Precisionair Yakatiza safari baada ya kuruka dakika 10

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Ndege ya Precisionair iliyokuwa inaruka kutoka Kilimanjaro kuelekea Dar es salaam saa moja na nusu asubuhi leo, imelazimika kurudi KIA baada ya kuruka dakika 10, kwasababu za kiufundi ambapo matairi yalikataa kuingia ndani kama inavyotarajiwa.
Hivi sasa abiria wanasubiri itengenezwe!
 
Ninampa hongera na big up huyo rubani, siyo hawa WAHINDI wazembe wa shirika la reli waliosababisha ndugu zetu kufa.
 
Ndege ya Precisionair iliyokuwa inaruka kutoka Kilimanjaro kuelekea Dar es salaam saa moja na nusu asubuhi leo, imelazimika kurudi KIA baada ya kuruka dakika 10, kwasababu za kiufundi ambapo matairi yalikataa kuingia ndani kama inavyotarajiwa.
Hivi sasa abiria wanasubiri itengenezwe!

Duh! Bora yamekataa kuingia ndani kuliko yangekataa kutoka nje wakati wa kutua!
 
Imekuwa kawaida ya Precisionair siku hizi hasa kuhusu ndege zao za ATR -- hutokea hitilafu zinapokuwa angani. tarehe 16 Machi mwaka huu ilikuwa ni hivyo hivyo kwa abiria kutoka Dar kwenda Taboroa. Iliurudi dakika chache baada ya kuruka.
 
THIS IS UKWELI KABISA, tukio hili lilitokea pia Tarehe 13 iligeuzia dodoma, tahere 15 singida zote march na ilirudi Dar. sina uhakika na 16 march.

CHA KUSIKITISHA NI KUWA, Ilipogoma tarehe 15 walibadirisha ndege, rubani alipotua Shinyanga akagoma kuwa amechoka, leseni yake haimrehusu kutembea usiku, abiria wa Shy walibebwa mzobe mzobe mpaka Tabora bila kuambiwa kuwa wataenda kulala, kufika tabora walitelemshwa na wafanyakazi bila customer care yoyote utafikiri daladala, baada ya majibizano maeengi walipelekwa kiulala Tabora hoptel mpaka safari ilipowadia kesho yake asubuhi.

MIMI NILIKUWA MMOJA WA ABIRIA SO SIO HABARI ZA KUAMBIWA NA MTU.

kwakweli hii ni HATARI sana, kuna siku itaondoka DAR ifike DOM ilete matatizo rubani akiamua kurudi DAR safari inaweza kuishia kweny HEKALU LA CHALINZE.

TCCA FANYENI KAZI YENU NA ABIRIA CHUNGA MOYO WAKO.
 
Imekuwa kawaida ya Precisionair siku hizi hasa kuhusu ndege zao za ATR -- hutokea hitilafu zinapokuwa angani. tarehe 16 Machi mwaka huu ilikuwa ni hivyo hivyo kwa abiria kutoka Dar kwenda Taboroa. Iliurudi dakika chache baada ya kuruka.

Asante kwa hizi taarifa, nategemea kuitumia huduma yao mwishoni mwa wiki kwani nishanunua ticket, je kuna ndege mbadala toka Dar kwenda Kia?? wadau nihabarisheni.
Pia Naomba kujua ni ATR zote zenye matatizo hayo?? au mara zote zimekuwa zikihusisha ndege hiyo hiyo??na je wana ndege gani nyingine?
 
Nimesikia ni ATR moja namba 5H - PAA, wanayo Boeing ya kukodi mara nyingi ndio inaenda KIA na Mwanza, alternative ni Any Time Cancellation (ATC) hatuna pa kuponea.
 
Poleni...sana wasafiri.hope mafundi watarekebisha soon na safari itakuwa nzurii.....
 
Ndege ya Precisionair iliyokuwa inaruka kutoka Kilimanjaro kuelekea Dar es salaam saa moja na nusu asubuhi leo, imelazimika kurudi KIA baada ya kuruka dakika 10, kwasababu za kiufundi ambapo matairi yalikataa kuingia ndani kama inavyotarajiwa.
Hivi sasa abiria wanasubiri itengenezwe!

Thanks WoS;

I mekuwa kawaida kwa PW, ila tukumbuke dalili ya mvua ni mawingu wajameni... na kwa precision haya sio mawingu zimeanza kuwa kama radi sasa

Mwaka wa tabu huu...
 
Mungu amaewanusuru abiria na kifo? Inabidi ifanyiwe matengenezo y akina ili isilete maafa kama ya treni.
 
Sasa naona inakuwa habari za kawaida kwa hizi ATR, pengine ndo ileile ilyogoma mwaka jana wakati inatoka Tabora kuja Dar. Iliruka karibu dk 20-30 yalipogoma ikaturidisha na kutulaza tabora-customer care??? majibu yametolewa hapo juu. Sasa swali- Tabora walisema uwanja una vumbi ndo maana imepelekea "system" husika ishindwe kufanya kazi, je KIA nako kuna vumbi? maana sijatia timu KIA siku nyingi!!!! Kama hakuna vumbi; basi lazima mamlaka husika iingilie kati , maana unakuwa mchezo wa kawaida sasa-na matokeo yake anybody can guess!
 
Hizi ndege inabidi zifanyiwe matengenezo makubwa, ama sivyo zitaleta maafa. Nilipanda ndege yao mwezi wa 11 mwaka jana kuelekea Mtwara, wakati tunaelekea kwa ndege tuliona tairi moja limebonyea, basi tukawa tunaulizana, kila mtu akatoa jibu lake hapo. Tulipotua Mtwara wakati ndege inakata kona tukaona moshi mzito nje, yani hatukujua nini kinaendelea bali kila mtu alimkumbuka Mungu wake. Tulipotoka tukakuta ni lile tairi ndio lilitaka kuwaka moto.

Watu waliokuja kupokea ndugu zao ndio walikuwa na wakati mgumu, manake waliona toka mwanzo tairi lilipoanza kutoa huo moshi.
 
Mfumwa

Kwa kweli zinahitajika zifanyiwe matengenezo makubwa, mwaka jana nilitumia moja wapo ya ndege za Precision kuelekea kwenye jimbo langu la uchaguzi (Mwanza)....ndege ilkuwa na joto mle ndani utazani upo kwenye tanuru, nilikuwa na mtoto wangu wa kike akaniambia baba kwanini tusifungue madirisha....wahudumu walituambia nitatizo dogo kwenye mfumo wa hewa sijui kitu gani....hizi ni rasha rasha tusisubiri sunami!
 
Msipate shaka, haya ni matatizo madogo hasa yanayosababishwa na harakati zetu za kujipanga jinsi ya kugawana kasungura ketu. Ukitilia maanani kuwa uchumi unapaa ATC itakuwa na ndege za kumwaga kuhakikisha kuwa wilaya zote zinafikiwa na usafiri wa ndege. Ahadi yetu ipo pale pale MAISHA BORA kwa kila Mtanzania, kwa kasi mpya nguvu mpya na ari mpya. Sawa wananchi? "Itikieni ndio mzee".

Mungu atuepushe na majanga haya!
 
"THIS IS UKWELI KABISA, tukio hili lilitokea pia Tarehe 13 iligeuzia dodoma, tahere 15 singida zote march na ilirudi Dar. sina uhakika na 16 march......"

*********************

Kandambilimbili: Kunradhi, ilikuwa Machi 15 na siyo 16. Alikuwamo dada yangu akienda Tabora.
 
THE LEGEND IS BACK......!..!
just like "THE UNDERTAKER"
in wrestling..... ATC ON STAGE wengine hukimbia KWANI ANATISHIA AMANI YAO.....(joke)
THAT IS THE ATC FEAR....!
 
Wana JF,

Suala la ndege za PW na hasa hiyo ndege yao ya ATR (Sijui ni product ya nchi gani) soon or later itakuja kuleta maafa. Kwa hii ya leo tushukuru pilot alikuwa na busara akarudi kutua. Sikumbuki ilikuwa tarehe ngapi lakini na mimi niliitumia hiyo ndege kutoka Arusha kuja Dar Es Salaam kupitia Zanzibar. Tulipofika Zanzibar tuliambiwa abiria tunaoelekea Dar tusishuke lakini ndege ilizimwa. Tulikaa pale karibu dakika 30 lakini mle ndani kulikuwa na joto la ajabu. Niliomba kushuka ili nipate hewa kidogo nje mhudumu akajaribu kunizuia nisitoke. Nasikitika nililazimika kutumia nguvu ili kutoka nje kupata upepo lakini watu walikuwa wanatoa jasho kama mvua mle ndani.

Kwa nini hawakuwasha Ac? Sijui kama ni tatizo la kiufundi au ni less customer care!!! Hawana mpinzani kwa hiyo wamefika mahala wanabweteka.

TCAA inabidi ifanye kazi hapa kuepusha maafa hapo baadae.

Tiba
 
Kosa la pilot ni nini? yeye kaona hatari na kurudisha ndege, sasa mlitaka nini? Watu wengine bwana unashindwa hata kuwaelewa!
 
Back
Top Bottom