The muderous Dictator will not take this lightly. Kagame anatumia msamiati wa genocide kutafuta sympathy na kutaka watu wake wa-rally Behind huku ikijulikana kama alivyotoa ushahidi Jenerali Kayumba Nyamwasa kwamba yeye ndiye aliyeamuru ndege iliyowabeba marais wa Rwanda na Burundi itunguliwe na genocide ikaanza. Pia alitoa ushuhuda mahakamani huko SA kwamba Kagame ndiye aiyeamuru na kutekeleza mauaji ya Laurent Desire Kabila.
The bloody thirsty dictator is paranoid!
Mkuu, umeanza lini kujenga hoja zisizo na utafiti..? Kama ndege ilitunguliwa na wanajeshi, kwa nini Jeshi la Hyabyarimana liligeukia raia wasio na hatia? Najua we' ni mtaalam wa Politics na International Relations, unawezaje kusema genocide ni msamiati tu unaotumiwa na Kagame na si kweli kwamba waafrika wenzio kwa maelfu waliuliwa? Inawezekana Kagame aliamuru ndege itunguliwe, lakini tukubali kwamba zile machete na ile list ya 'cockroaches na traitors' viliandaliwa mapema na genocide ilikuwa planned kabla ya ndege kutunguliwa.
Naomba ujifunze vizuri kuhusu maisha ya Kayumba Nyamwasa na kwa nini alitofautiana na Kagame wakati walikuwa marafiki wakubwa kabla na kipindi fulani baada ya kuchukua nchi. Pia, fanya utafiti na ujielimishe kuhusu aina na chanzo cha uasi wa M23 nchini DRC. Najua haya yote yako katika uwezo wako kuyafahamu vizuri lkn umechukuliwa na upepo wa 'uzalendo' ukaacha facts.