Premier League imefuta mechi kadhaa kutokana na ongezeko la maambukizi, pamoja na wachezaji wengi kujiweka karantini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,497
9,278
Wakati aina mpya ya kirusi cha corona kinachofahamika kama Omicron kikiendelea kusambaa kote Uingereza, ligi kuu ya Premier League ya England imefuta mechi kadhaa kutokana na ongezeko la maambukizi, pamoja na wachezaji wengi kujiweka karantini.

Mechi ya leo kati ya Leeds United na Aston Villa haitaendelea baada ya mechi ya Leeds dhidi ya Liverpool iliyopangwa kuchezwa jana kuahirishwa.

Mpambano wa Wolves na Arsenal pia hautochezwa leo. Wolves iliomba usogezwe mbele kwa sababu haina idadi ya kutosha ya wachezaji kutokana na Covid na majeruhi.

Mechi ya Wolves dhidi ya Watford tayari ilikuwa imeahirishwa. Kwa jumla Premier League iliahirisha mechi 15 katika kipindi cha wiki mbili na nusu zilizopita kutokana na visa vya viruso vya corona katika timu mbalimbali.

Suala hili limeibua mjadala wa kuruhusiwa kutumika wachezaji watano wa akiba badala ya watatu kama ilivyo kwa sasa, na makocha wengi wamepaza sauti zao wakiwemo Thomas Tuchel, Patrick Vierra, Ralf Rangnick na wengine wengi.
 
Mechi za Arsenal watuache tucheze hiki kipindi ni cha bahati kwetu wasituvuruge.tushaumizwa sana hiki ni kipindi cha kukonga nyoyo.
 
Back
Top Bottom