PRE SEASON 2019, Friendly Match: Simba SC yatoka sare na Orlando Pirates ya Afrika Kusini

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Klabu ya Simba SC ambao ni Mabingwa wa Tanzania, katika mwendelezo wao wa kujiandaa na msimu mpya wa TPL, 2019/2020 na michuano ya Kimataifa, pamoja na kuwapa burudani ya kweli kwa Wanasimba wote, na katika kuelekea tamasha la Simba Week, leo Julai 30 2019, walisafiri kutoka mjini Rustenburg kuelekea Johannesburg kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 ambapo Simba SC, ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Clatous Chota Chama 'Triple C' kunako dakika ya 33' Kabla Orlando Pirates hawajasawazisha dakika ya 40' kabla ya mapumziko kupitia kwa Mulenga.

IMG_20190730_184232_559.jpeg
IMG_20190730_184210_489.jpeg
 
Yes..! Unacheza na timu ambazo zipo CAFCL..Halafu gongowazi utasikia Simba anabebwa mara ooh TFF, kama unacheza na timu ya Kanisa na watoto wa shule, kweli utakuja kupambana na Mnyama Mkali?
Kipimo kizuri, sio matikiti wanajipima na ligi za mchangani
 
Back
Top Bottom