Precission kuipeleka mahakamani ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precission kuipeleka mahakamani ATCL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  Habari zilizoingia hivi punde zinasema wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya precission wanajiaandaa kuipeleka management ya ATCL
  mahakamani kutokana na kukaidi kulipa pesa za saccos ambazo wafanyakazi hao wamekuwa wanachama kwa miaka mingi..pamoja na wafanyakazi wa ATCL.

  A kiongea bila kutotaka kutajwa jina baadhi ya wafanyakazi walikusanyika jana wakiwepo wafanyakazi wa swissport na BP
  na kuamua kwa pamoja kuipeleka menejiment ya atcl mahakamani kuweza kupata haki zao.....

  Akizungumza kwa jazba mmoja wa wafanyakazi wa Swissport alisema namnukuu "UNAJUA SISI NI WANACHAMA WA CHAMA KIMOJA CHA KUKOPA NA KULIPA kijulikanacho kama WANAHEWA
  sasa kila tukienda viongozi wanatuambia wanaidai atcl million 425
  kila tukiombahata pesa kidogo tunakatiliwa kabisa wakati ni haki yetu na kusema pesa zote wameshikilia manegement ya ATCL..."

  Chanzo chetu kilijitahidi kumtafuta mkurugenzi wa ATCL bw David Mattaka bila mafanikio na kuambiwa yuko kwenye mkutano...
  habari zaidi zinasema baadhi ya wafanyakazi wa Swissport na Precission leo hii waliamua kwenda kumuona mkurugenzi na kukosa ushikirikiano... kibaya zaidi wakati tukiwa tunajitahidi kuendelea kujua ukweli wa swala hilli, baadhi ya wafanyakazi walikataa kabisa kujibu na kusema anayejua hilo ni Mattaka na management yake ...lakini ni kweli wanadaiwa hela nyingi tu na kibaya zaidi kwenye mishahara inaonyesha imekatwa wakati pesa hazipelekwi sehemu husika.....

  Nilijaribu kumpa pole dada yule na mwisho kumuuliza kama wafanyakazi mmelijua hili muda wote hamjui ni kosa la jinai kampuni kukata malipo ya mishahara ya mfanyakazi na kutumia bila ridhaa yalke ama mlijulishwa na kukiri hakuna kitu kama hicho kabla ya kuanza kunihuzunsha kwamba hata makato ya PPF hawajapeleka toka mwezi wa tano.....

  Swali linakuja hivi PPF mnalijua hili? Na kama kweli kama ilivyosemwa kuna hatua gani zaidi zinafanyika kuhakikisha malipo ya kila mfanyakazi yanawafakia katika muda unaotakiwa...iweje kampuni ya mohamed entrp..ikae mwezi mmoja bila kulipa muwafikishe mahakamani na kuwaachiia viongozi wa atcl wakicheza na maisha ya watu...je hamjui hivi sasa wafanyakazi ikatokea wakaomba kustaafu hamuoni usumbufu mtakaoanza kumfanyia mfanyakazi huyu aliekaa kwenye kampuni zaidi ya miaka 25....

  JE na hao wafanyakazi wanampango gani kuhakikisha pesa zao zinazokatwa zinalipwa sehemu husika?

  Hakuna sheria yoyote inaowafikisha hawa viongozi mahakamani na kama ipo JF tunaitaji kuwakomboa watu kama hawa, haiwezekani mtu anajua PPF yake haijalipwa toka mwezi wa tano mwaka jana na akakaa kimya lazima kuna kitu hapa katikati...

  Serikali kabla ya kuamua kupunguza kazi wafanyakazi wa ATCL mkawasaidia kwanza kuwalipia malimbikizo yao ambayo menejimenti ya atcl iliamua kuzichukua pesa zao bila taarifa na kushindwa kuzifikisha panapoitajika..kuliko kuwapunguza na kuanza kuwapa usumbufu wakati wa kudai haki yao

  Kwa hao wafanyakazi mnaojipanga kwenda mahakamani hakikisheni mnampata wakili anaejua sheria za kazi aweze kuwasaidia ...kwa hili halina tofauti na kuwaibia wafanyakazi.....

  Mh NYANGANYI....kweli unawezaje kuongoza viongozi wanamna hii wanaoamua kutumia hadi pesa za wafanyakazi pasipokujua...huoni kuna umuhimu wa kuwawajibisha wahusika haraka iwezekanavyo....

  Nawatakia mafanikio mema ,na kutoa ushauri muwe makini huko muendako.......turufu mahakamani imeamua kutawala utu wa watu
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  nilishawahi kusema siotozungumzia tena atcl mpaka serikali wairekebishe lakini kuna uitaji wa msaada mkubwa kuweza kuiikisha atcl inapotakiwa...bado safari ni ndefu..nilijua waziri aliwapa bodi siku saba itatoa mwanya wa kujua amuadhibu nani matokeo yake kuwaongezea watu ulaji usiokuwa na maana..mangapi yameandikwa hapa wameshindwa kufwatilia mwaka sasa......tunaitaji serikali ya aina gani kuamiini viongoi waliowateua ni wezi na majambazi??

  Nilishawahi kushauri hawa watu(management yote) ni ya kusekwa keko fasta baada ya kujiuzulu..matokeo yake hata kujiuzulu wamekataa na nasikia wameamua na kuapa kufa mpaka mwisho...

  solituion hapa baada ya kufikishwa mahakamani na precission
  wafanyakazi mnatakiwa kuja nyuma yao na kesi ya kuibiwa pesa zenu pasipokujua.....baada ya hapo kuna mnaandamaana rasmi kutoiitaji management na bodi yake.....huu ni wakati wa vitendo kaka zangu mlioko tanzania msipowafukuza watu kama hawa mtatufanya kuendelea kungangani mabox huuku mpaka vifo vyetu
   
Loading...