PPF Yafilisika, Yauza mpaka maeneo yalitengwa kwa ajili ya misikiti na makanisa Kiseke Mwanza

mchukiaufisadi

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
546
193
Source: The Guardian 14 December, 2011 page 10

Miaka ya 2003-2005, PPF kwa mbwembwe kubwa walianzisha mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wanachama wake kama mwitikio wa maombi ya wanachama wao. Ili kutekeleza hili walinunua viwanja Mwanza eneo la Kiseke, Iringa eneo la Mawelewele.

Kwa kuanzia, zilijengwa nyuma karibu 550 pale kiseke ambazo Rais Kikwete alizifungua kwa sherehe kubwa ya PPF. Eneo hili lilipangwa vizuri maeneo ya nyumba za kuishi, nyumba za ibada, shule, hospital masoko etc. Upangaji huu na mradi huu ulipangwa vema na Mkurugenzi Mkuu (Naftal Nsemwa) aliyekuwepo wakati huo kabla ya huyu wa sasa bwana Wiliam Erio.

Katika hali ya kusikisha Mkurugenzi mkuu(DG) wa sasa Bw. Erio William toka apokee cheo hiki hakuna jipya zaidi ya kugombana na wakandarasi aliowakuta, kuacha kutekeleza miradi ambayo wanachama waliahidiwa na kukimbilia miradi mipya ili apate 10%. Pia anapoteza muda mwingi kupambana na wafanyakazi waadilifu ndani ya mfuko, hasa wanaomzuia uizi, uzinzi na matumizi mabaya ya madaraka kama alivyokuwa Mattaka

Viwanja vya Mawelewele Iringa, pamoja na kuvinunua, PPF ilitumia pesa nyingi kuwafidia wenyeji, pesa nyingi kuweka waangalizi, PPF kutokana na matumizi mabaya ya fedha za wanachama kwa kugawana wakurugenzi kwa njia za ujanja mbalimbali, hawawezi tena kujenga nyumba za bei nafuu Iringa na tayari Halmashauri ya Iringa wamevichukua viwanja baada ya muda wa uendelezaji kupita.

Kichekesho ni pale Kiseke, PPF iliwekeza kwenye maji, umeme, barabara na miundombinu mingine. PPF imewadanganya wananchi walionunua nyumba wakitegemea kupata huduma za ibada, masoko, shule nk kwa ukaribu lakini sasa wanauza maeneo yote ya wazi.

Ni aibu kuuza hadi maeneo ya ibada. Mfano, eneo la kanisa wanauza Tshs 49.3milion, la msikiti Tshs 19milion. Hivi makanisa na misikiti wanakwenda kufanya biashara gani huko kiseke wanunue kwa bei yote hiyo. Kwa uhalisia, na jinsi mradi ulivyokuwa, ilikuwa PPF wajenge na kukabidhi, gharama zake zimeingizwa kwenye gharama za nyumba. Nyumba ambazo zina hizo gharama zimeshanunuliwa, sasa iweje viwanja hivi viuzwe tena? KUFILISIKA
Wanachama, serikali na vyombo vingine viliangalie hili ni dalili mbaya na ni uthibitisho kuwa PPF inawadanganya wanachama na pia inawaibia.

Maeneo ya matumizi mabaya PPF

  1. Bodi ya PPF inapata kila mwaka mafunzo nje ya nchi. Bajeti yao ni zaidi ya Tshs 250 Milioni kwa mwaka.
  2. Safari za nje za DG na wakurugenzi wengine ni nyingi mno, zikaguliwe tafadhari
  3. Malipo ya group endowment kwa wakurugenzi ya milioni 200, kila mmoja kwa kila miaka 3 (200MX8) 1.6 Bilioni baada ya miaka mitatu mitatu
  4. Group endowment kwa DG 540M kila miaka mitatu
  5. Gharama za samani (furniture) kila miaka mitatu (8,000,000X40%X12X8) Tshs. 307Milioni
  6. Kodi za magari ya kifahari. Kila baada ya miaka mitatu hununua mapya na kulipiwa kodi yote ya zaidi 50m kwa gari. 50Mx9directors making Tshs 450M
  7. Miradi isiyokamilika ya komputa, kama ENRICH (1BILION), AK System 400m, Fundmaster, 600M
Haya ni baadhi tu ya maovu yaliyopelekea PPF kufilisika kiasi kwamba hawana miradi mipya ya maendeleo.

Wana JF hebu saidieni kudodosa na kuchangia ili kuokoa fedha za wanachama. TUCTA mko wapi? Serikali mko wapi?
 
Maeneo ya ibada (Miskiti na Makanisa) yanaweza kuuzwa lakini si kwa tenda kama ambavyo PPF wanafanya! kwa mfano mimi nikiamua kununua kiwanja hicho kilichotengwa kwa ajili ya msikiti, nikaujenga inamaan utakua ni wa kwangu badala ya waumini!

PPF walitakiwa waorganize na wakazi waliowauzia nyumba hapo kiseke, waunde jumuia (za kikristu na kiislam), PPF ingeweza kujenga hiyo miskiti kanisa na kuziuzia hizo jumuia, au jumuia zingeweza kununua viwanja na kujijengea wenyewe. Kwa utaratibu walioutumia PPF management wamechemka!

PS: mleta mada hii makala ni ya kwako au Guardian? Maana umeandika source Guardian lakini naona makala ni ya kiswahili!
 
Maeneo ya ibada (Miskiti na Makanisa) yanaweza kuuzwa lakini si kwa tenda kama ambavyo PPF wanafanya! kwa mfano mimi nikiamua kununua kiwanja hicho kilichotengwa kwa ajili ya msikiti, nikaujenga inamaan utakua ni wa kwangu badala ya waumini!

PPF walitakiwa waorganize na wakazi waliowauzia nyumba hapo kiseke, waunde jumuia (za kikristu na kiislam), PPF ingeweza kujenga hiyo miskiti kanisa na kuziuzia hizo jumuia, au jumuia zingeweza kununua viwanja na kujijengea wenyewe. Kwa utaratibu walioutumia PPF management wamechemka!

PS: mleta mada hii makala ni ya kwako au Guardian? Maana umeandika source Guardian lakini naona makala ni ya kiswahili!

PPF wametangaza kuuza maeneo ya msikiti na makanisa kwenye gazeti la The Guardian.

Maelezo mengine yote nimeweka mimi maana naijua hali ya ndani ya PPF
 
Huu ndio uozo mwingine wa serikali ya JK. Yapo madudu mengi sana kwenye hizi bodi na taasisi za serikali,wanatafuna hela na hakuna anayewauliza. Mungu ibariki Tanzania
 
where is the outrage?sasa pesa za wanachama ziko salama?[/QUOTE]

Hali ndani ya mfuko ni mbaya mno, uwezekano wa pesa kuwa salama labda kama serikali ikiamua kufanya kazi kama serikali inavyotakiwa kufanya.

Kwa huu mtindo wa mjomba mjomba pesa zinateketea.

Hii ni aibu kubwa kwa PPF kuanza kuliquidate fixed assets zake ili kujiendesha? Shame upon SSRA, PPF board of Trustees and the Ministry of Finance on behalf of the government.

Nashauri Bodi ijiuzulu na menejiment ikibidi ishtakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka na fedha za wanachama kama ilivyofanya kwa David Mattaka aka David Cameroon
 
Kuna Kiongozi walimtuma kuja kwenye Dicota alitia aibu sana kwa kutetemeka na kutokuwa na PowerPoint inayoeleweka!. Hayo mafunzo ni ya nini kama hata kuongea na kufanya PowerPoint
 
Huyo ndugu willium erio (miongoni mwa jamii zinazojiita za kisomi) magereza panamhusu.
 
Serikali ijifunze toka NSSF iliyokuwa inakufa. Baada ya kumweka DG msomi wa masoko Teacher DAU mambo yakanyooka. Shirika kubwa kama lile unampa mwanasheria unategemea afanye nini, ni ujomba ujomba tu. Litakufa.
 
Acha kudanganya umma, I'm in the real estate and construction business. PPF wanayauza ni kweli lakini matumizi (land use) ya maeneo husika yanabaki vile vile hayabadiliki. Hivyo watakaoyanunua watajenga kwa matumizi tajwa hapo awali. Source: angalia advertisement/tender walizotangaza za mauzo ya maeneo (kiseke) mfano shule, public buildings like halls, hospitals etc na ukiangalia re-advertisement zao wameeleza vizuri.

Utafiti umeonyesha kuwa tasisi kama tasisi haiwezi endesha public buildings refer viwanda na tasisi mbali mbali zilizokufa zamani.

Naunga mkono maamuzi ya public areas to be sold. Ppf kama ppf hawawezi kuendesha shule, n.k ni rahisi kuuza eneo kwa watu binafsi wajasiriamali wenye uwezo.
 
Mh DG,

Sikusema wanabadili matumizi bali nimesema wamefirisika na kushindwa kutekeleza miradi. Huu mradi ulipobuniwa na wenye akili timamu, ulipangwa uwe mji wa mfano pale Mwanza. PPF walileta umeme hadi Kiseke, maji wameleta hadi kiseke. Makanisa na misikiti ilitengewa maeneo ambapo mradi ilikuwa uyajenge kwa ajili ya matumizi ya wakazi siyo kibiashara bali kama huduma muhimu eneo lile ambalo liko mbali sana na mji. Gharama za nyumba zilizouzwa ziliingizwa pia gharama za huduma ya jamii kama maji, umeme, shule, makanisa, misikiti na masoko. Watu wengi walipenda utaratibu huu na kuzinunua nyumba za PPF. Leo kuuza hayo maeneo ni sawa na kuwalaghai watanzania pamoja na kumdanganya Rais wa nchi maana siku ya ufunguzi, PPF walilalamika kwa Rais kuwa Tanesco, watu wa maji,wanawasumbua. Pia vibali vya ujenzi wa shule wanasumbuliwa kuvipata.

Tenda ni ya wazi isiyo na masharti, je mnunuzi wa eneo la msikiti akitaka kubadili matumizi kuwa baa atakataliwa? PPF wangawashauri wakaazi walinunua nyumba wajijengee nyumba za ibada kwa gharama zao kuliko kutangaza tenda za wazi. Au wangeongea na viongozi wachunga kondoo wa Mungu ili waone njia nzuri ya kuwakabidhi.

UKWELI ni huu

DG Erio kwao ni Mtwara, amenunua viwanja vingine huko sasa anahangaika kupata pesa za kujengea hizo nyumba. ndio maana anaua mradi wa Mwanza kama kumkomoa DG aliyepita na Mkurugenzi wa Investment aliyepita wakati kuhalisia tunaumia wanachama.

Bila kuonyesha dharau kwa mkoa wa Mtwara, PPF hawana wanachama wengi huko. Hawazidi hata 2%, anataka sifa mkoani kwake sijui ana ajenda gani.

Bw DG sijui DY, mshauri aachane na biashara kichaa hii itamfia. Nisawa NSSF wakati wa Mkulo walijenga nyumba za ghorofa pale Mwanga-Moshi, hayana faida yeyote zaidi ya kuwa mazalia ya popo.



Mh
Acha kudanganya umma, I'm in the real estate and construction business. PPF wanayauza ni kweli lakini matumizi (land use) ya maeneo husika yanabaki vile vile hayabadiliki. Hivyo watakaoyanunua watajenga kwa matumizi tajwa hapo awali. Source: angalia advertisement/tender walizotangaza za mauzo ya maeneo (kiseke) mfano shule, public buildings like halls, hospitals etc na ukiangalia re-advertisement zao wameeleza vizuri.

Utafiti umeonyesha kuwa tasisi kama tasisi haiwezi endesha public buildings refer viwanda na tasisi mbali mbali zilizokufa zamani.

Naunga mkono maamuzi ya public areas to be sold. Ppf kama ppf hawawezi kuendesha shule, n.k ni rahisi kuuza eneo kwa watu binafsi wajasiriamali wenye uwezo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom