Practical side of “The law of use and misuse” in Tanzanians politics

mkuu jd41 kuna mambo mengi ambayo yana changamoto nyingi na kubwa, ila ukweli ni kwamba hatuwezi kutatua mambo makubwa kabla ya kutatua mambo madogo kwanza

Kwa mfano kabla ya kwenda mbali sana, tujiulize tu kuwa sisi tuliopo jf kwa mfano, tunafanya nini, ili kutatua tatizo gani, wapi lini na kwa faida ya nani angalau kwa aina ya maoni tunayotoa tu?

unaweza kusema hilo ni jambo dogo sana, sawa; nakubali ni jambo dogo, lakini kama mtu anashindwa kuji behave kwenye jambo dogo, atawezaje kuji behave kwenye jambo kubwa? Kwa hiyo matatizo unayosema yapo ni kweli yapo, ila watu wanadai wanataka kutatua hayo makubwa wakati kuna vikitu vidogo vidogo tu ambavyo hawavifanyi na viko ndani ya uwezo wao na vina faida kwa mustakabali mzima wa siasa zetu.

Kwa mfano, mtu anaweza kuona kuna hoja nzuri, ambayo inasaidia kutatua tatizo Fulani (hata kama kwa asilimia ndogo) hachangii, akichangia anakuuliza mbona hunipi nafasi ya kuchangia, unamwambia haya changia, anakimbia, kesho yake unakuta analaumu hakuna demokrasia.
 
Mkuu kwa kiasi nakuelewa na kwa kiasi naomba kutofautiana na wewe.

Kuwa mwanachama wa chama fulani haimaanishi uamini au kutetea kitu ambacho wewe ndio ulipaswa kukisahihisha, ujinga, ushabiki, upuuzi na vitu kama hivyo. Kama maana ya vyama vya siasa kwa mtizamo wetu ni hiyo; basi hatuna haja ya kuwa na hivyo vyama kwa sababu viongozi wa nchi hutokana na viongozi wa vyama, viongozi wa vyama hutokana na wanachama, sasa kama wanachama ndio wanatakiwa kuwa hivyo then what is there?

Mimi mwenyewe nina chama na nafikiri wajibu wangu ni kukisaidia pamoja na kusaidia ustawi wa mwanadamu wa ajili ya manufaa ya wote, ndio maana nasema haya nisemayo. Sasa huyo anayesema chama chake ndicho kinachomsababisha awe mtu wa miujiza, tatizo si chama tatizo ni yeye.

Mara nyingi tumeeleza kuwa vyama sio vitu 'objective' ni 'abstract'. Kwa hiyo tunaposema vyama kimsingi tunazungumzia makundi ya watu na tunapozungumzia makundi ya watu tunazungumzia mtu mmoja mmoja na huyo mtu mmoja mmoja ni mimi na wewe na yeye.
Kama umenisoma vizuri nimezungumzia sababu inayofanya watu/ wapenzi wa vyama kuwa na mtazamo huo.

Hakuna fairness kwenye uwanja wa siasa, naamini kabisa kwamba, kama yote yanayowatatiza wapinzani ( nawatumia wao sababu naamini ndio wanaoona hawatendewi haki, upande wa CCM wao sidhani kama wana shida yoyote ukizingatia ndio wenye serikali) yangekuwa yanafanyiwa kazi na upande wa pili, basi pasingekuwa na hali hii unayoiona ya watu badala ya kujenga hoja kuishia kutukana, kukejeli n.k.

Kama hoja za upinzani zingekuwa zinafanyiwa kazi instantly, pasingekuwepo na hisia za chuki au hasira zinazosababisha matusi na kejeli, ila kwasababu hakuna lolote kati ya wanayolalamikia linalofanyiwa kazi, wanachoka, wanaona hakuna sababu kutumia akili nyingi kuuliza swali ambalo anaejibu anatoa jibu kivivu. Na hili hutokea mpaka bungeni.

Ukumbuke, wakati haya yote yakitokea, ndio pia viongozi wa vyama wanajikuta wamekuzwa katika hali hiyo, ya kutopewa majibu sahihi ya hoja zao, na pia wanachama na wapenzi wapya mitandaoni wanaona aina ya majibu wanayopewa toka upande wa pili, hivyo hii husababisha kutengeneza kizazi cha matusi, na kejeli.

Hivyo sasa, siku ambayo upande wa serikali utaamua kuwa serious kwenye kujibu concern za wapinzani, na wapinzani pia kujitahidi kuvumilia majibu ya karaha toka chama tawala, hili siku moja litasaidia kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la matusi na kejeli unalo li-address kwa sasa. Kwasababu mwisho wa siku sote ni watanzania, na wote tunataka hali nzuri kwa kila mwananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa kiasi nakuelewa na kwa kiasi naomba kutofautiana na wewe.

Kuwa mwanachama wa chama fulani haimaanishi uamini au kutetea kitu ambacho wewe ndio ulipaswa kukisahihisha, ujinga, ushabiki, upuuzi na vitu kama hivyo. Kama maana ya vyama vya siasa kwa mtizamo wetu ni hiyo; basi hatuna haja ya kuwa na hivyo vyama kwa sababu viongozi wa nchi hutokana na viongozi wa vyama, viongozi wa vyama hutokana na wanachama, sasa kama wanachama ndio wanatakiwa kuwa hivyo then what is there?

Mimi mwenyewe nina chama na nafikiri wajibu wangu ni kukisaidia pamoja na kusaidia ustawi wa mwanadamu wa ajili ya manufaa ya wote, ndio maana nasema haya nisemayo. Sasa huyo anayesema chama chake ndicho kinachomsababisha awe mtu wa miujiza, tatizo si chama tatizo ni yeye.

Mara nyingi tumeeleza kuwa vyama sio vitu 'objective' ni 'abstract'. Kwa hiyo tunaposema vyama kimsingi tunazungumzia makundi ya watu na tunapozungumzia makundi ya watu tunazungumzia mtu mmoja mmoja na huyo mtu mmoja mmoja ni mimi na wewe na yeye.
Hapa nakubaliana na wewe 100%.

Jamii itabidi ijifunze kukemea maovu, uongo, au upotoshaji hata unaofanywa na chama chako.

Kwa kufanya hivi, tutajenga picha kwa viongozi wa vyama vyetu kuogopa kunena uongo kwa kuwa watakuwa wanajua watakutana na upinzani kwanza, toka ndani ya vyama vyao, pili, toka nje ya vyama vyao.

Hii itasababisha kutengeneza kizazi cha kweli na haki, watu watakuwa tayari kupinga mabaya yanayotendwa na viongozi wa vyama vyao, na hili lita speed up maendeleo ya nchi, na kujenga jamii yenye kujali utu wa mtu, bila kutaka kujua anatokea chama gani, tofauti na ilivyo sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu jd41 mambo mengi nakuelewa vizuri tu na kwenye vipengele kadhaa nakubaliana na wewe.

sasa ningeomba hebu tutanue mjadala kidogo. Tuangalie kwenye picha pana Zaidi kidogo nje ya CCM na CHADEMA. Hiyo inaweza kutupa uwezo wa kuona mambo kwenye mwanga bora Zaidi.

Hivi hakuna mambo mengi tu ambayo yako nje ya hiyo ligi na yangepaswa kufanywa lakini hakuna anayefanya, na ukiuliza amma haujibiwi, au unashambuliwa vibaya mno, au unayemuuliza atafanya mbinu hadi asingizie tatizo ni mwenzake?

Je! Unawezaje kuzungumzia wanaohama hama vyama kila mara bila maelezo ya msingi na kuyakana yale wanayotetea accordingly? kwa hali hiyo ni nani anaaminika na kwa nini? au nani anapaswa kuaminiwa na kwa nini?

Hatuoni anayelalamika kuteswa leo inawezekana kakaa angle mbaya ndio maana analalamika ila akipata angle nzuri atafanya yale yale anayolalamikia?na kinyume chake, sasa hapo tunategemea katika upana wake baadae iwe nini na maswali mengine kama hayo.

Kwa maoni yangu tunapoangalia kila jambo katika level ya CCM na CHADEMA na tukaishia hapo tunakuwa tumejifungia kwenye kachumba kadogo sana halafu kaliko jaa mambo kiasi kwamba unaweza kukosa hewa. Ni muhimu kwanza kutanua duara.
 
Umeongea mambo ya msingi sana. Lakini sasa hii inaanza na mtu mmoja mmoja kwa sababu hakuna kitu kama 'chama' ambacho kiko pale. Tatizo sasa linakuja kila mtu anadhani sio yeye, bali wapo "watu"
 
Mkuu, nakushauri usishangae wala usisikitike. Tuungane tuibadili Tanzania. Ijapokuwa taratibu taratibu ila kwa uhakika Zaidi. Wa kuleta mabadiliko ya msingi ni mimi na wewe na mwingine na mwingine.

Mimi nilipita kipindi cha kushangaa, nikapita kipindi cha kusikitika, nikapita kipindi cha kulaumu, nikapita kipindi cha kukata tamaa, sasa niko kwenye kipindi cha kuchukua hatua. Nakushauri tuungane tuchukue hatua na kuwashawishi wengine wafanye the same.

Jamii yetu ishafika kwenye hatua mbaya sana na kibaya Zaidi haijijui kama inakabiliwa na tatizo la msingi na ndio maana unaona hali iko hivi. Kwa hiyo wala usishangae ni jambo linalotarajiwa.
Nakubaliana na wewe kabisa bwana Azizi Mussa . Nguli wa uandishi marehemu Shaaban Robert (RIP) kwenye kitabu chake cha Kusadikika ni mfano mzuri sana wa uliyoyaandika. Nchi ya Kusadikika ilikuwa imetumbukia kwenye utamaduni mbaya. Wasadikika wote walikuwa wameshakubaliana na hiyo hali na hakuna aliyeona umuhimu au uthubutu wa kukemea lolote. Akatokea shujaa mmoja kwa jina Karama. Akaamua kuvunjwa mwiko wa kulaumu, kulalamika na kukataa tamaa na kuamua kusema ukweli. Japo alikuwa peke yake lakini hakujali. Shaaban Robert anaelezea hivi juu ya watu wanaoamua kuchukua hatua wakati wengine wameshakata tamaa: ''Kama watu waliokusudiwa kuwa mwenge kwa wengine wangalikuwa wakingojea shangwe la watu kabla ya kuanzisha makusudi yao maendeleao katika maisha yangeliadimika. Kwa bahati njema, mtu yoyote katika hawa hutegemea mwongozo usiotaka shangwe mpaka amefaulu'' (Shaaban Robert, Kusadikika, ukurasa 7)
 
Kuna kanuni moja muhimu sana katika sayansi ambayo leo tungependa kuichambua kwa kina na kueleza jinsi inavyoathiri siasa za Tanzania na kusababisha jamii yote kwa ujumla kupoteza mueleko ikiwemo wengi miongoni mwa wanaosoma mada hii.

Kupitia uchambuzi wa huu, tutajibu kwanini kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida yanatokea kila mahali ikiwemo humu JF na kutoa suluhu na kueleza nini kitatokea ikiwa tutaendelea kufanya tufanyavyo.

Nazungumzia kanuni inayojukikana kama “the law of use and disuse”. Kanuni hii inasema kwamba, “Whenever you use, it grows and whenever you don’t use you loose” Yaani “Kwa kadiri unavyotumia kitu ndivyo kinavyokuwa kwa kadiri usivyokitumia kinapotea".

Siasa za demokrasia; msingi wake mkuu ni hoja kwa hoja. Yaani, badala ya watu kutukanana wanatoa hoja. Ushawishi; yaani badala ya watu kupigana na kukabana wanajenga ushawishi. Mijadala; yaani badala ya watu kulazimishana au kudhalilishana wanajadiliana.

Hii ni tofauti na mifumo mingine yote ya siasa ambayo misingi yake ni nguvu, hila, uhuni, dhuluma, ulaghai, uongo au vyote kwa pamoja.

Kwa bahati mbaya tunadai sisi ni wana demokrasia ila tumeachana na misingi hiyo hapo juu. Inapotakiwa kutoa hoja tunaongea ujinga, matusi, mizaha, ushabiki na kudhalilishana. Inapohitajika kutumia akili kufikiri tunatumia maguvu.

Sasa tukirudi kwenye kanuni yetu na kuingunganisha na tatizo linalotukabili; Kama tungeendelea na kufanya mijadala ya hoja kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na tukaendelea kuwekeza kwenye eneo hilo, maana yake tungejijengea uwezo zaidi wa kujenga hoja.

Kwa kuwa kujenga hoja kunahitaji kutumia akili; tungejijengea zaidi uwezo wa kufikiri.Kwa kadiri ambavyo tungekuwa tunajijengea Zaidi uwezo wa kufikiri ndivyo ambavyo tungezidi kujijengea uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabili kwa busara.

Tungekuwa tunaendelea kufanya siasa za ushawishi, tungejijengea uwezo Zaidi wa kushawishi na hivyo tungekuwa na siasa za hoja na ushawishi zaidi kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hiyo ingekuwa ni faida kwa watu wote.

Kwa bahati mbaya tumechagua kinyume chake. Hakuna mtu ambaye amewahi kutoa sababu ya msingi kwamba kwa nini tumeamua kuchagua kinyume chake.

Ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba kuna watu wachache wanaojua kuwa tufanyacho si sahihi na wanachukua hatua, kuna wengi wanaojua tufanyacho si sahihi ila hawachukui hatua, kuna wanaojua ila wanaendelea kwenda kwenye muelekeo usio sahihi huku wakishangaa matokeo.

Kwa kuwa tumechagua kuwa panapohitaji hoja, basi tunaongea ujinga; kwa mujibu wa kanuni yetu hapo juu, tunajikuta tunajijengea uwezo zaidi wa kufikiri na kuongea ujinga.

Kwa kuwa panapohitaji kutumia akili tunatumia msuli; basi tunajijengea nguvu ya msuli badala ya fikra (madhara yake kwa mapana tutayaeleza baadae). Tunapotakiwa kuongea mambo ya msingi tunafanya ushabiki, kwa hiyo tunaongeza uwezo wetu wa kushangilia.

Watu wanasema wana dola, unataka watumie ubongo ili iweje!

Kama kuna vyombo vya dola vinavyotekeleza maagizo kutoka juu, kwa nini watu wajihangaishe na kufikiri!

Watawala wetu wanapenda ganda la ndizi, yaani kuwahoji wayafanyayo ni kuwakwamisha, wanataka wateleze tu kutuletea SGR, ndege, Stiglers gorge nk bila kuulizwa!

Kwa msingi ubongo wa wana CCM umedumaa, hawawezi kujenga hoja kwa kuwa kuna njia rahisi ya kutumia dola badala ya fikra!
 
Mkuu, jitahidi ukiona jambo ambalo si sawa usitafute mtu wa kumlaumu. jiulize wewe unaweza kufanya nini kwa nafasi yako na kwa mazingira yako ili kuboresha yale unayoweza kuboresha.

Unatakiwa uelewe, unayemlaumu naye anakulaumu au analaumu mtu. Kiongozi wa leo, kuna kipindi alikuwa mtoto, akawa kijana, akaenda hadi akafika alikofika. Mtu hafiki mahali kama tukio bali process na ndicho ninachozungumzia hapa.

Kuna watu tumekuwa nao mtaani, tulikuwa na uwezo wa kuwajenga kwa namna fulani hatukufanya hivyo, leo tunasema sasa tufanyeje.

Kuna watu tulikuwa nao hapa jf muda wote, tunapigana vijembe, kujadili ujinga, matusi na ushabiki, baadae wakawa viongozi wakubwa, wakafanya waliyo fanya, tukalaumu tulivyo laumu na kuishia hapo.

Kesho kuna wengine watatoka humu humu, wataiacha dunia midomo wazi na kama kawaida tutalaumu huku tukisema sasa tufanyeje, tunasahau tulikuwa nao humu na tulikuwa na nafasi ya kuwa shape lakini hatukufanya hivyo.
Husomeki, be specific
 
mkuu jd41 mambo mengi nakuelewa vizuri tu na kwenye vipengele kadhaa nakubaliana na wewe.

sasa ningeomba hebu tutanue mjadala kidogo. Tuangalie kwenye picha pana Zaidi kidogo nje ya CCM na CHADEMA. Hiyo inaweza kutupa uwezo wa kuona mambo kwenye mwanga bora Zaidi.

Hivi hakuna mambo mengi tu ambayo yako nje ya hiyo ligi na yangepaswa kufanywa lakini hakuna anayefanya, na ukiuliza amma haujibiwi, au unashambuliwa vibaya mno, au unayemuuliza atafanya mbinu hadi asingizie tatizo ni mwenzake?

Je! Unawezaje kuzungumzia wanaohama hama vyama kila mara bila maelezo ya msingi na kuyakana yale wanayotetea accordingly? kwa hali hiyo ni nani anaaminika na kwa nini? au nani anapaswa kuaminiwa na kwa nini?

Hatuoni anayelalamika kuteswa leo inawezekana kakaa angle mbaya ndio maana analalamika ila akipata angle nzuri atafanya yale yale anayolalamikia?na kinyume chake, sasa hapo tunategemea katika upana wake baadae iwe nini na maswali mengine kama hayo.

Kwa maoni yangu tunapoangalia kila jambo katika level ya CCM na CHADEMA na tukaishia hapo tunakuwa tumejifungia kwenye kachumba kadogo sana halafu kaliko jaa mambo kiasi kwamba unaweza kukosa hewa. Ni muhimu kwanza kutanua duara.
Ok, tukitoka nje ya hivyo vyama viwili, tuzungumzie wanaohama hama vyama.

Hapo wanasiasa wetu wengi wako kimaslahi zaidi, nimechunguza nikaona kwamba wengi huwa wanatazama kwanza ni upande gani (chama gani) kina soko kwa wakati husika, hivyo hukimbilia kule wanapoamini kuna nguvu zaidi ya wao kushinda, either kwa kupigiwa kura na wapigakura au kubebwa na nguvu za nje (dola).

Sababu ya kutafuta maslahi kwao imekuwa ngumu kuitaja mbele za umma, hivyo hujikuta wakilazimisha kutoa sababu nyepesi nyepesi ilimradi kuhalalisha uamuzi wao wa kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Lakini sababu sio hiyo pekee, tumeona kuna baadhi ya wanasiasa wakitishwa na kulazimishwa kuhama toka upande mmoja kwenda mwingine, japo nao wakihama hushindwa kusema kweli kuogopa kuwaudhi waliokubaliana nao, hivyo kwa mtazamo wangu, sababu hasa za wanasiasa kuhama toka upande mmoja kwenda mwingine ni hizo mbili kubwa.

Na inawezekana ikawa kweli unachosema, hata hao wanaolalamika kwasasa inawezekana wanalia kwasababu wapo kwenye angle mbaya, siku nao wakifika kileleni wanaweza kufanya hayo hayo wanayoyalalamikia kwasasa.

Kusema kweli hapo sioni wakumuamini, wanatuchezea akili tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea mambo ya msingi sana. Lakini sasa hii inaanza na mtu mmoja mmoja kwa sababu hakuna kitu kama 'chama' ambacho kiko pale. Tatizo sasa linakuja kila mtu anadhani sio yeye, bali wapo "watu"
Tatizo lililopo kwenye hilo nililozungumza naona itakuwa ngumu sana kwasasa kutengeneza kizazi cha aina hiyo.

Naona tabia ya kutukana, kukejeli, imeachwa kwa muda sana sasa ipo kwenye DNA ya wanachama na wapenzi wa vyama husika.

Sijui itawezekanaje kuanza na mtu mmoja mmoja wakati watu hao hao ndio sehemu ya tatizo lililopo hivi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu jd41 kuna mambo mengi ambayo yana changamoto nyingi na kubwa, ila ukweli ni kwamba hatuwezi kutatua mambo makubwa kabla ya kutatua mambo madogo kwanza

Kwa mfano kabla ya kwenda mbali sana, tujiulize tu kuwa sisi tuliopo jf kwa mfano, tunafanya nini, ili kutatua tatizo gani, wapi lini na kwa faida ya nani angalau kwa aina ya maoni tunayotoa tu?

unaweza kusema hilo ni jambo dogo sana, sawa; nakubali ni jambo dogo, lakini kama mtu anashindwa kuji behave kwenye jambo dogo, atawezaje kuji behave kwenye jambo kubwa? Kwa hiyo matatizo unayosema yapo ni kweli yapo, ila watu wanadai wanataka kutatua hayo makubwa wakati kuna vikitu vidogo vidogo tu ambavyo hawavifanyi na viko ndani ya uwezo wao na vina faida kwa mustakabali mzima wa siasa zetu.

Kwa mfano, mtu anaweza kuona kuna hoja nzuri, ambayo inasaidia kutatua tatizo Fulani (hata kama kwa asilimia ndogo) hachangii, akichangia anakuuliza mbona hunipi nafasi ya kuchangia, unamwambia haya changia, anakimbia, kesho yake unakuta analaumu hakuna demokrasia.
Hivi hapa ni mdogo ndio huanza kujifunza toka kwa mkubwa au mkubwa ndio hujifunza toka kwa mdogo?

Unavyosema inabidi sisi hapa jf kwa mfano tuanze kushughulikia vitu ulivyoviita vidogo vidogo, ni kama vile unataka wale wakubwa wanaokosea ndio wajifunze toka kwetu.

Kwa mfano uliotoa ni kweli, ukimya huchangia kukuza tatizo, ila pia nakosa ujasiri wa kulaumu huo ukimya kwasababu tumekuzwa kwenye mazingira ya kutofanyiwa kazi kile mtu atachosema, au niseme ushauri atakaotoa.

Chukulia mfano hata bungeni, kuna kundi kubwa la wabunge lililozoea kuzomea kundi dogo hata kwenye hoja za msingi kwa maslahi ya taifa.

Na ukitazama wengi wanaounda hilo kundi kubwa, wana elimu zao nzuri tu, lakini wameamua kwa makusudi kabisa, kwa mapenzi kwa chama chao, kupinga kila jema linalosemwa na kundi dogo.

Je, unaamini sisi hapa jf, tunaweza kubadilisha mtazamo wa lile kundi kubwa kwa aina ya michango tutakayokuwa tunaitoa? kwasababu navyoamini mimi, wale viongozi ndio wangetakiwa kuanza kuonesha mfano kwetu, sababu nijuavyo kwenye jamii yetu, mdogo ndio hujifunza kwa mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jd41 nadhani hujanielewa vizuri, sizungumzii habari ya mkubwa kujifunza kwa mdogo au mdogo kujifunza kwa mkubwa.

Ninachosema ni kila mmoja achukua hatua anazoweza kulingana na mazingira yake. Kwa lugha nyingine tuache utamaduni wa kila mmoja kudhani anayetakiwa kufanya kitu ni mwenzake tu.

Kila mtu anatakiwa kuwajibika hata kama impact yake ni ndogo, lakini bado ni muhimu.kunbuka kuna mtu au vitu unaweza kuona haviko sawa ila kulingana na mazingira yako huwezi vibadili, katika hali hiyo anza na kilichipo ndani ya uwezo wako na ndio nikatoa mfano wa jf.
 
Hapa nimekuelewa.

Naona unaondoa dhana ya kuwa na role model, so that kila mmoja awe role model kwa mwenzie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetoa mfano mzuri,lakini kaa ukijua kuwa Vita vya panga haviamuliwi kwa panga.

Lakini pia angalia hii hamahama ya watu kutoka CDM...watu wanatumia haki ya kidemokrasia ya kujiunga na CCM,imegeuka kuwa nongwa kwa CDM...wanawaita majina yote mabaya na matusi juu hadi hata kupeana mikono hwataki.

Sikatai kuwa hata CCM kuna ujinga huo huo,lakini CDM umezidi,ukionekana tu upo upande wa serikali utaoga matusi vijembe kejeli na kudharauliwa....ndio maana hata kulikuwa na zomeazomea kipindi flani....CDM hao. Unamzomea mtu,unamwita kondoo halafu kesho unatarajia akupe kura!

Tujifunze kujibu hoja na kushawishi....The power of Influence...sio kugombanisha watu mtaani.
Hayo yote yana chanzo, tujiulize kwanini CDM na wafuasi wake wamefikia hali hiyo, na kama mleta mada anavyosema, jambo likitendeka sana hukua, na kinyume chake hufa, sasa tujiulize; kama wafuasi wa CDM wakiwa na hoja je, upande wa pili huwa na majibu sahihi ya hoja zao? jibu ni hapana.

Chukua mfano; kauli ya Bashiru ya hivi karibuni CCM inalindwa na dola, ni nani umewahi kumsikia kutoka upande wa pili akikanusha hoja ile officially, jibu ni hakuna. CCM nao badala yake hujibu kwa vijembe kwamba wao wameshika mpini, na ukiwatazama vizuri unaona kabisa wanajivunia nguvu ya dola iliyo upande wao.

Mfano mwingine; matumizi ya jeshi la polisi kwenye shughuli za kisiasa, utakuta mtu kama Mbowe anafanya mkutano wake halafu wanaibuka wasumbufu wanaanza kufanya fujo pasipo polisi kuingilia kati, japo wanakuwepo jirani, watu wanasubiri kusikia kauli ya kukemea toka kwa viongozi wa serikali lakini huwa kimya.

Haya mambo husababisha watu kuwa sugu, wanaona hakuna fairness, hakuna yeyote toka upande wowote anaekubali makosa ya chama chake. Hivyo inajengeka imani kwamba wale ni kundi la walionacho na sisi ni kundi la wasionacho, hapo panakuwa hakuna tena demokrasia, matokeo yake ni matusi na kejeli, kwasababu ya kuchoka kuonewa, matusi yanakuwa kama source fulani ya kuipumzisha nafsi ( soul satisfaction).

Wewe binafsi ni mfano wa yale mleta mada anayozungumzia, umeona ubaya wa CDM pekee but usitake kuniambia hujawahi kuona udhaifu/ ubaya toka chama kingine, hopefully ndio kitakuwa chama chako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yote yana chanzo, tujiulize kwanini CDM na wafuasi wake wamefikia hali hiyo, na kama mleta mada anavyosema, jambo likitendeka sana hukua, na kinyume chake hufa, sasa tujiulize; kama wafuasi wa CDM wakiwa na hoja je, upande wa pili huwa na majibu sahihi ya hoja zao? jibu ni hapana.

Chukua mfano; kauli ya Bashiru ya hivi karibuni CCM inalindwa na dola, ni nani umewahi kumsikia kutoka upande wa pili akikanusha hoja ile officially, jibu ni hakuna. CCM nao badala yake hujibu kwa vijembe kwamba wao wameshika mpini, na ukiwatazama vizuri unaona kabisa wanajivunia nguvu ya dola iliyo upande wao.

Mfano mwingine; matumizi ya jeshi la polisi kwenye shughuli za kisiasa, utakuta mtu kama Mbowe anafanya mkutano wake halafu wanaibuka wasumbufu wanaanza kufanya fujo pasipo polisi kuingilia kati, japo wanakuwepo jirani, watu wanasubiri kusikia kauli ya kukemea toka kwa viongozi wa serikali lakini huwa kimya.

Haya mambo husababisha watu kuwa sugu, wanaona hakuna fairness, hakuna yeyote toka upande wowote anaekubali makosa ya chama chake. Hivyo inajengeka imani kwamba wale ni kundi la walionacho na sisi ni kundi la wasionacho, hapo panakuwa hakuna tena demokrasia, matokeo yake ni matusi na kejeli, kwasababu ya kuchoka kuonewa, matusi yanakuwa kama source fulani ya kuipumzisha nafsi ( soul satisfaction).

Wewe binafsi ni mfano wa yale mleta mada anayozungumzia, umeona ubaya wa CDM pekee but usitake kuniambia hujawahi kuona udhaifu/ ubaya toka chama kingine, hopefully ndio kitakuwa chama chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetoa mfano mzuri,lakini kaa ukijua kuwa Vita vya panga haviamuliwi kwa panga.

Lakini pia angalia hii hamahama ya watu kutoka CDM...watu wanatumia haki ya kidemokrasia ya kujiunga na CCM,imegeuka kuwa nongwa kwa CDM...wanawaita majina yote mabaya na matusi juu hadi hata kupeana mikono hwataki.

Sikatai kuwa hata CCM kuna ujinga huo huo,lakini CDM umezidi,ukionekana tu upo upande wa serikali utaoga matusi vijembe kejeli na kudharauliwa....ndio maana hata kulikuwa na zomeazomea kipindi flani....CDM hao. Unamzomea mtu,unamwita kondoo halafu kesho unatarajia akupe kura!

Tujifunze kujibu hoja na kushawishi....The power of Influence...sio kugombanisha watu mtaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lililopo kwenye hilo nililozungumza naona itakuwa ngumu sana kwasasa kutengeneza kizazi cha aina hiyo.

Naona tabia ya kutukana, kukejeli, imeachwa kwa muda sana sasa ipo kwenye DNA ya wanachama na wapenzi wa vyama husika.

Sijui itawezekanaje kuanza na mtu mmoja mmoja wakati watu hao hao ndio sehemu ya tatizo lililopo hivi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye jambo lolote liwe zuri au baya kiasi gani, katika udogo au ukubwa wake linaanza na mtu mmoja mmoja. Tukishaelewa hiyo principle, tunakuwa tushapiga hatua ya kwanza, kwa kadiri tunavyochelewa kuielewa na kuifanyia kazi ndivyo tatizo linakuwa kubwa zaidi na zaidi.

Hata hivyo nakubaliana nawe kwamba tatizo ni kubwa sana, lakini maisha yanatakiwa yaendelee, sasa option haiwezi kuwa kutofanya kitu
 
Hapa nimekuelewa.

Naona unaondoa dhana ya kuwa na role model, so that kila mmoja awe role model kwa mwenzie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Role model ni kitu kizuri, lakini unafanyaje pale yule ambaye ungetamani awe role model anapoamua kuwa kinyume chake? Je! Utamlazimisha! Lakini unao uwezo wa kumlazimisha? Utamuomba? Utamshawishi?

Kama kuna unaloweza kati ya hayo fanya, ila kama huna basi fanya lile uwezalo katika udogo au ukubwa wake.

Ninachosisitiza ni kwamba kutochukua hatua kwa kisingizio chochote sio option bora kwa kuwa inaongeza tatizo la msingi
 
Umetoa mfano mzuri,lakini kaa ukijua kuwa Vita vya panga haviamuliwi kwa panga.

Lakini pia angalia hii hamahama ya watu kutoka CDM...watu wanatumia haki ya kidemokrasia ya kujiunga na CCM,imegeuka kuwa nongwa kwa CDM...wanawaita majina yote mabaya na matusi juu hadi hata kupeana mikono hwataki.

Sikatai kuwa hata CCM kuna ujinga huo huo,lakini CDM umezidi,ukionekana tu upo upande wa serikali utaoga matusi vijembe kejeli na kudharauliwa....ndio maana hata kulikuwa na zomeazomea kipindi flani....CDM hao. Unamzomea mtu,unamwita kondoo halafu kesho unatarajia akupe kura!

Tujifunze kujibu hoja na kushawishi....The power of Influence...sio kugombanisha watu mtaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo neno ulilotumia "watu wanahama kutumia haki yao kidemokrasia" ni kichaka tu mnachojifichia ili kuhalalisha uhamaji haramu.

Unasema hata CCM kuna ujinga huo huo ila CDM umezidi sijui umetumia kipimo gani? hivi kati ya anayezomea na kukejeli, na anayepiga na kuumiza yupi mbaya zaidi?

Usiwasemee watu, wao ndio wenye siri ya uhamaji wao, tumeona viongozi wa Chadema wakitishwa maisha ili kuhamia upande wa pili, wengine kupigwa kwasababu ya kugoma kuhamia upande wa pili, wengine kuhongwa pesa ili tu wahamie upande wa pili ( Meya wa Chadema Iringa Mjini).

Kuna kina Mawazo walipigwa mpaka kuuawa mpaka leo hakuna hata mmoja aliewahi kukamatwa akituhumiwa kwa mauaji yale, achilia mbali kufungwa gerezani, badala yake tunaona kina Mbowe wakienda gerezani kila siku kwa kesi za kutengeneza.

Hiyo niliyokupa ni mifano michache tu inayothibitisha huko ulipo hakuna hiyo demokrasia unayoizungumzia, hivyo kuzomewa na kukejeliwa ni haki yenu, sijui nyie mlitaka mpongezwe kwa hayo matendo ya hovyo mnayoyafanya?

Sasa ndio mleta mada anakwambia, anza wewe kukemea huo upuuzi kwa level yako, usikae kunyooshea tu CDM kidole kwa mtindo huo hautamaliza tatizo, coz hata CDM nao wana haki ya kuwanyooshea nyie vidole kwa mnayowafanyia viongozi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom