Practical side of “The law of use and misuse” in Tanzanians politics

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
1584197392271.png

Kuna kanuni moja muhimu sana katika sayansi ambayo leo tungependa kuichambua kwa kina na kueleza jinsi inavyoathiri siasa za Tanzania na kusababisha jamii yote kwa ujumla kupoteza mueleko ikiwemo wengi miongoni mwa wanaosoma mada hii.

Kupitia uchambuzi wa huu, tutajibu kwanini kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida yanatokea kila mahali ikiwemo humu JF na kutoa suluhu na kueleza nini kitatokea ikiwa tutaendelea kufanya tufanyavyo.

Nazungumzia kanuni inayojukikana kama “the law of use and disuse”. Kanuni hii inasema kwamba, “Whenever you use, it grows and whenever you don’t use you loose” Yaani “Kwa kadiri unavyotumia kitu ndivyo kinavyokuwa kwa kadiri usivyokitumia kinapotea".

Siasa za demokrasia; msingi wake mkuu ni hoja kwa hoja. Yaani, badala ya watu kutukanana wanatoa hoja. Ushawishi; yaani badala ya watu kupigana na kukabana wanajenga ushawishi. Mijadala; yaani badala ya watu kulazimishana au kudhalilishana wanajadiliana.

Hii ni tofauti na mifumo mingine yote ya siasa ambayo misingi yake ni nguvu, hila, uhuni, dhuluma, ulaghai, uongo au vyote kwa pamoja.

Kwa bahati mbaya tunadai sisi ni wana demokrasia ila tumeachana na misingi hiyo hapo juu. Inapotakiwa kutoa hoja tunaongea ujinga, matusi, mizaha, ushabiki na kudhalilishana. Inapohitajika kutumia akili kufikiri tunatumia maguvu.

Sasa tukirudi kwenye kanuni yetu na kuingunganisha na tatizo linalotukabili; Kama tungeendelea na kufanya mijadala ya hoja kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na tukaendelea kuwekeza kwenye eneo hilo, maana yake tungejijengea uwezo zaidi wa kujenga hoja.

Kwa kuwa kujenga hoja kunahitaji kutumia akili; tungejijengea zaidi uwezo wa kufikiri.Kwa kadiri ambavyo tungekuwa tunajijengea Zaidi uwezo wa kufikiri ndivyo ambavyo tungezidi kujijengea uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabili kwa busara.

Tungekuwa tunaendelea kufanya siasa za ushawishi, tungejijengea uwezo Zaidi wa kushawishi na hivyo tungekuwa na siasa za hoja na ushawishi zaidi kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hiyo ingekuwa ni faida kwa watu wote.

Kwa bahati mbaya tumechagua kinyume chake. Hakuna mtu ambaye amewahi kutoa sababu ya msingi kwamba kwa nini tumeamua kuchagua kinyume chake.

Ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba kuna watu wachache wanaojua kuwa tufanyacho si sahihi na wanachukua hatua, kuna wengi wanaojua tufanyacho si sahihi ila hawachukui hatua, kuna wanaojua ila wanaendelea kwenda kwenye muelekeo usio sahihi huku wakishangaa matokeo.

Kwa kuwa tumechagua kuwa panapohitaji hoja, basi tunaongea ujinga; kwa mujibu wa kanuni yetu hapo juu, tunajikuta tunajijengea uwezo zaidi wa kufikiri na kuongea ujinga.

Kwa kuwa panapohitaji kutumia akili tunatumia msuli; basi tunajijengea nguvu ya msuli badala ya fikra (madhara yake kwa mapana tutayaeleza baadae). Tunapotakiwa kuongea mambo ya msingi tunafanya ushabiki, kwa hiyo tunaongeza uwezo wetu wa kushangilia.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Ungeandika yote hapo hapo!
Mada ni ndefu kidogo, kwa hiyo tunaenda taratibu. Karibu tubadilishane mawazo na tusaidiane kubadilisha mawazo ya watanzania kwa namna ambayo itasaidia kuwezesha mabadiliko chanya tatokee.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Sasa kwa kuwa kwa kadiri unavyotumia kitu/akili/mwili ndivyo inavyokuwa kwa mujibu wa kanuni kwenye uzi wa msingi; na sisi tumeamua kujiimarisha kwenye siasa hizi tulizochagua, basi ndivyo tunakuwa hivi tulivyo, na kwa kadiri tunavyoendelea ndivyo tutakavyozidi kuwa hivi tunavyokuwa huku kila mtu akishangaa kwa nini sasa tumekuwa hivi na kwa nini tunaendelea kuwa hivyo tunavyokuwa
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Haijalishi unatembea taratibu au kwa kukimbia;Kama unaenda kwenye mwelekeo usio sahihi, ni hakika utasogea na utafika unakoenda.

Kadhalika, tembea utakavyotembea, taratibu au kwa kasi lakini maadamu kwenye muelekeo sahihi, utasogea na ipo siku utafika.

Ni muhimu kuchagua, ama kujisahihisha au kuendelea kupotea, huku tukiwa na uhakika kwamba hakuna anayenufaika na upotevu wetu ikiwemo sisi wenyewe.Lazima tuelewe kwamba mpaka tunafika tulipo, kila mtu kuna namna anashindwa kuwajibika mahali. Na njia peke ya kutoka tulipo ni kubadili muelekeo, vinginevyo, tulaumu tusilaumu, tulaumiane tusilaumiane, tushangaane au tusishangaane kama tutaendelea kwenda kwenye wrong directions, nafikiri haihitaji akili nyingi kujua kinachotarajiwa.
 
Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,118
2,000
Kuna kanuni moja muhimu sana katika sayansi ambayo leo tungependa kuichambua kwa kina na kueleza jinsi inavyoathiri siasa za Tanzania na kusababisha jamii yote kwa ujumla kupoteza mueleko ikiwemo wengi miongoni mwa wanaosoma mada hii.

Kupitia uchambuzi wa huu, tutajibu kwanini kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida yanatokea kila mahali ikiwemo humu JF na kutoa suluhu na kueleza nini kitatokea ikiwa tutaendelea kufanya tufanyavyo.

Nazungumzia kanuni inayojukikana kama “the law of use and misuse”. Kanuni hii inasema kwamba, “Whenever you use, it grows and whenever you don’t use you loose” Yaani “Kwa kadiri unavyotumia kitu ndivyo kinavyokuwa kwa kadiri usivyokitumia kinapotea".

Siasa za demokrasia; msingi wake mkuu ni hoja kwa hoja. Yaani, badala ya watu kutukanana wanatoa hoja. Ushawishi; yaani badala ya watu kupigana na kukabana wanajenga ushawishi. Mijadala; yaani badala ya watu kulazimishana au kudhalilishana wanajadiliana. Hii ni tofauti na mifumo mingine yote ya siasa ambayo misingi yake ni nguvu, hila, uhuni, dhuluma, ulaghai, uongo au vyote kwa pamoja.

Kwa bahati mbaya tunadai sisi ni wana demokrasia ila tumeachana na misingi hiyo hapo juu. Inapotakiwa kutoa hoja tunaongea ujinga, matusi, mizaha, ushabiki na kudhalilishana. Inapohitajika kutumia akili kufikiri tunatumia maguvu.

Sasa tukirudi kwenye kanuni yetu na kuingunganisha na tatizo linalotukabili; Kama tungeendelea na kufanya mijadala ya hoja kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na tukaendelea kuwekeza kwenye eneo hilo, maana yake tungejijengea uwezo zaidi wa kujenga hoja. Kwa kuwa kujenga hoja kunahitaji kutumia akili; tungejijengea zaidi uwezo wa kufikiri.Kwa kadiri ambavyo tungekuwa tunajijengea Zaidi uwezo wa kufikiri ndivyo ambavyo tungezidi kujijengea uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabili kwa busara.

Tungekuwa tunaendelea kufanya siasa za ushawishi, tungejijengea uwezo Zaidi wa kushawishi na hivyo tungekuwa na siasa za hoja na ushawishi zaidi kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hiyo ingekuwa ni faida kwa watu wote.

Kwa bahati mbaya tumechagua kinyume chake. Hakuna mtu ambaye amewahi kutoa sababu ya msingi kwamba kwa nini tumeamua kuchagua kinyume chake. Ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba kuna watu wachache wanaojua kuwa tufanyacho si sahihi na wanachukua hatua, kuna wengi wanaojua tufanyacho si sahihi ila hawachukui hatua, kuna wanaojua ila wanaendelea kwenda kwenye muelekeo usio sahihi huku wakishangaa matokeo.

Kwa kuwa tumechagua kuwa panapohitaji hoja, basi tunaongea ujinga; kwa mujibu wa kanuni yetu hapo juu, tunajikuta tunajijengea uwezo zaidi wa kufikiri na kuongea ujinga. Kwa kuwa panapohitaji kutumia akili tunatumia msuli; basi tunajijengea nguvu ya msuli badala ya fikra (madhara yake kwa mapana tutayaeleza baadae).Tunapotakiwa kuongea mambo ya msingi tunafanya ushabiki, kwa hiyo tunaongeza uwezo wetu wa kushangilia.
Wapinzani wakati mwingine wana hoja za msingi na nzuri sana tatizo wanavyoziwakilisha. Ila 2020 wengi wanakosa ubunge. Maana sasa hawapendeki kabisa, wanaishia kukodi watu kuja kwenye mikutano
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Wapinzani wakati mwingine wana hoja za msingi na nzuri sana tatizo wanavyoziwakilisha. Ila 2020 wengi wanakosa ubunge. Maana sasa hawapendeki kabisa, wanaishia kukodi watu kuja kwenye mikutano
Tanzania hatujawahi kuwa na tatizo la chama cha siasa. Hilo ni tatizo bandia. Tuna tatizo la watu mmoja mmoja. Tunapounganisha mtu mmoja mmoja mwenye tatizo tunapata kundi lenye matatizo. mtu huyo mmoja mmoja ataendelea kuwa na matatizo na kundi litaendelea kuwa na matatizo bila Kujali jina la kundi husika (liite jina upendalo) na hali hiyo haiabadilika mpaka mtu mmoja mmoja atakapoamua kwa dhati kubadilika.

Hoja hii tumekuwa tukiitoa mara kwa mara.Kwa bahati mbaya haijawahi kupingwa wala kuwa challenged kwa namna yoyote, kinyume chake kila mtu hujifanya kama hajaiona, halafu siku inayofuata anaibuka kulalamikia mambo yale yale. "Utasikia kila mtu anahoji hivi tunaelekea wapo?" kama vile tunaendeshwa na majanga ya asili.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Kuna watu wanadai aina ya mabadiliko tunayopendekeza yatatuchelewesha kupata tunayohitaji. Wanasahau kwamba kuna vitu havifai kuharakisha na ukiharakisha bila kufuata hatua stahiki unapata matokeo ya bandia.

Ni sawa na wewe ni daktarin, watu wana maabukizi kwenye damu ambayo yanawatafuna kwa ndani vibaya mno na wanaendelea kuambukizana. Halafu wanataka uwashauri wapake make up usoni na mafuta mwilini ili waonekane wako "Fit" huku wanaoza kwa ndani.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Wewe mwana JF kwa mfano unapaswa kuelewa; unapoandika kitu hapa, akaandika na mwingine na mwingine, 1x2x5x100x20000...… hiyo mwisho wa siku unakuwa ndio msimamo wa umma lakini mwanzo ilianza kama mtu mmoja tu.

Kwa hiyo kama umeandika jambo la maana, na mwingine la maana, na mwingine point; mwishowe inakuwa ndio umma huo na mwisho unakuta hiyo inapelekea vitu vya maana kutokea.

Kama unashabikia ujinga kwa mfano, au kuandika vitu ambavyo havisaidii kuleta unafuu wowote kwenye jambo flani na wengine wakafanya kama wewe, mwishowe huo unakuwa ndio umma.

Halafu baadae kwa pamoja mnaungana kushangaa nini kinatokea, huku kila mtu akidai sio yeye na yeye hana la kufanya.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,526
2,000
Kuna watu wanadai aina ya mabadiliko tunayopendekeza yatatuchelewesha kupata tunayohitaji. Wanasahau kwamba kuna vitu havifai kuharakisha na ukiharakisha bila kufuata hatua stahiki unapata matokeo ya bandia.

Ni sawa na wewe ni daktarin, watu wana maabukizi kwenye damu ambayo yanawatafuna kwa ndani vibaya mno na wanaendelea kuambukizana. Halafu wanataka uwashauri wapake make up usoni na mafuta mwilini ili waonekane wako "Fit" huku wanaoza kwa ndani.
Mkuu hoja zako zimeenda shule. Huwa nasikitika sana thread za aina hii hazipati credit inayostahili hapa. Badala yake zile za propaganda uongo, kusutana na kutambiana ndiyo zina wachangiaji wengi. Thread zako hazinipiti. Huwa nazisoma mara mbili mbili. Natamani sana mtu kama rais wa nchi au kiongozi wa chama angekutumia wewe kuandaa hotuba zake. Huo uwezo unao kabisa.
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,002
2,000
Kuna kanuni moja muhimu sana katika sayansi ambayo leo tungependa kuichambua kwa kina na kueleza jinsi inavyoathiri siasa za Tanzania na kusababisha jamii yote kwa ujumla kupoteza mueleko ikiwemo wengi miongoni mwa wanaosoma mada hii.

Kupitia uchambuzi wa huu, tutajibu kwanini kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida yanatokea kila mahali ikiwemo humu JF na kutoa suluhu na kueleza nini kitatokea ikiwa tutaendelea kufanya tufanyavyo.

Nazungumzia kanuni inayojukikana kama “the law of use and misuse”. Kanuni hii inasema kwamba, “Whenever you use, it grows and whenever you don’t use you loose” Yaani “Kwa kadiri unavyotumia kitu ndivyo kinavyokuwa kwa kadiri usivyokitumia kinapotea".

Siasa za demokrasia; msingi wake mkuu ni hoja kwa hoja. Yaani, badala ya watu kutukanana wanatoa hoja. Ushawishi; yaani badala ya watu kupigana na kukabana wanajenga ushawishi. Mijadala; yaani badala ya watu kulazimishana au kudhalilishana wanajadiliana. Hii ni tofauti na mifumo mingine yote ya siasa ambayo misingi yake ni nguvu, hila, uhuni, dhuluma, ulaghai, uongo au vyote kwa pamoja.

Kwa bahati mbaya tunadai sisi ni wana demokrasia ila tumeachana na misingi hiyo hapo juu. Inapotakiwa kutoa hoja tunaongea ujinga, matusi, mizaha, ushabiki na kudhalilishana. Inapohitajika kutumia akili kufikiri tunatumia maguvu.

Sasa tukirudi kwenye kanuni yetu na kuingunganisha na tatizo linalotukabili; Kama tungeendelea na kufanya mijadala ya hoja kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na tukaendelea kuwekeza kwenye eneo hilo, maana yake tungejijengea uwezo zaidi wa kujenga hoja. Kwa kuwa kujenga hoja kunahitaji kutumia akili; tungejijengea zaidi uwezo wa kufikiri.Kwa kadiri ambavyo tungekuwa tunajijengea Zaidi uwezo wa kufikiri ndivyo ambavyo tungezidi kujijengea uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabili kwa busara.

Tungekuwa tunaendelea kufanya siasa za ushawishi, tungejijengea uwezo Zaidi wa kushawishi na hivyo tungekuwa na siasa za hoja na ushawishi zaidi kwa kadiri muda unavyozidi kwenda na hiyo ingekuwa ni faida kwa watu wote.

Kwa bahati mbaya tumechagua kinyume chake. Hakuna mtu ambaye amewahi kutoa sababu ya msingi kwamba kwa nini tumeamua kuchagua kinyume chake. Ambalo tuna uhakika nalo ni kwamba kuna watu wachache wanaojua kuwa tufanyacho si sahihi na wanachukua hatua, kuna wengi wanaojua tufanyacho si sahihi ila hawachukui hatua, kuna wanaojua ila wanaendelea kwenda kwenye muelekeo usio sahihi huku wakishangaa matokeo.

Kwa kuwa tumechagua kuwa panapohitaji hoja, basi tunaongea ujinga; kwa mujibu wa kanuni yetu hapo juu, tunajikuta tunajijengea uwezo zaidi wa kufikiri na kuongea ujinga. Kwa kuwa panapohitaji kutumia akili tunatumia msuli; basi tunajijengea nguvu ya msuli badala ya fikra (madhara yake kwa mapana tutayaeleza baadae).Tunapotakiwa kuongea mambo ya msingi tunafanya ushabiki, kwa hiyo tunaongeza uwezo wetu wa kushangilia.
Upande wa mpini kashika kichaa tutawezaje kujadiliana naye?
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Unatakiwa uwelewe unachoandika humu kwa mfano, kuna watu wanasoma, na kwa kadiri wanavyosoma kwa kurudia rudia inaathiri namna yao ya kufikiri. Kwa hiyo wakisoma kwa kurudia rudia mada na comment za maana inawashawishi kuwa watu wa maana, wakirudia rudia comment za kijinga inawasababisha kuwa wajinga.Sio kwamba wanaamua, inatokea tu.

wakirudia rudia kuandika au kusoma comment zinazodhalilisha wengine wanajijengea tabia ya udhalilishaji n.k na hii inatokea automatically. Mtu hapangi kwamba sasa nataka niwe 'mnoko' kwa mfano, inatokea tu pale anapopata taarifa za namna hiyo kwa wingi zinajaa kicwani mwake na anaanza kuzifanyia kazi.

Kwa hiyo tusishangaee ni nini kinatokea au inakuwaje; ni kanuni kadhaa zinakuwa zinafanya kazi.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Mkuu hoja zako zimeenda shule. Huwa nasikitika sana thread za aina hii hazipati credit inayostahili hapa.
Mkuu, nakushauri usishangae wala usisikitike. Tuungane tuibadili Tanzania. Ijapokuwa taratibu taratibu ila kwa uhakika Zaidi. Wa kuleta mabadiliko ya msingi ni mimi na wewe na mwingine na mwingine.

Mimi nilipita kipindi cha kushangaa, nikapita kipindi cha kusikitika, nikapita kipindi cha kulaumu, nikapita kipindi cha kukata tamaa, sasa niko kwenye kipindi cha kuchukua hatua. Nakushauri tuungane tuchukue hatua na kuwashawishi wengine wafanye the same.

Jamii yetu ishafika kwenye hatua mbaya sana na kibaya Zaidi haijijui kama inakabiliwa na tatizo la msingi na ndio maana unaona hali iko hivi. Kwa hiyo wala usishangae ni jambo linalotarajiwa.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Upande wa mpini kashika kichaa tutawezaje kujadiliana naye?
Mkuu, jitahidi ukiona jambo ambalo si sawa usitafute mtu wa kumlaumu. jiulize wewe unaweza kufanya nini kwa nafasi yako na kwa mazingira yako ili kuboresha yale unayoweza kuboresha.

Unatakiwa uelewe, unayemlaumu naye anakulaumu au analaumu mtu. Kiongozi wa leo, kuna kipindi alikuwa mtoto, akawa kijana, akaenda hadi akafika alikofika. Mtu hafiki mahali kama tukio bali process na ndicho ninachozungumzia hapa.

Kuna watu tumekuwa nao mtaani, tulikuwa na uwezo wa kuwajenga kwa namna fulani hatukufanya hivyo, leo tunasema sasa tufanyeje.

Kuna watu tulikuwa nao hapa jf muda wote, tunapigana vijembe, kujadili ujinga, matusi na ushabiki, baadae wakawa viongozi wakubwa, wakafanya waliyo fanya, tukalaumu tulivyo laumu na kuishia hapo.

Kesho kuna wengine watatoka humu humu, wataiacha dunia midomo wazi na kama kawaida tutalaumu huku tukisema sasa tufanyeje, tunasahau tulikuwa nao humu na tulikuwa na nafasi ya kuwa shape lakini hatukufanya hivyo.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Hakuna mtu anayezaliwa mbaya, watu huwa hufanywa kuwa wabaya au wazuri na mambo wanayoingiza vichwani mwao. Watu huingiza vitu vichwani, kwa kuona, kusikia, kusoma, kufanya au kufanyiwa.

Kwa hiyo mada yako moja au comment moja unayoandika kwenye mtandao wa kijamii unaidharau ila inatosha kabisa kuandaa kundi la watu wema au waovu wazuri au wabaya.

Kwa bahati mbaya Zaidi hili ni jukwaa la siasa, siasa huandaa viongozi, viongozi huamua muelekeo wa nchi ukiwemo wewe; sasa fikiria huyo unayemuandaa kila siku anasoma nini? anasikia nini? anafanya nini? anaona nini? anafanyiwa nini?

Halafu kesho kutwa akiwa kiongozi wako, akifanya miujiza unashangaa nini kinatokea!
 
dolomon

JF-Expert Member
Jun 5, 2018
546
1,000
Umesema jambo jema sana, yaani kuna watu hasa CHADEMA,ukiwa kinyume tu na mtazamo wao unakuwa ADUI! Wana democrasia hawa hunishangaza sana....badala ya kujadili hoja,wao huja na matusi kejeli na kuitana majina mabaya na ya hovyo. Kuna wana mabadiliko humu wapo vizuri sana,badala ya kutusi,wanashawishi,ulipopotoka anakurekebisha na maisha yanaendelea.

Naomba nikukose hy kanuni,unless useme hy ni kanuni yako na sio ya Darwini au Lameck kati yao, inaotwa Law of use and disuse,sio misuse.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Wengi humu ndani tunapenda zaidi vyama vyetu, hivyo tunakosa ujasiri wa kunyooshea kidole pale chama husika mtu akipendacho kinapokosea, yaani tunaongozwa zaidi na mapenzi kwa chama hivyo tumetiwa upofu wa kukiri pale chama chako kinapokosea.

Hivyo mara nyingi tunajikuta tunaongozwa zaidi na mioyo kwenye kufanya maamuzi/kufikiria kuliko kutumia kichwa uweze kupambanua bila kuhusisha na mapenzi yako binafsi kwa chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Umesema jambo jema sana, yaani kuna watu hasa CHADEMA,ukiwa kinyume tu na mtazamo wao unakuwa ADUI! Wana democrasia hawa hunishangaza sana....badala ya kujadili hoja,wao huja na matusi kejeli na kuitana majina mabaya na ya hovyo. Kuna wana mabadiliko humu wapo vizuri sana,badala ya kutusi,wanashawishi,ulipopotoka anakurekebisha na maisha yanaendelea.

Naomba nikukose hy kanuni,unless useme hy ni kanuni yako na sio ya Darwini au Lameck kati yao, inaotwa Law of use and disuse,sio misuse.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo yote yana chanzo, tujiulize kwanini CDM na wafuasi wake wamefikia hali hiyo, na kama mleta mada anavyosema, jambo likitendeka sana hukua, na kinyume chake hufa, sasa tujiulize; kama wafuasi wa CDM wakiwa na hoja je, upande wa pili huwa na majibu sahihi ya hoja zao? jibu ni hapana.

Chukua mfano; kauli ya Bashiru ya hivi karibuni CCM inalindwa na dola, ni nani umewahi kumsikia kutoka upande wa pili akikanusha hoja ile officially, jibu ni hakuna. CCM nao badala yake hujibu kwa vijembe kwamba wao wameshika mpini, na ukiwatazama vizuri unaona kabisa wanajivunia nguvu ya dola iliyo upande wao.

Mfano mwingine; matumizi ya jeshi la polisi kwenye shughuli za kisiasa, utakuta mtu kama Mbowe anafanya mkutano wake halafu wanaibuka wasumbufu wanaanza kufanya fujo pasipo polisi kuingilia kati, japo wanakuwepo jirani, watu wanasubiri kusikia kauli ya kukemea toka kwa viongozi wa serikali lakini huwa kimya.

Haya mambo husababisha watu kuwa sugu, wanaona hakuna fairness, hakuna yeyote toka upande wowote anaekubali makosa ya chama chake. Hivyo inajengeka imani kwamba wale ni kundi la walionacho na sisi ni kundi la wasionacho, hapo panakuwa hakuna tena demokrasia, matokeo yake ni matusi na kejeli, kwasababu ya kuchoka kuonewa, matusi yanakuwa kama source fulani ya kuipumzisha nafsi ( soul satisfaction).

Wewe binafsi ni mfano wa yale mleta mada anayozungumzia, umeona ubaya wa CDM pekee but usitake kuniambia hujawahi kuona udhaifu/ ubaya toka chama kingine, hopefully ndio kitakuwa chama chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,520
2,000
Wengi humu ndani tunapenda zaidi vyama vyetu,
Mkuu kwa kiasi nakuelewa na kwa kiasi naomba kutofautiana na wewe.

Kuwa mwanachama wa chama fulani haimaanishi uamini au kutetea kitu ambacho wewe ndio ulipaswa kukisahihisha, ujinga, ushabiki, upuuzi na vitu kama hivyo. Kama maana ya vyama vya siasa kwa mtizamo wetu ni hiyo; basi hatuna haja ya kuwa na hivyo vyama kwa sababu viongozi wa nchi hutokana na viongozi wa vyama, viongozi wa vyama hutokana na wanachama, sasa kama wanachama ndio wanatakiwa kuwa hivyo then what is there?

Mimi mwenyewe nina chama na nafikiri wajibu wangu ni kukisaidia pamoja na kusaidia ustawi wa mwanadamu wa ajili ya manufaa ya wote, ndio maana nasema haya nisemayo. Sasa huyo anayesema chama chake ndicho kinachomsababisha awe mtu wa miujiza, tatizo si chama tatizo ni yeye.

Mara nyingi tumeeleza kuwa vyama sio vitu 'objective' ni 'abstract'. Kwa hiyo tunaposema vyama kimsingi tunazungumzia makundi ya watu na tunapozungumzia makundi ya watu tunazungumzia mtu mmoja mmoja na huyo mtu mmoja mmoja ni mimi na wewe na yeye.
 
Top Bottom