President John Magufuli: A Model Leader in Africa for Employing Science in Politics

Bess

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
542
649
Chombo cha habari za kimataifa CGTN chenye makao yake makuu Nairobi kimemtaja Rais Magufuli kama kiongozi wa kuigwa katika Afrika.

Uchambuzi huu umeonesha kwamba sio kila mwanasiasa anaweza kusema uongo kwenye siasa na kutoa ahadi hewa za kujenga daraja hata pasipokuwepo na mto. Mwanasiasa anaweza kutumia njia za kisayansi kuahidi na kutatua matatizo kiuhalisia.

The former Soviet Union’s Premier, Nikita Khrushchev opined that “politicians are the same world over: they promise to build a bridge even when there is no river”.

Ametambuliwa kama mfano hata wa viongoz wa Afrika kwamba taaluma yake ya sayansi ya kemia imemfanya afanye na kusema vitu dhahiri, nje ya nadharia za taaluma ya sanaa.

"Magufuli ought to be remembered in Africa in the way he has attempted to employ a science-based approach to implement political promises"

Takwimu zinaonesha pasi na shaka kwamba ameweza kutekeleza wastani wa asilimia 70 ya ahadi zake wakati wa kampeni mwaka 2015

The style in the dispensation and implementation of his political agenda is influenced by his background as a top-notch Chemist

Tarehe 20/11/2015 alifungua bunge la jamhuri ya Muungano na kueleza changamoto 20 alizokusanya wakati wa kampeni, tarehe 16/06/2020 alipohutubia bunge alieleza maendeleo makubwa aliyofikia katika kukabiliana na hizi changamoto

Moja kubwa ni rushwa: Kupitia taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa takribani Tsh. 272.38 bilioni na imesajili kesi 2256 kwa mda wa 2015-2020.
Na sasa imejengeka hofu kuu kabla ya kupokea ama kutoa rushwa kubwa kwa jamii ya kiTanzania.

Aliahidi elimu bure kutoka elimu ya msingi hadi kidato cha nne. Hii imeongeza idadi ya wanaojiunga kidato cha kwanza kutoka asilimia 56 mwaka 2025 hadi 87.7 mwaka 2020

Sekta ya afya ilikuwa inakumbwa ukosefu wa dawa, vifaa na wahudumu. Wakati wake hospital mpya 71, na vituo vya afya 487 vimejengwa; vituo 1198 viko mbioni kukamilika.

Huduma ya maji vijijini imekua kutoka asilimia 47 hadi 70.1 na mijini upatikanaji wa maji umefikia 84% kutoka 74% mwaka 2015

Utawala wa Jpm haujaongeza tu uzalishaji wa umeme kutoka MW 1,308 mwaka 2015 hadi MW 1,602, bali pia umehakikisha usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini. Vijiji 9,112 sasa vina umeme kutoka vijiji 2081 tu mwaka 2015. Pia gharama ya uunganishaji pamoja matumizi imepungua sana enzi ya utawala huu. Hii imesaidia kukuza sekta ya viwanda vidogo vidogo katika maeneo mengi ya nchi

one cannot take away his shrewdness and intellectualism of using science in the implementation of his political agenda. His leadership mission is destined to triumph because he does a proper diagnosis of the problem and lays down proper strategies to resolve it.

Anasifiwa kuingoza Tz kufikia lengo la uchumi wa kati miaka 5 kabla ya mda uliopangwa

Jumuiya ya kimataifa pamoja na kumkosa, linapokuja suala la tathmini ya kina kuhusu uchumi wa nchi huishia kusema 'Thumbs up to the Bulldoze'

President John Magufuli: A Model Leader in Africa for Employing Science in Politics
 
Nilifikiri CNN ,FOX news, BBC, Likes of television za russia au china.
Sky news. Hivyo ndio vyombo vinavyo angaliwa sana na kusikilizwa sana.
Hizo local channel bado sana. However si vibaya kutangaza mazuri ya mhe.rais
 
UTAFITI FAKE kwanini tuukubali? Hujasikia vilio vya Wafanyakazi, Wakulima, Wafanyabiashara, Wahitimu wa vyuo etc? Hao kwenye huo utafiti WALIHOJIWA? Au walikurupuka na kuandika upuuzi wao ambao uko biased?

Herufi 11 za haya maneno haziwezi kuwa kipimo cha kujibu andiko la kiutafiti.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza
Yanayoendelea ndani ya nchi wanayajua wenye nchi wengine ni kelele za udwanzi kwenye masikio ya maskini vijana wazee wamama wakulima wafanyakazi na wafanyabiadhara waliopo ndani ya nchi.
 
Hawajawahi kumsikia Magu hawa jamaa, may sababu muda wote anatumia kiswahili hawajui anachoongea. Ngoja siku wamsikie anaongea kiingereza and awaambie Xi ni rais wa N. Korea and Kim ni rais wa China.
 
Nitakusoma nikiwa na nafasi. Kwa Leo nimechukia baada ya kukusoma sentesi chache na kughundua ujinga mwingi.
Ujinga ni kutokujua kitu, inawezekana ww ndio huna habarr ya kilichoandikwa
 
Back
Top Bottom