Precision Air versus FastJet, Nani zaidi

Lamchina

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
240
120
Jana ndege mpya kubwa aina ya AIR BUS imezinduliwa na kampuni ya Fast Jet yenye uwezo wa kubeba abiria 150-200.
Ni jambo zuri na la kusifiwa sana,sasa tatizo ni nauli kati ya makampuni hayo hapo juu. Precision wanatoza zaidi ya Tsh 350,000 safari ya kwenda Mwanza na Kurudi DAR, Wakati Fast JET ukiwahi kukata ticketi nauli ya kwenda na kurudi ni chini ya Tsh 100,000.
Fast Jet wamezindua safari yao jana na safari rasmi itaanza kesho tarehe 29/11/2012. Kwa tofauti hizo za nauli bishara itakuwaje kwa makampuni hayo? Fast Jet watamudu ushindani au watakuwa kama Community Air Line? Precision ataendelea kupata wateja kama kawaida? Nauli ya mabasi toka Mwz hadi Dar ni Tsh 80,000 kwa kwenda na kurudi na unafika saa nne usiku upande wao kibiashara itakuwaje?

Karibuni wadau tuchanganue changamoto katika technologia ya ya Air Line!
:plane:
 
Fast Jet ndo mkombozi wa mtanzania. Nimenyanyasika sana na hawa Precisionair kwa jinsi usafiri wao ualivyokuwa ghali eti kwa kisingizio kwamba serikali hutoza kodi kubwa ndoo maana ticket zao ni ghali! Kwa mfano, leo hii rafiki yangu anaenda Dar leo jioni kutoka KIA, wamemcharge Shilingi laki tatu (350,000/-) ONE WAY!!! Kwa Fast Jet ni Shs. 59,000/- ONE WAY! hii ni pamoja na kodi zote! NATANGAZA KIFO CHA PRECISIONAIR RASMI KUANZIA LEO!
 
FastJet inaleta changamoto kubwa kwa Precision air na hii ni nzuri lakini ni hatari sana kwa usafiri wa anga Tanzania kwa sababu FastJet hawawezi kwenda routes nyinginezo ukiacha ya Dar-Mwz na Dar-KIA. Dege lao kubwa vile kwanza haliwezi kutua mfano Mtwara na hakuna abiria wa kutosha kwenda kwenye destinations nyingine zaidi ya Mwz na KIA. Sasa kama Precision air ikifa hii fastjet itaweza kutoa huduma mikoa mingi kama precision wafanyavyo kwa sasa? kwa maneno hayo nisingependa Precision air ife!!

Precision air wajifunze kwamba competition is stiff and many more new entrants in the market are there to come. Waboreshe huduma ili abiria wasiwakimbie. Kuna watu kulipa laki 4 sio tatizo kwao bora tu huduma iwe nzuri. All in all competition in the service industry is a good thing. So Viva FastJet
 
Mimi ni mmoja kati ya watu ambao wana support sana competition kwenye kila kitu. Precision Air wanacharge bei kubwa kwa safari zao, na hii inachangiwa sana na kukosekana kwa mbadala katika sekta ya usafiri wa anga.

ujio wa Fastje (Low cost flights models) si tu utaleta ushindani kwa safari za ndani za anga bali hata kwenye usafiri wa barabarani. Wamiliki na waendeshaji wa mabasi katika route ambazo Fastjet wanahudumu itawalazimu kujipanga upya na kuongeza ufanisi katika kuendesha shughuli zao ikiwemo kutambua thamani ya wateja.

Angalizo muhimu kwa Fastjet ni kuwa makini sana na "fitna za kibiashara" ambazo Precision Air wataanza kuzifanya. Kumbuka fitna walizofanyiwa Community Airline pamoja na ATC. Kuna watu serikalini wananufaika na monopoly ya Precision Air na wako tayari kufanya chochote ili Fastjet washindwe ku operate katika soko la Tanzania. Hii inadhihirishwa pia na statement iliyotolewa na msemaji wa Fastjet UK ambaye alinukuliwa akilalamikia urasimu walioupata/wanaoendelea kuupata katika ku secure necessary documents ili kuweza ku serve miji yote ya Africa Mashariki.

Otherwise...All the best to Fastjet!
 
Jana ndege mpya kubwa aina ya AIR BUS imezinduliwa na kampuni ya Fast Jet yenye uwezo wa kubeba abiria 150-200.
Ni jambo zuri na la kusifiwa sana,sasa tatizo ni nauli kati ya makampuni hayo hapo juu. Precision wanatoza zaidi ya Tsh 350,000 safari ya kwenda Mwanza na Kurudi DAR, Wakati Fast JET ukiwahi kukata ticketi nauli ya kwenda na kurudi ni chini ya Tsh 100,000.
Fast Jet wamezindua safari yao jana na safari rasmi itaanza kesho tarehe 29/11/2012. Kwa tofauti hizo za nauli bishara itakuwaje kwa makampuni hayo? Fast Jet watamudu ushindani au watakuwa kama Community Air Line? Precision ataendelea kupata wateja kama kawaida? Nauli ya mabasi toka Mwz hadi Dar ni Tsh 80,000 kwa kwenda na kurudi na unafika saa nne usiku upande wao kibiashara itakuwaje?

Karibuni wadau tuchanganue changamoto katika technologia ya ya Air Line!
:plane:

Fahari wawili wakigombana ziumiazo ni nyika!! in this case atakayefaidi ni mlaji as it has happened with mobile phone companies. competition is healthy and good for the consumer. karibu fastjet
 
Ili kuwasaidia kupunguza gharama za uendeshaji, serikali iondoe kodi kwenye mafuta ya ndege kwa kampuni za ndege za ndani.
 
Macho yangu yote ni kwenye uzi huu, nipo kama Tomaso wa kwenye biblia mpaka abiria atakayesafiri na hawa jamaa wa 'nauli mpya' aje atoe ushuhuda!

Leo muda wa saa 8: 10 asubuhi nimepita kwenye ofisi zao barabara ya Kenyatta hapa Mwanza nimewaona watu wengi wakisubiri huduma sijuhi ni wateja au?
 
Hivi mnaamini kabisa nauli yaweza kuwa 32,000/-?
Mimi yangu macho, nasubiri kusoma hapa comments zenu za kulaumu na kulaani!
Precissionair FOREVER! Mimi ni abiria tu msininange tafadhali!
tatizo wengi wetu tunadhani nauli ndicho kigezo pekee lakini tunasahau kuwa hata mabasi mengine yanatoza 35,000 Dar - Mz lakini yanayotoza 70,000 yanajaa haraka kabla ya hayo!
Ingelikuwa kuwa kila kampuni ya ndege inajenga uwanja wake hapo ingelikuwa sawa lakini ukijumulisha gharama za mamalaka ya viwanja vya ndege, Sumatra, sijui Ewura, Wizara, TRA, nk, nk, nk, nk .....then ukaongeza na 10% ya waziri 'muidhinisha mkataba', haraka haraka laki inapita. Sasa hapo ongeza na mafuta, unifomu za wafanyakazi (kumbuka ATC ziligharimu 80m), kurudisha mikopo, na mark-up ya kukaa kwenye kiti kirefu wakati wa machweo vs 32,000/-.
Nami ngoja nisubiri comments maana hapa jf kuna hata za mwaka 2006
 
Inanikumbusha EasyJet na Ryanair huko kwenye nchi za wenzetu, haya ndio mapinduzi ya anga yanayotakiwa

Mimi ni mpandaji mzuri sana wa Ryanair na kwa kweli inasaidia sana kwa vile mara nyingi bei zake ni chini kuliko ndege zingine. Hata hivyo ili kupata bei hizo rahisi unatakiwa ku book mapema sana, kuepuka peak seasons au week ends. Vilevile huwezi kuchukua mzigo mzito, hakuna huduma yeyote ya bure ndani ya ndege, kila kitu unatakiwa ununue hadi maji. Hata hivyo ukiweza kuvumilia hayo ni rahisi sana.
 
Hivi mnaamini kabisa nauli yaweza kuwa 32,000/-?
Mimi yangu macho, nasubiri kusoma hapa comments zenu za kulaumu na kulaani!
Precissionair FOREVER! Mimi ni abiria tu msininange tafadhali!

Mkuu, ni kwetu(nchi zetu) tu, mambo yanakuwa magumu namna hii.Sehemu nyingine Province to Province/State to State flight ni cheap,..na ndiyo usafiri unaotumika kuliko hata mabasi, so YES, that fare ipo ila payment/charging fee ya mizigo ndiyo huwa kubwa.

Precision, ilikuwa nzuri hadi pale walipoanza kutunyanyasa kwa delay na kuahirisha kwa safari ambako kulikuwa hakuna sababu.
 
Ilimradi mafisadi wasiamue kuifisad fastjet basi wengi tutaendelea kjufurahia huduma za fastjet. Natumai Precisionair watajipanga upya on regional flights. Natamani fastjet walete videge vidogo vya kwenda mbeya BK etc. Baya kwa ujio wa fastjet nio kwamba air Tanznaia ndo haifufuki tena.
 
Jana ndege mpya kubwa aina ya AIR BUS imezinduliwa na kampuni ya Fast Jet yenye uwezo wa kubeba abiria 150-200.
Ni jambo zuri na la kusifiwa sana,sasa tatizo ni nauli kati ya makampuni hayo hapo juu. Precision wanatoza zaidi ya Tsh 350,000 safari ya kwenda Mwanza na Kurudi DAR, Wakati Fast JET ukiwahi kukata ticketi nauli ya kwenda na kurudi ni chini ya Tsh 100,000.
Fast Jet wamezindua safari yao jana na safari rasmi itaanza kesho tarehe 29/11/2012. Kwa tofauti hizo za nauli bishara itakuwaje kwa makampuni hayo? Fast Jet watamudu ushindani au watakuwa kama Community Air Line? Precision ataendelea kupata wateja kama kawaida? Nauli ya mabasi toka Mwz hadi Dar ni Tsh 80,000 kwa kwenda na kurudi na unafika saa nne usiku upande wao kibiashara itakuwaje?

Karibuni wadau tuchanganue changamoto katika technologia ya ya Air Line!
:plane:

Fair Competition Commission wanatakiwa watupe jibu kama ni halali kutoza chini ya kiwango cha matumizi (below cost) ili kuua ushindani......sidhani kama inakubalika Lamchina
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuoperate airbus kwa nauli ya 32k kwenda Mwanza!!!

I guess hiyo 32k ni offer ya ticket chache lets say 10% ya tickets for every flight, Marketing strategy
 
Mimi ni mpandaji mzuri sana wa Ryanair na kwa kweli inasaidia sana kwa vile mara nyingi bei zake ni chini kuliko ndege zingine. Hata hivyo ili kupata bei hizo rahisi unatakiwa ku book mapema sana, kuepuka peak seasons au week ends. Vilevile huwezi kuchukua mzigo mzito, hakuna huduma yeyote ya bure ndani ya ndege, kila kitu unatakiwa ununue hadi maji. Hata hivyo ukiweza kuvumilia hayo ni rahisi sana.
Kwa safari fupi kama za hapa kwetu inawezekana. Mtu anatoka home kashiba...ananunua maji tu safari nzima lol!
 
Huwezi kuoperate airbus kwa nauli ya 32k kwenda Mwanza!!!

I guess hiyo 32k ni offer ya ticket chache lets say 10% ya tickets for every flight, Marketing strategy
Haya ni maoni yako au ukweli wenyewe? Kama ndio ukweli weka basi data!
 
Ili kuwasaidia kupunguza gharama za uendeshaji, serikali iondoe kodi kwenye mafuta ya ndege kwa kampuni za ndege za ndani.

Kiuchumi, serikali makini haiwezi kufanya hivyo. Wanaopanda ndege ni asilimia ndogo sana ya watanzania. Kodi inayokusanywa kwenye mafuta ya ndege ikitumika vizuri inafaidisha watanzania wengi zaidi kuliko hawa wanaotumia usafiri wa ndege. Kuondoa kodi kwenye mafuta ya ndege ni sawa na kuondoa ziwa mdomoni mwa kichanga na kumpa baba yake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom