@Pasco
Nimewahi kuchelewa ndege uwanja wa Heathrow Uingereza nikiwa na ujumbe fulani na tulikuwa kama abiria 10 hivi kwa pamoja na tulijichanganya baada ya safari ndefu toka Miami na kubadili ndege pale London kuja Dar. Ilibidi BA itusubiri kwa zaidi ya nusu saa huku abiria wote wakiwa wameshaingia katika ndege na tulipoingia tulikuta wazungu wamenuna hadi wamekuwa wekundu lakini hatukujali maana cha muhimu ndege ilitusubiri ingawa sisi weusi.
Sometimes kusubiri abiria huwa ni kawaida kwa ndege zinazojua umuhimu wa wateja wao, usishangae hilo la KIA na Precision. Hilo la kwako wewe, hawakukutendea haki hata kidogo, walipaswa kukupa ruksa ku-check in walikuwa na muda wa kutosha.
Pole kwa yaliokukuta bwana pasco lakini kusubiri abiria ni jambo la kawaida kabisa, niliwahi kusubiriwa kwa dakika 49 na ethiopia airline addis airport nikiwa na unganisha safari yangu toka dar kuelekea london nilipotelemka kwenye ndege yangu nilipelekwa moja kwa moja kwenye ndege ilionisubiri ambapo niliingia ikafungwa mlango nakuondoka abiria wengi hawakuamini kabisa aliekuwa anasubiriwa ni mimi mtu wa kawaida tena nikiwa katika casual wear, kwa hiyo kusubiriwa kwenye ndege hakumaanishi anesubiliwa ni mtu wa cheo fulani au anajulikana la hasha kuna vigezo airline inaweza kutumia kumsubiri abiria kadri wanavyoona inafaa