Precision air mwanza airport staff wamekuwa wezi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision air mwanza airport staff wamekuwa wezi??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Askofu, Nov 4, 2009.

 1. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Wana JF,

  Heshima Mbele,

  Siku ya Ijumaa Tarehe 30 October, 2009 nikiwa Mwanza nilifanya Booking ya Ndege ya Precision Air kwa ajili ya kutoka Mwanza Tarehe 01 November, 2009 (Jumapili) asubuhi kuja Dar. Kwenye Ticket iliandikwa reporting time ni saa moja kamili asubuhi(07h00).

  Kama kawaida niliwahi mapema kutafuta samaki wa kuja nao Dar, nikanunua samaki wa size ya kati wapatao 33 nikawekewa kwenye ile ndoo kubwa ya lita 20, ndoo ikafungwa vizuri kama kawaida na kamba then nikaandika jina kwenye Name Tag.

  Nilipofika airport yapata saa 1 na dakika 45 hivi asubuhi (0745hrs), nikaanza kusubiri, kwenye list pale kwenye ubao wao wa ratiba za ndege palikuwa panaonyesha kuwa ndege ipo na inaondoka saa 2:35 asubuhi (0835hrs), na sikupata wasiwasi kwa sababu nikaona abiria wanazidi kumiminika.

  Ikafika saa 3 asubuhi, nikaona kimya. Imagine pale Mwanza airport hakuna sehemu ya kupumzika au kukaa, abiria wanasimama tu mpaka ndege itakapofika. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba ofisi za PW ziko ndani, ina maana mpaka uingie ndani ndio unaweza kuonana nao. Sio mimi tu niliekuwa nashangaa, tulikuwa wengi, ikabidi tuulize what was going on, tukaambiwa kuwa tusubiri ndege inakuja. Mara ikafika saa nne asubuhi. wakaitwa abiria wa Nairobi na Entebe lakini abiria wa Dar tukaambiwa tusubiri.

  Baadae ikabidi tulazimishe kukaguliwa mizigi ili tuingie ndani tukapumzike, maana pale nje tulisimama sana, wale walinzi wakakubali wakatukagua tukaingia ndani. Tulipofika pale ndipo tukapata the shock of the year... Kwamba flight was delayed mpaka saa moja jioni. Nikauliza kwa nini hawakutupatia taarifa za flight cancellation, wakasema walipiga simu lakini hatukupatikana.

  Nikataka kujua arrangement zilizopo wakati tunasubiri ndege saa moja usiku, nikaambia there was no any arrangement, kwa maana nyingine ni kwamba tutajiju. Wakasema kwamba kuna ndege inatoka Shinyanga itafika pale saa sita hivyo tunaweza kupata nafasi, tukajipa moyo kwamba saa sita sio mbali, ndege kweli ikafika saa sita lakini to our surprise ndege ikawa imejaa kiasi kwamba hata waliokuwa booked kwenye hiyo flight wakaachwa... Kama kawaida hao walioachwa nao wakaahidiwa kuwa kuna ndege nyingine inakuja na kuondoka saa nane, watu tukaendelea kusubiri, hapo ujue bado tumesimama hatujapatiwa boarding pass ili tuingie ndani kwenye waiting lounge tukae.... safari hii kikatokea kituko tofauti... wanadai mizigo imekuwa mingi kwa hiyo ndege haiwezi kuchukua abiria wote, hapo tena abiria wakaachwa.

  Sasa kilichokuja kunishangaza na kunisikitisha zaidi... ni kwamba baada ya ku-check in nikapewa boarding pass yapata saa tisa, nikaingia kwenye lounge kusubiri. Tukasubiri mpaka ndege ilipoingia hapo saa moja kasoro usiku, tukaondoka vizuri Mwanza ingawa safari hii sikujua abiria wangapi wameachwa tena. Ndege ilingiia Dar saa nne kasoro hivi, nikaenda kusuburia Samaki wangu niliowanunua tangu asubuhi nikiwa na matumaini madogo sana ya kukuta wakiwa fresh. I was shocked ndoo yangu ilipofika nikakuta ile kamba imekatwa na nilipofungua ndani nikakuta nusu ya samaki wamechukuliwa.

  Nikapata wasiwasi na mzigo wangu mwingine, nikaamua kukagua Begi langu... kwa kweli niliumia... nilikuta kufuli limevunjwa. Hapo yapata saa 4 na robo usiku.

  Sasa nikajiuliza, nikaripoti polisi? je, itanichukua muda gani mpaka niondoke kwenda nyumbani? maana kama wote tuwajuavyo wangesema kuwa hawana karatasi au wanakuchelewesha kwa makusudi tu. Na kitu kingine, wangeniambia niache mizigo yangu kama exhibit (kidhibitisho). Sasa imagine, nimeamka saa kumi na mbili asubuhi niwahi vizuri Airport, nikanunua samaki kabla ya saa mbili asubuhi, nikasimama airport kwa zaidi ya saa 8, halafu bado mizigo yangu ikaibwa na sasa yapata saa nne na nusu usiku wa Jumapili, naishi Boko. I might be stupid, lakini niliamua kuacha... Mungu anajua.

  Lakini kama hii tabia itaendelea, sijui itakuwaje. Siku moja Kaka yangu aliniletea samaki kutoka Kwanza kamba ikiwa imekatwa na samaki wako nusu, nikafikiri amemgawia mtu, nilipomuuliza akasema samaki wamechukuliwa na Airport Staff pale Mwanza. Nimeshasikia cases kama 3 hivi, lakini sikutegemea kama sasa wanavunja na mabegi.

  Wana JF, next time you travel from Mwanza, especially with Precision Air... Don't check in your valuables, zitapotea.

  With all due respect
  Nawasilisha
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pole sana Ndugu! Sasa kwa utaratibu huu ambao umenza 1st November ya kufanya handling wenyewe na kuanza wizi wa aina hii si itakuwa taabu! Maana ingekuwa swissport ndo wanafanya handling Tusingewalaumu precision Air na Tungewalaumu Swissport
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Askofu uyasemayo ni kweli mie nikirudi kwenye swala zima la time huwa naboreka vya kutosha ,pili sehemu ya mapumziko ukiwa unasubiri ni issue ,
  Hilo swala la wizi wa samaki nalo ndo linatia fola
   
 4. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  1st Lady, nafikiri mtu anapopanga safari yake anakuwa anajua sababu, either anawahi au anashughuli za kufanya. Sa hawa ndugu wana cancel flight halafu kwanza hawatoi ripoti, then kama kulikuwa na ndege ya saa 6 na saa 8 kwa nini at least wasituweke kwenye hizo?

  Yaani mi nilisikitika.... Kilichoniuma ni samaki wangu. Next time nitawawekea sumu... tatizo wanakusanya hivyo wanajaza kwenye ndoo halafu wanauzia mtu tena, hivyo unaweza kudhuru innocent souls
   
 5. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Asante sana!!

  Kwa utaratibu huu.... KWISHNEI... wataiba hadi gagulo
   
 6. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mimi najua usafiri wa ndege sana mwanza to dar,dar to mwanza ni vichekecho sana hakuna la kuchangaa hata kidogo....tena wanapoharisha safari hakuna hata mtu mmoja unaweza kujua.je number ya simu unaacha ya nini ofisini...kwao.wabumbavu kuannzia uongozi wao wa juu mpaka watunza mizogo....ni ng'ombe kabisa wanapotezea watu muda wao na mali zao.
   
 7. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kuna msichana mmoja anasema ananipenda sana.....lakini naona kama vitendo vichache vya kunipenda....je ukitakujua mwanamke anakupenda utajuaje?
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,660
  Likes Received: 21,879
  Trophy Points: 280
  Umepotea njia?
   
Loading...