoenda kufanyika, sio kuchimba!

Kwa hoja hizo, nikuombe u-share hiyo mikataba hapa uliyoisoma ili kila mtu atafsiri anavyoelewa yeye kwa afya ya mjadala.

Taarifa za kuhusika kwa wachina na JK zilikuwepo na hazikuwahi kukanusha na ama serikali au familia, zaidi akiwa madarakani na ilihusishwa na madawa ya kulevya, ni vyema sasa ukatanabaisha kama ndio UNAKANUSHA rasmi na ni kwa niaba ya nani!

JK kumtaka JPM, pia matendo yaliyoonekana hayakusema hivyo, zaidi yalitueleza kuwa jina la JPM ilibidi litumike ku-neutalize situation iliyokuwa imejitokeza, hakuwa chaguo la yeyote kwa wale waliokuwepo kwenye madaraka.

JPM alisema, gesi imeuzwa, haya yalikuwa ni maneno ya raisi wa nchi mwenye vyanzo vingi vya taarifa, zaidi ya yeyote humu! Na hapa sizungumzi issue ya maamuzi ya mtu binafsi, nazungumzia utoaji wa taarifa!

Suala la JK kulinda maliasili za taifa kwaajili ya taifa kwa ujumla, hili hutakaa unishawishi, sitakubali asilani! Lililowazi ni kuwa, nchi ilisimama kwa ujumla wake ili waliowake waneemeke, na hata baada ya miaka 10, wengi wakishangilia uwepo wa pesa mtaani, na haswa kwa majiji makubwa tu, ambazo kimsingi zilitokana na matumizi ya ovyo ya walio wake huko mtaani.

Nchi ikabakia pale pale, huku wachache wakimiliki pesa kuliko nchi.

Maendeleo ya kweli na ya ujumla ni gharama, na gharama hiyo ndio wachache wanufaika wa mfumo wa kinyang'anyi hawako tayari kuzikubali.

Kazi iendelee, inaendeleza pale alipoishia JK, pengine mngetupa taarifa za nchi ilipo kimaendeleo na kimadeni kisha baada ya miaka 5 mje tena na taarifa za nini kimefanyika, tulipotekea, tulipo na tunakoelekea ili sisi tujue kama kuna chochote kimefanyika.

Miaka 60 bado tunazungumzia kuwa na vyoo bora na madawati, tunazungumzia umeme wa 1600MW tu kama nchi yenye 945,000km2! Tunazungumzia bajeti ya 32trillion ambapo, uwezo wa ndani ni 18trillion tu, na hapo 80% inatumika kuendesha serikali, maendeleo ni 5%
 
Hiki ndicho nilisema:-

Na nilichokuambia Mkandarasi na Funding!!

Umeshindwa kujibu hoja, unakimbilia viroja... TYPICAL JPM SUPPORTER! Mkishindwa kujibu hoja mnakimbilia kuita wenzenu wanatumika na mafisadi... VERY STUPID

Ina maana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo?!

Wacha maneno na porojo...

Badala ya kuruka rukaruka... jibu swali ambalo nilikuuliza kuhusu hiyo sheria!!!

Lemme guess! Huna huo ubavu wa kuweka kwa sababu kwa sababu hata kuiangalia, HUJAWAI kuiangalia hiyo sheria!!
Kusema kwamba yeyote anayem-critise mama Samia ni mfuasi wa JPM huo ni utOpolo na inonyesha jinsi ulivyo na mahaba ya kijinga. Kuna watu wengi tu humu jf na hata nje ya jf ambao wao Tanzania ndio namba moja kwao na hivyo wanabase sana kwenye maslahi mapana ya nchi kuitetea nchi yao regradless ni nani yupo ikulu. Hakuna awamu ya uongozi ambayo haijawahi kutofanya makosa wakiwa madarakani. Sasa kama wamu hii ikifanya makosa watu wakaikosoa wewe kwa akili yako hao ni wafuasi wa Magufuli basi huenda wewe ni ukoo wa Samia. UNASIKITISHA SANA KWA MTAZAMO HUO.
 
Hivi wewe babaaa…kuwa majority share holder ndio kupata pesa nyingi…gesi avune mwingine wewee ukae kusubiria kuambiwa kilichopatikana ndio wakupe cha kwako…
Hivi unaelewa maana ya majority shareholder wewe?!

Umeona huo mgawanyo wa faida kama sheria inavyotaka?

Kama hoja ni gesi kuvuna mwingine, hiyo sheria ya madini mnayomsifia Magu, kwani ni nani anayevuna hayo madini?! Ni serikali?

And FYI, kwavile zaidi ya 40 Trillion Cubic Feet za gesi zinapatikana Deep Sea, wawekezaji wakataka kujenga Gas Processing Plant huko huko baharini, lakini serikali ikagoma kwa hoja tusingeweza ku-monitor kinachoendelea huko baharini!
Haya kabla ya sheria ya 2018 ya madini hali ilikuwaje uko nyuma…
Jibu swali: Ina maana kwa ufahamu wako hapo, unataka kusema Sheria ya Madini ya 2018 ni bora kuliko Sheria ya Gas ya 2015?!
 
MMk
Hii nchi nadhani nadhani tatizo kubwa ni elimu yetu mbovu, hivi kazi ya Balozi nje ya nchi ni ipi? Tuna Balozi wa kudumu UN na tuna waziri wa mambo ya nje, hakuna haha ya kuhire institute ya Blair kujenga reputation hewa iliyopotea. Hivi hiyo reputation iliyopotea kimataifa ni ipi?

Pia ni low IQ ya Hali ya juu kuhire Blair institute Kwa sababu ya Tanzania ku access COVID 19 vaccines, ni utopolo Kwa ufupi maana tuna wizara ya afya, tuna MSD ambayo imekuwa ikiagiza na kusambaza madawa nchini na mbaya zaidi tuna kitengo na watalaam wa tiba ya magonjwa ya mlipuko yaani hao wote hawana uwezo w ku access COVID 19 vaccines?

Tony Blair ni mfanya biashara anajua Samia world bank wame approve pesa za COVID 19 , hivyo yeye anawaza ile pesa kwenda kwenye institute yake na kampata mama yenu mpendwa, hata USA na mataifa Yana sukuma kila nchi za Dunia ya tatu wapate pesa kutoka world bank ili in return pesa zote zinarudi kwao kw ajiri ya kupata chanjo za corona by force , sisi kama nchi tutabakiwa na kulipa loans na pesa itakuwa imekwenda kwao, kwahiyo ni lazima uwe kiongozi wa kutafakari haya mambo Kwa kina sio kuitikia Kwa kila jambo.

Mataifa hayo wanajua Tanzania population inskuwa , mil60 kuchanjwa wote maana yake serikali itshitaji si chini ya trilion 3 , so world bank na IMF na WHO hawaoni shida ku approve pesa Kwa ajiri ya chanjo Kwa sababu immediately zikiwa approved astrazeneca, Pfizer, Johnson ndo hao wata supply hizo dawa, hivo WHO Yuko pale kutoa mapande kama yakina zidane kwao, so go against ndipo utaona Cha moto. Tujiulize tu ni proposal ngapi ziko pending world bank kutoka Tanzania au nchi zingine za Dunia ya tatu kuomba fedha za kuanzisha viwanda ili kujikwamue na kuweka vijana wetu kwenye ajira hazijawa approved? Ok good let's focus on COVID-19, tuko million 60, tuliochanjwa laki 3 , waliokufa hawafiki hata elfu moja, hata tunapoongea hapa Bado mil60 yote hawako mahospitalini wakipumulia machine na haitatokea , hii force kutoka majuu sio Kwa ajili ya kuzuia corona na Kwa ajili ya kuuza vaccines, hatukatai tusichanjwe lakini kama taifa tuangalie priority zetu na agenda zetu kwanza, agenda ya taifa hili sio kuhire institute kuondoa reputation hewa, agenda yetu ni maendeleo na kuondoa umasikini uliokithiri Tanzania, vijana wapate ajira wajiingizie kipato na sio mengine .
Mkuu kuna mbumbumbu watakupinga na kukuita Sukuma gang,ila usema ukweli, Tanzania haitaji mzungu kutatua matatizo yetu, tunaitaji viongozi wazelendo waliosomeshwa na kodi yetu kusaidi Nchi yetu
 
..hiyo link hapo chini ina maelezo ambayo yanatoa majibu ya maswali yanayotutatiza kuhusu pr / lobbying firms.

Cc TUJITEGEMEE, Chige, Ngungenge, Wacha1
Asante sana Mkuu. Link imetoa majibu mengi ya maswali yangu.
 
Nashukuru kwa taarifa ulizotupa, kuna la kujifunza pia.

Katika mengi uliyoeleza, napata tabu kuamini ukweli wa taarifa hizi ikiwa unasema huo ujazo wa trilioni 57 haujaguswa hata tone!
Haijaguswa HATA TONE!

REMEMBER: Gas ambayo ingechimbwa ilitakiwa kuwa processed pale Lindi kwenye ile plant ambayo ingegharimu USD 30 Billion!! Je, umeshawahi kusikia kwamba kiwanda kimeshajengwa?! Na kama hakijajengwa, hiyo gas inachakatwa wapi?
Sijui kama ni kweli, pengine unisaidie kujua zaidi, ile 1.3t ya Songas, mpaka sasa inafanya kazi gani na hiyo ya Mtwara inatokea wapi? Kisha uniambie Tanesco wanatumia gesi ipi pale ubungo na Kinyerezi.
1.3TCF sio ya SONGAS peke yake bali ni jumla ya Gesi ya Songosongo ambayo ndo inatumika na hao SONGAS/PAN AFRICAN pamoja na Gesii ya Mtwara ambayo inatokea Msimbati!

Ile ya Songosongo chini ya SONGAS ndio inazalisha umeme pale Ubungo na ile ya MTwara/Msimbati ndiyo inazalisha umeme pale Kinyerezi!!!

SONGAS ni mradi wa ubia kati ya serikali kupitia TANESCO na TPDC pamoja na private investors. However, majority shareholder ni kampuni yenye HQ yake Uingereza.

Gas ya Msimbati/Mtwara ndiyo inazalisha umeme pale Kinyerezi, na huu ni mradi wa serikali, kupitia TANESCO!!

Hivyo basi, kwa sasa zaidi ya 50% ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi ya Songosongo (Songas) na Msimbati (Kinyerezi).
Pia, unapozungumzia Processing plant ya Lindi, sijui kama umeelewa vizuri ni nini kinaenda kufanyika pale, CNG ndo kinachoenda kufanyika, sio kuchimba!
Sasa kwani nimesema hapo ndo wanachimba wakati hata jina tu linasema "processing"?!

Gesi inachimbwa baharini! Ile inayochimbwa ni raw gas, kwahiyo LAZIMA iwe processed, liquefied na ndipo unaweza kuisafirisha ama kwa mabomba (na ndo maana lile bomba linalotoka Mtwara ni kubwa mno kuliko matumizi yake kwa sasa) au kwa meli for export!

Sasa hiyo kazi ya uchakataji ndo ingefanyika Lindi! Kwavile Lindi na Mtwara peke yake zimegundulika zaidi ya 47TCF, wakaamua kugawana uchumi... Lindi wana-handle processing, na Mtwara wana-handle transportation for export kupitia bandari!
Kwa hoja hizo, nikuombe u-share hiyo mikataba hapa uliyoisoma ili kila mtu atafsiri anavyoelewa yeye kwa afya ya mjadala.
Mikataba ipi wakati unaambiwa hadi sasa hakuna kilichofanyika?!

Mchakato uliofanyika na kukamilika hadi sasa ni EXPLORATION. Hapa kwenye exploration kila kampuni imefanya kwenye vitalu ambavyo ilipewa leseni kufanya exploration. Hata hivyo, kampuni husika kugundua gas haimaanishi ndo tayari ana umiliki wa hiyo gas!

Hatua ambayo ingefuata ni uuzaji wa vitalu ambavyo TAYARI vimeshathibitika kuwa na gas. Of course, wale waliogundua gas kwenye plots husika bila shaka ndio wangepewa priority ya kununua hivyo vitalu!

Hata hivyo, kwa mujibu wa Gas & Petroleum Act 2015, sio kwamba wanamilikishwa hivyo vitalu bali mmiliki halali wa hivyo vitalu ni TPDC kupitia National Oil Company!!

So, Kampuni X ikishinda tenda ya ununuzi wa Kitalu husika, National Oil Company mwenye kitalu chake anatakiwa na umiliki wa at least 25% na asilimia inayobaki inaenda kwa mwekezaji!

Lakini faida watakayopata NOC haitatokana na 25% pekee bali itatokana pia na mgawanyo wa faida kama watakavyokubaliana.
Taarifa za kuhusika kwa wachina na JK zilikuwepo na hazikuwahi kukanusha na ama serikali au familia, zaidi akiwa madarakani na ilihusishwa na madawa ya kulevya, ni vyema sasa ukatanabaisha kama ndio UNAKANUSHA rasmi na ni kwa niaba ya nani!
Hivi mambo ambayo yalikuwa yanasemwa kuhusu JK kama wangeamua kuanza kukanusha si ingekuwa kila siku wanafanya kazi ya kukanusha?! Nikupe mfano wa wazi kabisa...

Je, hatukuambiwa kwamba JK kaiuza Kigamboni kwa George Bush, na wanataka kujenga kambi ya jeshi?!

Je, ikiwa miaka kibao imepita, unaona dalili yoyote ya Kigamboni kuuziwa Bush, au Kigamboni kujengwa kambi za jeshi la Marekani?
JK kumtaka JPM, pia matendo yaliyoonekana hayakusema hivyo, zaidi yalitueleza kuwa jina la JPM ilibidi litumike ku-neutalize situation iliyokuwa imejitokeza, hakuwa chaguo la yeyote kwa wale waliokuwepo kwenye madaraka.
Watu mlikuwa mnashindwa tu kusoma ramani...

Hebu nijuze kama kuna waziri yeyote ambae JK aliwahi kutembea nae sana mikoani kumzidi JPM?! Hata wizara yake ndiyo ilikuwa inapendelewa zaidi kwa kupewa fungu kubwa maradufu compared na wizara zingine!!

Kwamba ku-neutralize... hivi unadhani JK hakufahamu bifu kubwa kati ya Wafuasi wa Lowassa na wale wa Membe?! Unadhani hakufahamu kwamba ukimkata mmoja, yule aliyekatwa hasira zao watazihamishia kwa asimu wao?!

Ile ilikuwa ni well calculated and excuted plan! Ili kumfurahisha Salma na Best Friend Bernard, Lowassa akakatwa, akaachwa Ben! Wafuasi wa Lowassa hasira zao wakahamishia kwa Ben!
JPM alisema, gesi imeuzwa, haya yalikuwa ni maneno ya raisi wa nchi mwenye vyanzo vingi vya taarifa, zaidi ya yeyote humu! Na hapa sizungumzi issue ya maamuzi ya mtu binafsi, nazungumzia utoaji wa taarifa!
Sasa kama anajua imeuzwa, kwanini serikali yake ilikuwa inaendelea na mchakato wa ujenzi wa processing plant?!

Kwanini 2019 wakataka kupitia Production Sharing Agreement?!

The problem mlikuwa mnamwamini sana JPM, na sie wengine tukiwaambia JPM ni mwongo, watu wanasema tuna chuki!!

Narudia, HAKUNA UKWELI WOWOTE kuhusu gas kuuzwa!!!
Suala la JK kulinda maliasili za taifa kwaajili ya taifa kwa ujumla, hili hutakaa unishawishi, sitakubali asilani!
Mosi sijasema popote kwamba yeye ndo bingwa wa kulinda mali asili ya taifa, bali nilichosema ni kwamba GAS HAIJAUZWA!!

Na wala sikulazimishi ukubali, lakini lililo wazi hadi sasa, WOTE niliowaomba waweke hapa hiyo sheria mbovu wameshindwa kuweka, lakini nami nikaweka sheria ya 2015 inayosema:-
1. Mmiliki wa Vitalu ni Serikali
2. Serikali atakuwa na at least 51% SHARES of NOC, na NOC anatakiwa kuwa na angalau 25% of each block though itategemeana na uwezo wa NOC

3. Profit sharing Model inaonesha at least 50/50 lakini ukiisoma vizuri, percent ya serikali itakuwa inaongezeka kadri total production costs zitakavyokuwa zinapungua mwaka hadi mwaka!!

However, it's upon negotition.

Hata hayo hapo juu, wala SIKULAZIMISHI kukubali ingawaje nikikuambia unioneshe sheria nayofanana na hiyo kutoka kwa Mlinzi Wetu Mkuu wa Raslimali za Taifa, yaani The Late JPM, sidhani kama utanionesha!! HUtanionesha kwa sababu HAIPO, manake sheria yake bora kabisa ni ile ya Mrahaba 5% hadi 6%, na percentange ownership ya 16%!

Mwenye macho haambiwi tazama!!
Lililowazi ni kuwa, nchi ilisimama kwa ujumla wake ili waliowake waneemeke, na hata baada ya miaka 10, wengi wakishangilia uwepo wa pesa mtaani, na haswa kwa majiji makubwa tu, ambazo kimsingi zilitokana na matumizi ya ovyo ya walio wake huko mtaani.

Nchi ikabakia pale pale, huku wachache wakimiliki pesa kuliko nchi.

Maendeleo ya kweli na ya ujumla ni gharama, na gharama hiyo ndio wachache wanufaika wa mfumo wa kinyang'anyi hawako tayari kuzikubali.

Kazi iendelee, inaendeleza pale alipoishia JK, pengine mngetupa taarifa za nchi ilipo kimaendeleo na kimadeni kisha baada ya miaka 5 mje tena na taarifa za nini kimefanyika, tulipotekea, tulipo na tunakoelekea ili sisi tujue kama kuna chochote kimefanyika.

Miaka 60 bado tunazungumzia kuwa na vyoo bora na madawati, tunazungumzia umeme wa 1600MW tu kama nchi yenye 945,000km2! Tunazungumzia bajeti ya 32trillion ambapo, uwezo wa ndani ni 18trillion tu, na hapo 80% inatumika kuendesha serikali, maendeleo ni 5%
No comment!!
 
Back
Top Bottom