President Banda insists Lake Malawi is for Malawi not Tanzania

Huyu Mama mbona hatulii! Kama anajihakikishia Ziwa lote ni lake kwa nini kila siku anapiga domo. Aondoe Ushoga nchini kwake kwanza.
 
sisi hatuna shida ila ajue tu kuwa tuko katika hatua nzuri ya maandalizi...na mda ukifika asitafute mchawi....
 
Mbona hasemi na upanda wa mozambique pia ni wake?!!!

Huyu mama bana!!!
 
ICJ ndio mwamuzi wa suala hili. Tulipeleke mahakamani haraka iwezekanavyo.Hatutaki vita sisi wote ni black race. Tusiuwane sisi ni ndugu moja.Pan-africanism itumiwe katika maeneo kama haya na si vita.
 
Juzi aliwaalika wanadhimu wa kijeshi wa USA, nadhani wamezidi kumpumbaza kuwa atashinda mgogoro huu,

Banda nikuhabarishe tu kuwa Tanzania ni super military kwa afrika mashariki na kati!

Tanzania ni nchi ya kwanza afrika na ya 6 duniani kwa uwezo wa kupigana vita vya ardhini, kwa afrika ni ya kwanza!

Hatutaki vita, tunataka suluhu ya mazungumzo!
 
Katika comments za hawa jamaa nimeona matusi ambayo jamaa mmoja kachangia kuwa Tanzania ni taifa la wajinga kwa vile ni nchi pekee yenye wingi wa madini lakini inaongoza kwa umasikini.
Kwa kweli nimeumia sana kwa ukweli huo.Hivi tutaendelea kutukanwa na kebehi kibao kutoka kwa mataifa hata dhaifu kama malawi mpaka lini?
Kwa nini hatuchukui hatua kwa wanaotusababishia tudharaulike duniani kwa sababu ya wao kubebana?
Kwa kweli kama mtu bado anaweza kusimama wima na kutetea utawala huu na wakati huo yeye si sehemu ya utawala basi huyo anamapungufu akilini. Hatuwezi kuendelea kutukanwa katika ukweli tunaoweza kuubadilisha.
 
ICJ ndio mwamuzi wa suala hili. Tulipeleke mahakamani haraka iwezekanavyo.Hatutaki vita sisi wote ni black race. Tusiuwane sisi ni ndugu moja.Pan-africanism itumiwe katika maeneo kama haya na si vita.

No ...!! A thief, black one, unamwache akuibie unamwona mchana then unasubiri ICJ....!!?? Uko nyuma sana kwa hili..??

Mwizi wa Ziwa letu eti achukue lote...!!!! Dawa tunampa muda hakuna cha ICJ wala nani...!!! Akiendlea kuleta ubishi aguse hata meter moja ya upande wetu aone...

Muda ukiisha hataki nusu kwa nusu tunachukua ZIWA NYASA LOTE NA SI ZIWA MALAWI AS NAMED...!!

Ni masaa tu tunamvua underware huyu... ngoja..!!

Mwacheni acheze kwanza...!!
 
ICJ ndio mwamuzi wa suala hili. Tulipeleke mahakamani haraka iwezekanavyo.Hatutaki vita sisi wote ni black race. Tusiuwane sisi ni ndugu moja.Pan-africanism itumiwe katika maeneo kama haya na si vita.

sisi hatuwezi kushitakiwa huko...ndani ya ICJ kuna waraka unatakiwa usaini unaowezesha wewe kushitakiwa na mwanachama mwingine ambapo tanzania haikusaini hivyo malawi hawezi kutushitaki huko.
 
Kila lakheri ndugu yangu kama wewe una advocate vita. Vita ya Uganda hadi leo makovu yetu hayajapona wewe unafanya ushabiki wa vita au unafikili vita ni mchezo. Halafu lazima ujue Dunia hii ina super nations, Nchi yetu si kubwa kiasi hicho.Tukianza vita kuna baadhi ya viongozi wataanza kutafuta namna ya kuiba.
 
Siku hizi nguvu ya jeshi ni vifaa va kisasa kama drones ,missiles shield,zinazozuia makombora na vifaru kulipuliwa,jeshi la ardhini linakuwa linaenda kumalizia ghasia zilizobakia baada ya kikosi cha anga kufanya mashambulizi xo dont underestimate ur enemy,u don't know what he is capable of,let us be alert,tujiandae kwa lolote litakalotokea,i believe jeshi letu liko vizuri ila tusijisahau kwa kujiona tumefika hakuna nchi inayotuzingua

Juzi aliwaalika wanadhimu wa kijeshi wa USA, nadhani wamezidi kumpumbaza kuwa atashinda mgogoro huu,

Banda nikuhabarishe tu kuwa Tanzania ni super military kwa afrika mashariki na kati!

Tanzania ni nchi ya kwanza afrika na ya 6 duniani kwa uwezo wa kupigana vita vya ardhini, kwa afrika ni ya kwanza!

Hatutaki vita, tunataka suluhu ya mazungumzo!
 
Mwacheni mama wa watu si unajua tena hata Umoja wa Nchi za Ulaya wameshamwambia apunguze safari za nje na matumizi makubwa ya serikali yake, kwa hiyo anataka kutumia ziwa Nyasa kuwapotosha wananchi wake
 
Juzi aliwaalika wanadhimu wa kijeshi wa USA, nadhani wamezidi kumpumbaza kuwa atashinda mgogoro huu,

Banda nikuhabarishe tu kuwa Tanzania ni super military kwa afrika mashariki na kati!

Tanzania ni nchi ya kwanza afrika na ya 6 duniani kwa uwezo wa kupigana vita vya ardhini, kwa afrika ni ya kwanza!

Hatutaki vita, tunataka suluhu ya mazungumzo!

Kiongozi wa hao wanajeshi aliwashushua wamalawi walipoingiza ishue ya mpaka kwenye mazungumzo yao. Alisema Marekani ni rafiki wa nchi zote mbili za Tanzania na Malawi - hivyo hawataki kuingizwa katika upande moja wa mgogoro huo. Alisema wataunga mkono jitihada za kutatua bila vita.
 
Kila lakheri ndugu yangu kama wewe una advocate vita. Vita ya Uganda hadi leo makovu yetu hayajapona wewe unafanya ushabiki wa vita au unafikili vita ni mchezo. Halafu lazima ujue Dunia hii ina super nations, Nchi yetu si kubwa kiasi hicho.Tukianza vita kuna baadhi ya viongozi wataanza kutafuta namna ya kuiba.
Kwa kuamini kwako kuwa umasikini wetu unatokana na vita vya uganda inaonyesha jinsi gani ulivyo kilaza..! The only issue is corruption, jiulize inakuwaje mtanzania mmoja amiliki trilion 3 za wizi na mtu huyo anaheshimika nchini? Halafu calculate the total sum lost ndo utajua kama unastahili kuwa na makovu au laa.
 
Huyu mama anamdharau sana JK na Tanzania kwa ujumla. Solution ni kumchapa tu na kumwondoa madarakani kabisa kama Amin.
 
Naona wewe Kifarutz hujaelewa mantiki yangu. Ninachojaribu kukwambia ni kwamba usishobokee vita.Kwani wanasiasa wenu baadaye watapata sababu ya kusingizia umaskini wetu katika vita hiyo.Na pia wakati wa Vita pesa nyingi sana huwa zinaibiwa na wajanja wachache hasa viongozi.Soma report za dunia kuhusu utoroshaji wa pesa, kipindi cha vita ya Uganda na Tanzania pesa nyingi sana iliibiwa na Viongozi wetu.Mimi mtu wa kijijini ambaye umaskini kwetu umetamalaki siwezi hata kidogo kushobokea vita kama wewe unavofanya.Kama mnapesa namna hiyo za kupigana vita si zitumieni kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima na jengeni shule za kutosha ili tupate maendeleo makubwa. Acha hizo. Vita hailipi kwa taifa maskini kama hili. Mnataka kuwapa faida wauza silaha.
 
Kwahiyo - Tuachie Ziwa , Wilaya ya NGARA Kwa Rwanda. Kagera - Uganda na Arusha kwa Kenya, Be a greater thinker
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom