Precision Air huu ni wizi wa wazi wazi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision Air huu ni wizi wa wazi wazi..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Manyanza, May 10, 2012.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wakuu mwaka jana mwezi wa tisa niliamua kunua share za kampuni ya ndege ya Precision...
  nilinunua share 3000 kwa bei ya sh 475 kwa kila share..
  nimemua kuziuza baada ya kuona hazifanyi vizuri katika soko la Hisa la Dar es Salaam.. maana mpaka leo ni sh 480 kwa hisa hii ni toka mwezi wa 12 mpaka leo ina maana imeongezeka sh 5 kwa kila hisa
  nimepigwa na butwaa baada ya kuenda kwa moja ya partners wa DSE, nimefika pale nikaambiwa kama unataka kuuza Hisa zako kuna charges zao ambazo hua wana kata, wamenipigia mahesabu ikawa kama hivi...

  3000x1.02x480=1,468,800

  means
  total share=3000
  charges=1.02
  price per share=480

  NIMEJARIBU KUULIZA HIYO 1.02 INATOKA WAPI, SIJAPATA JIBU LA KURIDHISHA ZAIDI YA BLA BLA

  wakachukua na ile gharama niliyonunulia share yaani 3000x475=1,425,000

  wakatoa na hiyo Total hapo juu ili kupata charge zao, yaani 1,468,800-1,425,000=43,800

  Ina maana hiyo 43,800 ndio cost charges zao( hii cost charge wamenikata katika pesa yangu)

  HUU NI WIZI NA HAKUNA FAIDA YOYOTE NILIYOPATA NA BADO WAMENIKATA KIASI KIKUBWA CHA PESA

  So kwa muda wote huo mimi sijapata chochote kwa sababu nikichukua gharama niliyonunulia share nikitoa cost charges zao nakua nimepata hasara ya Tsh 43,800, na wameniambia zitachukua muda mrefu karibu mwezi mmoja ili ziweze kuuzwa kwenye soko maana zipo nyingi sana SHARE ZA PRECISION KWENYE SOKO KUU LA HISA DSE
   
 2. B

  BARRY JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  hiyo ni kawaida tu, lazima ulipe a cetain percent nakumbuka kama 2%. Tatizo ni kuwa shares za precision hazilipi!
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeshangaa sana kutoka mwaka jana mpaka leo, ongezeko ni sh 5 kwa kila hisa, kweli hakuna issue
   
Loading...