PPFT: Askofu Kakobe usitumie mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.

Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.

"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.

Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.

Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.

"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake,” alisema.

Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.

Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.

Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.

Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.
Chanzo: Habarileo.
 
Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Huyu aliyeitoa tamko Ana hadhi gani katika jamii? Huu umoja unahusisha vijikanisa gani? CCM mnahangaika sana , Kinana leo huko Singida hakuna habari nini ?
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,373
2,000
tpkea lini katibu tawala msaidizi akamwakilisha mwanasiasa mkuu wa mkoa!kwani wakuu wa wilaya hawapo..huyu mtendaji anatumika kisiasa,..
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,373
2,000
itifaki inakataa mtendaji kumwakilisha rc wakati dc's wapo!anatumika kiccm huyu mtendaji
 
Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,262
2,000
Watu hawamwelewi Kakobe hata chembe. Wanamwona kwa nje nje tu. Wazungu wanasema don't judge a book by its cover. Mimi naamini Kakobe ni mtumishi wa Mungu ambaye anatumika kufikisha ujumbe kwa watawala ambao hata kama wameweka pamba masikioni utawafikia tu.

Mkuu wale waliosema JK ni chaguo la Mungu wao ni sawa, lakini Kakobe kudai Tanganyika ni mchochezi!! Hakuna mahali popote kwenye katiba panapokataza mtumishi wa Mungu kushiriki ktk siasa.
 
GBBS

Member
Apr 2, 2012
78
125
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.

Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.

"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.

Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.

Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.

"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake,” alisema.

Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.

Akifunga semina hiyo Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Leonidas Gama, alisema inasikitisha kuona viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa, kwa kutoa kauli zinazowafanya wananchi kuhoji kama viongozi hao hawatumii dini kutekeleza malengo ambayo sio mema.

Alisema Serikali bado ina imani na viongozi wa dini, kwa wale wanaozingatia maadili na utume wao wa kuhakikisha amani iliyodumu kwa miaka mingi inadumishwa.

Aliwataka waumini kutowaunga mkono wanaotumia mimbari kuwa jukwaa la siasa kwa kutoa maneno makali yanayohatarisha amani na kupandikiza chuki miongoni mwa waumini na wananchi.
Chanzo: Habarileo.

Hakuna mahali popote ambapo Askofu Kakobe amesema maneno ya uchochezi.Nilichokisikia kwa Askofu Kakobe ni kuisema kweli.Tatizo baadhi ya watu hasa watawala wakiambiwa ukweli na kuona yanayosemwa yanagusa masilahi yao ndio wanasema uchochezi.Mchochezi ni yule anayeficha ukweli na kusema uongo! Mtu wa jinsi hiyo anachochea watu kuleta vurugu pale watakapogundua kwamba wamedanganywa.
 
makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo mmi napita tuu maana naona kuna mvua kali kidogo nikaoni chumba changu kiko hali gani na huyu askofu nna mhishimu sana
 
Otorong'ong'o

JF-Expert Member
Aug 17, 2011
35,461
2,000
Hakuna mahali popote ambapo Askofu Kakobe amesema maneno ya uchochezi.Nilichokisikia kwa Askofu Kakobe ni kuisema kweli.Tatizo baadhi ya watu hasa watawala wakiambiwa ukweli na kuona yanayosemwa yanagusa masilahi yao ndio wanasema uchochezi.Mchochezi ni yule anayeficha ukweli na kusema uongo! Mtu wa jinsi hiyo anachochea watu kuleta vurugu pale watakapogundua kwamba wamedanganywa.

We huoni hiyo habari imeripotiwa na Gazeti gani...?? Angalia mgeni rasmi ni nani..??

Huyo Askofu sijui atakuwa kapewa fungu kiasi gani...Njaa ni mbaya sana..
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
Huyu aliyeitoa tamko Ana hadhi gani katika jamii? Huu umoja unahusisha vijikanisa gani? CCM mnahangaika sana , Kinana leo huko Singida hakuna habari nini ?

Kwani KAKOBE ana hadhi gani katika jamii? Kiongozi wa Dini anayetumia maandiko matakatifu kuwatawanya Kondoo hafai katika jamii ya wastaarabu.
 
Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
7,290
2,000
Askofu Ikongo mbona ndio namsikia leo, halafu hao waliokuwa nao kwani sio wanasiasa? Anataka apewe shavu kama yule mwingine Mtetemela halafu hawa sijui wanawakilisha kina nani, nadhani wanawakilisha matumbo yao...
 
Mkirua

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
5,656
1,225
Chanzo: Habari leo, Mtoa hoja: MwanaDiwani....
Ngoja nitafute nyuzi nyingine za maana
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK

Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,881
2,000
Umoja wa makanisa ya kipentekoste tanzania ni PCT.na mwenyekiti wake ni Akofu David BARTEZ.Huyo Askofu Ikongo lazima aseme hicho alichokisema kuhusu Askofu KAKOBE na anatumika na CCM yeye mwenyewe anajua hilo.Kisa cha majina ya PCT yaliopelekwa Ikulu kukataliwa ni kwa sababu PCT kukata majina ya maaskofu watatu ambayo wangetumiwa na ccm kwenye Bunge la Katiba na mmoja ni huyo Ikongo.na ccm walipoona watu wao hawapo kati ya majina yaliyotumwa Ikulu ndiyo zikaanza zile sarakasi zooooote oh PCT hawajaleta majina.shishangai na sitashangazwa na matamko ya Ikongo.Tegemeeni matamko mengi kama hayo kutoka kwa Ikongo.
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,998
2,000
Askofu kakobe aangaliwe kwa tahadhari sana.

Asije Kuwachoma moto kondoo wake kama walivyochomwa enzi zile na Mtumishi yule anaeitwa KIBWETERE..

KONDOO KUWENI MAKINI.
 
Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
736
500
Watu hawamwelewi Kakobe hata chembe. Wanamwona kwa nje nje tu. Wazungu wanasema don't judge a book by its cover. Mimi naamini Kakobe ni mtumishi wa Mungu ambaye anatumika kufikisha ujumbe kwa watawala ambao hata kama wameweka pamba masikioni utawafikia tu.
wapi kitufe cha like mkuu!? umesema kweli Mungu akukumbuke!
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Huyo Ikongo ni kibaraka tu wa Interahamwe, wala hata hana Kanisa. Kikao hicho cha Moshi kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa aliyesema kwamba anataka kuzungumza na Viongozi wa dini Jumatatu, na kwamba watakuwepo pia wageni kutoka Dar. Ajenda ya kikao haikutajwa, wala hao wageni kutoka Dar hawakutajwa kuwa ni akina nani. Wakati Viongozi wa dini wanamsubiri Mkuu wa Mkoa, ndipo ikaelezwa kwamba Mkuu wa Mkoa atakuja baadaye, lakini kabla hajafika, kuna Kiongozi wa dini kutoka Dar atakayekuwa mzungumzaji. Ndipo akasimamishwa Ikongo, ambaye muda karibu wote wa "semina" yake aliwaambia Viongozi wa dini wasiwe kama Kakobe ambaye amekuwa mstari wa mbele kuidai Tanganyika katika mahubiri yake ya "chuki na uchochezi". Mwisho wa hiyo "semina", Ikongo akamaliza kwa kuwaponda pia Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT), Askofu David Batenzi; na Katibu Mkuu wa PCT, Askofu David Mwasota.

Baada ya Ikongo kumaliza ndipo aliposimama Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa, aliyesema kwamba anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa, ambaye eti amepata majukumu muhimu yaliyomfanya alazimike kwenda Same. Katibu huyo pia akawaambia Viongozi wa dini kuilinda amani, kama vile kuzungumzia Tanganyika ndiyo kuiondoa amani. Viongozi wengi wa dini waliohudhuria, walisikitika sana kuona kwamba wamedanganywa kwamba Mkuu wa Mkoa atazungumza nao, kumbe ni propaganda za "Kiongozi wa Dini" Ikongo, ambaye hataki Viongozi wa dini kuzungumzia kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika. Interahamwe wanataka Viongozi wote wa dini wawe kama yule mpuuzi Askofu Mtetemela, na yule Sheikh Jongo aliyelia kwenye Bunge la Katiba kutokana na kukolewa na mahaba ya Interahamwe, na pia Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, aliyesema watu wameitafsiri vibaya kauli ya Lukuvi aliyosema Kanisani Dodoma, kama vile alizungumza lugha ya Kichina, tusiyoielewa!!!
 
hana hadhi ya kumfikia Askofu David Batenzi kwa sababu Askofu Batenzi siyo mchumia tumbo kama Ikongo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom