Pre - Corruption ndiyo inatawala dunia

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
JF Members Salam kwenu nyote:

Mada yangu kama kichwa cha habari kinavyosema, kuna ukweli mkubwa ndani yake na watekelezaji wa hili ni wapiganaji wenyewe. Wengi wao wametenda hayo bila kujua kama ni kosa.

'Pre' maana yake kabla ya. Hii ni tafsiri rahisi.

Pre - Corruption ni maandalizi ya aidha mtoaji rushwa kwa mpokeaji ambapo yawezekana mpokeaji anafahamu au hafahamu juu ya hilo.

Pre - Curruption ipo kiungwana sana kwani mtoaji wa aina hii ya rushwa anaweza akaushawishi umma wote mkajua ni kawaida kumbe ndiyo rushwa yenyewe.

Ahadi zisizotekelezeka, unatoa ahadi ambazo unajua haziwezekani kutekelezwa, utamweka mtu madarakani kwa mfano kwa ahadi kuwa tukimchagua atatujengea daraja hewani toka Tanzania Bara hadi Zanzibar nasi kwa uchu wa mabadiliko hayo tukaona anatufaa, lakini baada ya kuchaguliwa kwake mkaona hata kukumbushwa juu ya ahadi zake hapendi.

Ukiona una kiongozi wa namna hiyo ujue amepata madaraka kwa mtindo huu.

Kumbuka Pre - Curruption ni ahadi hewa. Ukimuahidi mwanao kuwa akifaulu vizuri utampa zawadi mfano utampa computer set, halafu mtoto akafanya vizuri wewe kama mzazi usifanye kama ilivyoahidi hiyo sio Pre - Corruption kwani jambo alilofanya ni kumhimiza yeye mwenyewe kwa manufaa yake. Hii Pre - Corruption ni kwa hawa wanasiasa wetu.

Inatubidi tuwe makini na wale wanaotoa ahadi hewa. Hadi sasa tunayo maendeleo katika nchi yetu ambayo yameathirika yakasimamiwa na yakatekelezeka, lakini pia wapo hadi sasa wanaobuni namna watakavyo kuja kutuhadaa katika kampeni mwaka 2020 TUWASIKILIZE NA TUCHUKUE HATUA.
 
Back
Top Bottom