Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kuna kanuni moja muhimu sana katika sayansi ambayo leo tungependa kuichambua kwa kina na kueleza jinsi inavyoathiri siasa za Tanzania na kusababisha jamii yote kwa ujumla kupoteza mueleko ikiwemo wengi miongoni mwa wanaosoma mada hii.
Kupitia uchambuzi wa huu, tutajibu kwanini kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida yanatokea kila mahali ikiwemo humu JF na kutoa suluhu na kueleza nini kitatokea ikiwa tutaendelea kufanya tufanyavyo.
Nazungumzia kanuni inayojukikana kama “the law of use and disuse”. Kanuni hii inasema kwamba, “Whenever you use, it grows and whenever you don’t use you loose” Yaani “Kwa kadiri unavyotumia kitu ndivyo kinavyokuwa kwa kadiri usivyokitumia kinapotea".
Siasa za demokrasia; msingi wake mkuu ni hoja kwa hoja. Yaani, badala ya watu kutukanana wanatoa hoja. Ushawishi; yaani badala ya watu kupigana na kukabana wanajenga ushawishi. Mijadala; yaani badala ya watu kulazimishana au kudhalilishana wanajadiliana.
Hii ni tofauti na mifumo mingine yote ya siasa ambayo misingi yake ni nguvu, hila, uhuni, dhuluma, ulaghai, uongo au vyote kwa pamoja.
Kwa bahati mbaya tunadai sisi ni wana demokrasia ila tumeachana na misingi hiyo hapo juu. Inapotakiwa kutoa hoja tunaongea ujinga, matusi, mizaha, ushabiki na kudhalilishana. Inapohitajika kutumia akili kufikiri tunatumia maguvu.
Sasa tukirudi kwenye kanuni yetu na kuingunganisha na tatizo linalotukabili; Kama tungeendelea na kufanya mijadala ya hoja kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na tukaendelea kuwekeza kwenye eneo hilo, maana yake tungejijengea uwezo zaidi wa kujenga hoja.
Kwa kuwa kujenga hoja kunahitaji kutumia akili; tungejijengea zaidi uwezo wa kufikiri.Kwa kadiri ambavyo tungekuwa tunajijengea Zaidi uwezo wa kufikiri ndivyo ambavyo tungezidi kujijengea uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabili kwa busara.
Tungekuwa tunaendelea kufanya siasa za ushawishi, tungejijengea uwezo Zaidi wa kushawishi na hivyo tungekuwa na siasa za hoja na ushawishi zaidi kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hiyo ingekuwa ni faida kwa watu wote.
Kwa bahati mbaya tumechagua kinyume chake. Hakuna mtu ambaye amewahi kutoa sababu ya msingi kwamba kwa nini tumeamua kuchagua kinyume chake.
Ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba kuna watu wachache wanaojua kuwa tufanyacho si sahihi na wanachukua hatua, kuna wengi wanaojua tufanyacho si sahihi ila hawachukui hatua, kuna wanaojua ila wanaendelea kwenda kwenye muelekeo usio sahihi huku wakishangaa matokeo.
Kwa kuwa tumechagua kuwa panapohitaji hoja, basi tunaongea ujinga; kwa mujibu wa kanuni yetu hapo juu, tunajikuta tunajijengea uwezo zaidi wa kufikiri na kuongea ujinga.
Kwa kuwa panapohitaji kutumia akili tunatumia msuli; basi tunajijengea nguvu ya msuli badala ya fikra (madhara yake kwa mapana tutayaeleza baadae). Tunapotakiwa kuongea mambo ya msingi tunafanya ushabiki, kwa hiyo tunaongeza uwezo wetu wa kushangilia.