Pres.Obama(Miaka 4,safari-32),Pres.JK(Miaka 7,safari 392),Hayati Nyerere(Miaka 25,safari 68)

Huenda huenda kujitibia. Maana sioni zaidi ya hili kama siyo kukagua miradi au kuweka pesa Uswisi. Mwenye jibu tofauti na hili anisaidie. Hapa hujahesabu trips alizopiga akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje kwa miaka kumi! Kweli rais bomu tunaye!
 
JK asiposafiri tutakufa njaa....kwa hiyo safari zake zina tija kwa taifa.
 
"wapo wanaobeza safari zangu ; hawajui bila safari hizi watanzania watakufa NJAA" by dr dr dr J.kikwete
 
Tutajie maendeleo yaliyopatikana kwa Nyerere kutokusafiri, Subirini tufe ndo mje kupndisha Historia tunajua 1985 nyerere anaondoka Ikulu bidhaa zote za msingi zilikuwa zinaitwa Bidhaa adimu unga, mchele, sukari, dawa ya meno zilikuwa zikipatikana kwa kibali cha mjumbe tena baada ya kuhakiki idadi ya wanakaya kumbuka hapo sio unapewa bure bali unanunua, watu wamevaa Sanda wakiwa hai kwa kukosa nguo halafu mnadanganywa eti nyerere kang'atuka kaacha viwanda labda vya kuzalisha Propaganda, kama uchache wa safri ndo maendeleo leo Jk asingekuwa anazungumzoa kujenga barabara, shule,madaraja maana hao mnaowaota wangekuwa washajenga, kama mpaka leo wanaopata umeme ni 14% ya wa TZ hivo viwanda vilijiendesha kwa kutumia samadi? Jk senior na Jr ndo wale wale labda kama mna ajenda mloificha kwapani!
 
zubedayo_mchuzi Obama miaka 4 safari 32 wastani safari 8 kwa mwaka, akikaa madarakani miaka 7 safari 56, Mheshimiwa sana Jk miaka 7 safari 392, wastani mwaka 1 safari 56.
 
Last edited by a moderator:
zubedayo_mchuzi madai yake anaenda kutembeza bakuli wanawe wasife na njaa huku nyumbani ila cha ajabu kila anaporudi hatuelezwi kinachopatikana zaidi ya bla bla tulizozizoea
 
Last edited by a moderator:
wewe Songoro lazima utakuwa ni mtoto wa dhaifu. kwani dhaifu ndio amezileta bidhaa hizo madukani?? zote zilikuwepo madukani,kilichoongezeka ni ufisadi, watu kuichukia zaidi ccm na polisi na kampuni za rizmoja basi. kati ya watu wamewahi kuandika pumba ni wewe.huyo anaingia madarakani petrol ilikuwa tshs 630 tu, miaka saba yake ya ikulu imefika tshs 2050!! hakuna mtu mwenye hamu nae labda ma.. mu zake tu.
 
Last edited by a moderator:
kama Nimekosea hapo mtanisahihisha.

Rais Barack Obama,amekaa ikulu kwake miaka 4,Amesafiri safari 32,

Hayati Baba wa taifa,amekaa ikulu miaka 25,amesafiri safari 68.

Rais Wa Sasa wa Tz(Dk Jk),ikulu miaka 7,safari 392..

Je hizo safari huwa zinatija kwa Taifa?
Hivi mkuu hizi takwimu ni sahihi kweli?Nashindwa kuamini!Mkuu tupe source ya data zako.Kama ni kweli hi ni kashifa na aibu kubwa kwa Jk.Nini kinaweza kuhalalisha ubadhirifu huu wa fedha za umma kwa safari zisizo na uthibiti.

Hivi CAG huwa anakagua matumizi ya fedha zinazopelekwa ikulu?Kama anakagua taarifa hiyo huwa inapelekwa bungeni?Mimi naona bunge limpe CAG mamlaka zaidi ili kama ikulu inatumia vibaya fedha za walipa kodi basi iwe na nguvu za kisheria kudhibiti matumizi ya fedha zinazopelekwa ikulu.Huu ni ufisadi kama wa TANSCO,bandari na kwingineko kwa kisingizio cha safari za raisi.Haya ni matumizi mabaya ya madaraka.Anastahili kudhibitiwa.

Kupiitia katiba mpya tuweke utaratibu wa kudhibiti safari za viongozi wakuu wa nchi maana huu ni upuuzi uliopitiliza.
 
Anaenda birthday, kupumzika , kusalimia jamaa, kuomba msaada wa ccm na kujijenga

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Magufuli...SAFIRI SANA RAIS WETU, BILA KUSAFIRI HIZI BARABARA TUNGEPATA WAPI?
WAPO WANAOKUBEZA KWANINI UNASAFIRI SANA, HAWAONI BARABARA HIZI?
haya ni mawazo ya msomi mwenye phd pale UDSM.
afu hawa nadio tunadhani wanafaa kutuongoza.watauza nchi hawa
 
JK ni mtaka yote....., hata mikutano/washa/semina/makongamano yasiyomhusu yeye yupo. Anakula good time maana ndo muda wake na kazi yake, presha za wananchi haziko kichwani mwake. Anawaza kuku na bata tu.
Pitia na hapa <http://jasonbournetz.wordpress.com/>, unaweza kupata picha ya Kitu mtoa mada anasema.
 
Hizo safari za JK ni pamoja na zile za Kwenda Mtwara na Lindi ndiyo maana zimekuwa nyingi kuliko za Obama.
 
Malengo makuu ya safari za Kikwete:
1/Kuomba misaada ya kibinadamu na kiuchumi.

2/Kuomba kusamehewa madeni.

3/Kuvutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza nchini.

4/Kutangaza vivutio vya kitalii na Kuvutia watalii wa kigeni.

5/Kuhudhuria mikutano, makongamano, warsha, semina na matukio ya kimataifa.

6/Kwenda kuonana na watu maarufu kisiasa, kimichezo, kimuziki, kiuigizaji, kimitindo.

7/Kuhudhuria mafunzo ya kiuchumi, kijamii nk.

8/Kwenda kutia saini mikataba mbalimbali ya kiuchumi na kimataifa.

SOURCE: IKULU.
 
Mkuu,
ni vigumu sana kuchangia mada yako kwa sababu hujaiboresha kwa kueleza hizo data zimetoka wapi na safari kama ni za ndani au nje ya nchi.

Ninachoweza kusema, safari za Rais wa Taifa la Marekani lazima tu zitakuwa ni chache kulinganisha na viongozi wa nchi za Afrika hasa Tanzania kama ulivyodokeza. Ikumbukwe kuwa safari ya Rais wa Marekani inaanza kuandaliwa muda mrefu kwa kutanguliza watu wake wa usalama, vifaa vya ulinzi na usafiri wa Rais na watu wake kama mwezi au miezi kabla ya safari kulingana na sehemu au nchi anayokwenda, kwa maana hii, gharama ya ulinzi na umuhimu wa safari ni mambo ambavyo yanapewa kipao cha mbele sana kwa vile Taifa la Marekani ndilo kubwa na lenye nguvu ulimwenguni. Labda tu tujikumbushe jinsi maandalizi ya safari za Rais wa Taifa la Marekani zinavyoratibiwa kiusalama





Ni kweli bila udadavuzi, kwa kuangalia kwa nje, safari za Rais Jakaya Kikwete tunaona kama zimekuwa ni nyingi, ni vigumu pia kuchanganua faida au tija zinazopatikana katika safari za Rais wa Taifa la Marekani ukilinganisha na Rais wa Tanzania kwa vile sababu na madhumuni ya safari zao kisiasa na kiuchumi ni tofauti kabisa.

Hatuwezi kukubali au kukanusha kuhusu uwingi wa safari kati ya Rais Mwalimu Nyerere na Rais Jakaya Kikwete lakini vilevile kumbuka kipindi cha Nyerere dunia ilikuwa tofauti sana kisiasa na kiuchumi (two block) ukilinganisha na sasa ambapo nchi karibu zote ziko kwenye siasa ya aina moja yenye kuchagizwa na uchumi wa soko huria kwa maana kwamba nchi nyingi duniani kwa sasa zimekuwa karibu kimahusiano katika nyanja za siasa na kiuchumi. Safari za Rais Mwl. Nyerere kipindi kile zilikuwa ni kuzitembelea nchi hizo chache zenye mahusiano ya kisiasa na kiuchumu miongoni mwao (Eastern block) na hata malengo na madhumuni yake yalikuwa tofauti na sasa.
 
Last edited by a moderator:
zubedayo_mchuzi
is
images
images
images


Mizunguko huko ulimwenguni ina raha zake kukutana na hawa
kuliko majukumu yaliyomo ndani ya mipaka ya Tanzania?
 
Last edited by a moderator:
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom