Pregnant idea.......thank you my friend......i love you my wife. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pregnant idea.......thank you my friend......i love you my wife.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Going Concern, Feb 22, 2012.

 1. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kwakua maisha mjini yalizidi kua magumu kulikua hakuna jinsi, tukaona turudi kijijini. Nilimpenda sana mkewangu, nikaona niende kukaa kwa kaka yangu naemfata. Walipendana sana na mke wake. Thanks god walikua wamepata katoto ka kiume baada ya kuishi miaka mitano kwenye ndoa….mtoto wao alikua anaitwa Jeff, alikua na miaka miwili. Siku moja My bro na mkewe walikua wanaenda mnadani kwani ilikua ni siku ya jumapili, ikabidi waniache nyumbani mimi, mkewangu na motto wao(Jeff).
  Ketendo cha kuondoka tu, nilitoa mkeka nje nikamwacha mkewangu jikoni anapika, nakumbika ilikua saa tano na nusu mchana. Nikiwa katika usingizi mtamu wa mchana nilishtushwa na mkewangu akiniita kwenda kula. Nilijivuta mpaka ndani nikaketi kwenye mkeka ili nipate msosi. Tulikula uku tukipiga story na wife mpka Jeff aliposema kashiba anaenda kucheza nje na kitoto cha mbwa ambacho tulikua tumekichukua siku tatu zilizopita. Pale nje tulikua tumeanika mahindi kwajili ya kupata unga, wakati tukiwa tumemaliza kupiga msosi nikawa nanapiga story na wife, pale nje kukaja njiwa wengi sana wakawa wanakula mahindi ndipo nilipo shika mpini wa jembe uliokua pembeni yangu, nikawarushia gafla akakatiza jeff akiwa anakimbizana na kile kitoto cha mbwa mpini wa jembe ukampiga kichwani akaanguka na kukata roho pale pale…………tulibaki tunatazamana na mke wangu tusijue nini cha kufanya…………..nilimchukua Yule motto nikaingia nae ndani na kufunga nyumba kwani hakuna mtu aliyeona kilichotokea…baaada ya kama nusu saa tuliona tumweke ndani na Kuwait mpaka usiku ili twende kumzika mstuni kwani bro na mkewake walikua wanarudi kesho yake kwakua walipitia kwa mjomba aliyekua anaumwa sana.

  Ilipofika usiku tulienda kumzika na tukasema hakuna kumwambia mtu kuhusu kilichotokea. Ilipofika kesho saa tano asubuhi tukaenda kwa mjumbe kutoa taarifa kua motto wa kaka kapotea, alikua anacheza asubuhi nyumbani then hatujamwona toka mida ile, wakati tunatoka kwa mjumbe, tulikutana na bro na mke wake wakiwa wamebeba nguo nzuri kweli za motto wao ambaye alikua ni kila kitu maishani mwao kwani walimpata baada ya kunywa mitishambia almost miaka mitatu.
  Nilimwambia bro jeff katoweka kwenye mazingira ya kutatanisha na tumemtafuta kila kona lakini hatujafanikiwa. Siwezi kusahau siku hiyo, kaka yangu na mke wake walilia sana, mie pia na mke wangu tukawa tunalia kwani tulimpenda sana Jeff na hatukujua mwisho itakuwaje.

  Mjumbe aliitisha kikao baada ya siku mbili, ikabidi kuzunguka kijiji kizima, mstuni, kisimani, chooni lakini mwisho wa siku Jeff hakuonekana……………….ilipita kama wiki mbili nikiwa siongei na kaka kwani alikua hataki ata kuniona, siku zote alikua anasema kwanini nimemuacha mototo mpaka kapotea?
  Pale kijijini kulikua na rafiki yangu wa siku nyingi, hakuna kitu nilikua namficha toka utotoni. Siku moja tukiwa tunaenda kuangalia mpira nikaona itakua vizuri nikimwambia ukweli kuhusu ile issue Ili anipe pregnant ideas kwani nilijua ipo siku tu mambo yatajulikana Na Mimi sikutaka yajulikane kwani bro angeweza kuvunja undugu Na Mimi Kama akijua ukweli, nilimwambia rafiki yangu mwanzo mwisho mpaka sehemu tuliyo mzika Yule mtoto…….

  Sikutegemea maneno aliyonambia, alisema kosa kubwa ni kitendo cha mkewangu kuona kilichotokea na kujua kila kitu. Akanambia “womens are pots, full of poison”. Akanambia kama nakumbuka sehemu niliyomzika Yule mtoto, nikamwambia nakumbuka, akasema ikifika usiku nimpeleke ye atajua afanye nini…….Usiku kwenye saa 7 nilitoka kimya kimya nikamwacha mkewangu usingizini nikaenda kwa jamaa tukaongoza mpaka sehemu tulipomzika jefff. Jamaa ailikua kabeba jembe na alikua kaongoza na Mbwa wake aliyekua anampenda sana. Jamaa akanambia hatuna mda wa kupoteza, tukaanza kuchimba mpka tukafikia ule mwili uliokua unatoa harufi kali sana, tukautoa na kuuweka pembeni……..kipindi iko mi sijuwi jamaa anataka kufanya nini ila nilijua atakua tu na pregnant idea……..gafla jamaa akampush Yule mbwa kwenye shimo na kumfukia mzima mzima…………..


  Tukatafuta sehemu nyingine mbali kidogo tukaufukia uli mwili uliokua unatoa harufu nzito mno.mida iyo ilikua ni kwenye saa 9 usiku, jamaa akanambia sasa hapa mambo ni shwaaaari……

  inategeme na comments za watu kama wanaitaji kujua zaidi, i will keep on posting......
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wewe kaka wewe? umen ishtua pole kwa mkasa nitarudi baadae maana tumbo limeniuma ghafla
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhh bora ungemalizia though so painful ila malizia ndo tujue tuongee nini hapa.
   
 4. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Daah mkuu ni halihalisi ilikutokea au ni story? Mi naomba upost full story kwani imevuta hisia zangu..
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mtalingolo umeona eehhh
  Yaani imevuta sana hisia kama ni hali halisi
  Maana duh inaumiza sana
  Mtu ametafuta mtoto for five years na anakuja kuambiwa amepotea
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  l am speechless! I know how hard it is for you and your bro; ila ingekuwa vyema even after sometime umwambie kaka yako, hata kwa kutumia watu wengine!
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Hata sitaki imalizia baada ya kusikia mtoto kapigwa na mpini.
  Anyway, shigongo atainunua na kuipolishi vizuri
   
 8. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Malizia story bana aaaaaaaaaahhhh!
   
 9. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  msiache kwenda kanisani leo jumatano ya majivu, kwa wale wenzangu RC
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Umeikopi wapi?
  Have read it somewhere....long time back.......
   
 11. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  umetumia vizuri katiba ya nchi yako uhuru wa kuongea,
   
 12. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  We mtunzi mzuri sana mkuu!
   
 13. RR

  RR JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160

  Surely nishaiona mahali.....
  Hata bila ya uhuri wa katiba....
  kwamba wanakuja kufukua na kukuta mbwa, ilhali mke keshasema ulimuua na kumzika hapo!
   
 14. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  oky, utamalizia, thn mi ntaendelea tutaona mwisho wake,
   
 15. RR

  RR JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160

  Hapo wataka kusema ni utunzi wako?
   
 16. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  hii iliwahi tokea tanga kuna mzee mmoja maarufu sana,
  Unajua wanawake wa tanga sio wakuwapa siri hata umpende na akupende vip mkigomba tu ujue mtaa mzima watajua.
  Basi huyo mzee amejaaliwa kipesa na anampenda mke wake siku moja akaja na nguo kazivalisha sanda ka maiti vile akamwambia mke wake huu mwili inabid tuuzike ndan ili isije gundulika wakaenda store wakachimba wakazika wakafukia kesho akamwita fundi akaja sakafia vizuri.
  Maisha yakaendelea vizuri wakajaza magunia ya mikaa kwa pale juu, baada ya muda jamaa akaanza kumletea vituko wife kamzingua mwisho akaja mfukuza wife akalia akaomba msamaha hakuna kitu akamwambia tutaona we si mjanja.
  Akaenda polisi kawaelekeza kila kitu khs kuzika mtu ndan ya nyumba jamaa anashangaa polis mjumbe wanakuja pale wakaongoza mpk store wakatoa mkaa wakaamuru pavunjwe wakachimba wakakuta sanda wakaamin kuwa kuwa kuna mait wameitoa wanakuta n nguo tu.
  Mke yakabak yamemshuka wakamuuliza kwa nin umefanya hv akawajibu nilikuwa napima kama wanawake wa tanga wanajua kutunza siri akamwambia mke wangu naomba urud tu nyumban nakupenda sana toka siku hyo umwambii kitu kuhusu wanawake wa tangu.
   
 17. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  turushie part 2 yake aiseee, ila pole kwa yalikusibu!
   
 18. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ndoivo kaka nimependa aimalizie kabisa hyo story...
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ahahaaa ningeomba talaka
   
 20. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Jamaa hajaweka part 2 mpaka sasa? Tuwekee bwana kaka.
   
Loading...