Pres Jakaya Kikwete, You have made us proud!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,803
13,033
Nimefuatilia kwa makini mazishi ya Madiba huko Qunu kupitia luninga.

Kati yawatu wachache walio alikwakutoa hotuba katika mzishi hayo ni JK.

Nimefika South Africa miezi michache iliyopita n najua hisia za wananchi wa SA kwa waTanzania.

Niko bar sasa hivi na wachangiaji walio wengi wameridhika na uawakilishi wa JK katika mazishi ya mzee Madiba pamoja na hotuba ya kusisimua aliyoitoa na ambayo hata CNN wamekiri kuwa ilipendeza.

Mwisho wa yote ni kuwashukuru waTanzania wote kwa ushiriki wao katika ukombozi wa Afrika ya kusini,

=======

This article is worth reading: Bravo Kikwete for putting Mandela’s story in a Proper Context!


=======

Kwanini Hotuba Ya JK Kumuaga Mandela Ilikuwa Bora?

Ndugu zangu,

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela.

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'.

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia.

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru, Thabo Mbeki baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa.

Usiku Mwema.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
 
Hongera kwa kutuarifu kuwa upo huko na ulifanikiwa kwenda kutuwasilisha katika mazishi. Ila kiukweli, inaonesha ulishakunywa saana vinywaji hivyo vya bure huko kwenye mazishi. Bure mbaya
Leo, umebadili kiroba ndo maana hata huku edit habari yako. Pole
 
Nimefarijika na hotuba ya Raisi wangu na kuiona thamani yangu kwa wa Afrika kusini! Tatizo langu mm na yeye ni hapa nyumbani tu!
 
Hizi ni sera za TANU/CCM chini ya Nyerere,mambo ambayo Mtei na chadomo hawapendi.
 
Hongera kwa kutuarifu kuwa upo huko na ulifanikiwa kwenda kutuwasilisha katika mazishi. Ila kiukweli, inaonesha ulishakunywa saana vinywaji hivyo vya bure huko kwenye mazishi. Bure mbaya
Leo, umebadili kiroba ndo maana hata huku edit habari yako. Pole

Nilifika huko na na nilisha rudi bongo.
 
Ukweli siku zote hung'ara popote pale duniani. Ahsante sana Mkuu @NyakaiIkagogo. RIP Mwalimu matunda ya utendaji wako bado yanaonekana duniani hata baada ya miaka 28 tangu ung'atuke.

Matunda ya Mwl. Nyerere!
 
JK speech was very poorly prepared,a lot of grammatical errors.Akili za mwandishi wake alishindwa kuchanganya na zake.naona Mulugo syndrome inafanya kazi hata kwa JK
 
Jk anajua kuicheza karata yake linapokuja suala la kimataifa
hakupoteza nukta kuitangaza Tanzania
Though kuna utata ni lini Mandela aliingia Tanganyika ni February 1962 Nyerere akiwa waziri Mkuu
au ni miezi ya mwisho ya 1962
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom