joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
MY TAKE: Lazima baba wa familia ya EA ajulikane na heshima iwepo
____________
Shirika la Ndege la Precision Air limetangaza kusitisha kurejeshwa kwa safari zake za Nairobi nchini Kenya kutokana na uhitaji mdogo. Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema watatangaza ratiba mpya hivi karibuni
Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya gazeti la Business Daily kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Safari za Ndege (KCAA), Gilbert Kibe akisema kampuni ya Precision Air ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika licha ya sintofahamu iliyopo kati ya Tanzania na Kenya
Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA) imezuia mashirika manne ya ndege kutoka Kenya kutua nchini. Mashirika hayo ni Kenya Airways, AirKenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation