PPF wachafuka, agizo la Zitto kwa CAG kukagua 'Group Endowment'; sita wasimamishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PPF wachafuka, agizo la Zitto kwa CAG kukagua 'Group Endowment'; sita wasimamishwa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sexon2000, Jul 25, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo la ufisadi ndani ya PPF limechukua sura mpya na mbaya.

  Miezi ya January hadi March, kulikuwa na mjadala mrefu sana hapa jamvini juu ya tabia mbaya za uongozi wa PPF wa kutumia madaraka vibaya.

  Tuhuma zilizo anikwa hapa ni pamoja na;

  1. Wakurugenzi kujilipa zaidi shilingi milioni 220 kila mmoja za Group Endowment (GES) ambayo sio stahili yao mwaka 2008 na kurudia kujilipa tena mwaka huu mwezi wa tatu kiasi hicho hicho tena. Kwa utaratibu wa PPF kama mwajili, wafanyakazi wa mikataba hulipwa GRATUITY TU na imekuwa miaka yote na wafanyakazi wa kudumu wanapostaafu au kufa hulipwa group endowment. Cha kusikitisha na kwa kutumia madaraka vibaya, wakaamua na hiyo GES wajilipe walipo maliza mkataba. Mhasibu Mkuu wa PPF akakataa kuwa sio sahihi, wafanyakazi wakachachamaa kuzuia lakini wapi, wakachukua mwaka 2008 na wamelipwa tena 2011 licha ya kamati ya fedha ya Bunge kuzuia.

  2. Mwaka 2010, Mkurugenzi Mkuu wa sasa baada ya kumaliza miaka mitatu akalipwa GES isivyo halali Milioni 520, hizi ni nje ya 25% ya mishahara yake kwa kipindi cha mkataba kama gratuity, na ni nje ya 15% anayochangiwa kwenye pension na PPF amabyo nayo ni kinyume na waraka wa Wizara ya utumishi unaokataza watumishi wa umma wanaolipwa gratuity kuchangiwa tena na mwajili michango ya pension

  3. Mkurugenzi wa Fedha na Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani kujichukulia viwanja vya PPF Bahari Beach vilivyonunuliwa mwaka 1996 kwa milioni 56 lakini wao wakavichukua kwa milioni 16 tu mwaka 2004 kwa kisingizio kuwa vinalitia hasara shirika.

  4. Uzinzi ndani ya mfuko uliokithiri. Mkurugenzi Mkuu akiongoza kwa ngono na wafanyakazi ( vibinti vidogo vilivyoajiliwa kama vibarua), Mkurugenzi wa utawala na Mkaguzi wa ndani wakimfuatia.

  5. Uizi kupitia miradi ya uwekezaji, hasa ule wa Bunge na wa UDOM ( vyote vimeanza kuvuja na nyufa mmeziona)

  6. Unyanyasaji wa wafanyakazi wenye msimamo tofauti nao hasa wakipinga udokozi na uzinzi.

  YALIYOTOKEA BAADA YA MJADALA/

  1. Kamati ya ZITTO ikaagiza CAG akague utata wa malipo ya GES toka 2008. Magazeti yakaandika ufisadi huo na Mh. Mwanakijiji akamaliza kwa ripoti yake aliyoiweka humu JF

  2. Uongozi wa PPF ukaanza vitisho kwa wafanyakazi hasa wale wanaodhaniwa kuwa ndio waliotoa siri hiyo nje. Wakawanyang'anya computer zao, wakazuia mtandao wa internet ndani ya PPF

  3. Baadhi wakahojiwa na polisi

  KUSIMAMISHWA KAZI.

  Ijumaa iliyopita, uongozi wa PPF umewasimamisha kazi wale wote ambao computer zao zilinyang'anywa kwa tuhuma za;

  a. Kuhisiwa kushiriki kwenye mijadara ya JAMII FORUMS
  b. Kuhisiwa kutoa taarifa kwenye magazeti
  c.Kupanga mapinduzi ya kuupindua uongozi wa PPF (?????????)
  d. Kuhujumu mfuko eti wanazuia wanachama wasijiunge na PPF

  Hivi niandikapo, LANDCRUISER VX, ya PPF imekwenda Mbeya na kumbeba staff mmoja ili kumpelekea barua aliyekuwa Mhasibu Mkuu aliyegoma kuwalipa GES.

  WANA JF, WATANZANIA NA WAHESHIMIWA WABUNGE

  1. Kamati ya Bunge imeagiza ukaguzi ufanyike, leo mtu mwenye taarifa muhimu za huu ufisadi anasimamishwa kazi ili wakaguzi wakija wao waliodokoa ndio watoe majibu.

  Zitto na Kamati yake wanasemaje kuhusu hili?

  CAG anakubali upuuzi huu?

  2. Hivi katika hali ya uchumi wa nchi hii na mafao kidogo yanayotolewa na PPF, ni sahihi kupeleka barua moja tu kwa VX landcruser na kwalipa allowance dereva na mbeba barua? HII NAYO NI KASHFA. DG ajieleze VALUE FOR MONEY IKO WAPI? Mwezi March walifanya hivi hivi kwenda kumnyang'anya computer.


  Haya tunawasaidiaje hata kama sio wana JF,

  Mwanakijiji na Zitto Kabwe hebu liangalieni
   
 2. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha, matumizi mabaya ya fedha za umma inaonekana ndio fasheni na hawa the so called Vigogo wanashindana kuhujumu rasilimali za haya mashirika ya umma wakishayafikisha kwenye hali mbaya ndio hao wanasiasa wanaingilia kati kupiga blah blah..Kwa kuwa hii ishu Mh.Zitto anaifahamu atatumie nguvu zake kama M/kiti wa PAOC kuingilia kati kuwasaidia hawa jamaa vilevile hawa vigogo wabanwe kwelikweli..
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Tangu huu msamiati ‘‘UFISADI” uanze kufahamika na wizi ndio unazidi kushamiri, tutafika kweli kwa hali hii, michango yetu wao wanagawana
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Duly noted.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naomba niulize, hivi kwa nini Zitto hakulivalia njuga vilivyo hili swala la PPF? Yes, alitaka CAG afanye ukaguzi, je amefualije kujua kama CAG amefanya au atafanya ukaguzi? Pia ningetaka kujua ni kweli NSSF haina matatizo kama haya ya PPF?

  Baada ya Jairo-saga, Zitto angerudisha nguvu yake ya zamani ni kusamimia kile anachosema. Kamati ya bunge ina nguvu sana na kama wanaishia kutoa 'cosmetic' solution hatutafika mbali.
   
 6. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  GES ni kwa malipo ya waajiliwa wa kudumu wanapostaafu au KUFA. Hawa wakurugenzi walioajiliwa kwa Mikataba wameona wajilipe kiwango hicho kwa sababu yawezekana wanakaribia kufa hivi karibuni- Hebu waulizeni wanampango wa KUFA lini ili wana JF wajue.
   
 7. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo yote yalifanyika chini ya kapeti na imegundulika, mimi huwa najiuliza je ni mangapi bado hayajafahamika?.. Lazima tuwe wazalendo na nchi kufichua uozo serikalini, sekta binafsi na maeneo mengine, nawapongeza JF walivyo mstari wa mbele kuibua uozo huuu...tukaze buti wakuu
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa PPF wapuuzi sana, wanawalipa maprofesor mafao kiduchuuuu wao wanalishana milungula ya kufa mtu. Nilishasema, sheria zetu inabidi zibadilishwe, mtu akiiba kwenye haya mashirika ya umma apigwe jela maisha hakuna kucheka nao.

  PPF, LAPF, NSSF ni mashirika yatakayosaidia nchi kuendelea kwa kuwekeza. lakini kama tunayachekea chekea tu, wajanja wachache watakuwa wanafaidi jasho letu, huku sisi tukitaabika kwa uoga wetu.

  Tatizo lingine naloona, tumezoea kuona mtu anayefanya kwenye vitengo nyeti haswaa vya fedha lazima awe tajiri kwa sababu ya uwezekano wa kuiba, sasa ni wakati wa kuangalia upya hizi taratibu, wanaharibu sana maadili ya kazi. Utakuta mtu kama haibi, wabongo wenyewe kwa maneno yao wenyewe watakusema, "huyo jamaa hana lolote, jamaa anafanya kazi sehemu nyeti lakini maisha yake ni hovyo hovyo".
   
 9. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jamani kuna mtu anaweza kunipa huo waraka wa utumishi ili niufanyie kazi na mimi kwenye Namba 2 hapo juu? Maana naona hii ya kulipwa Gratuity na kuchangiwa kwenye mifuko ya pensheni na Employer ni tatizo kubwa sana. Please mwenye waraka ani PM au amwage hapa hapa.
   
 10. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama wewe hawajakufukuza si inamaana wameonea watu wasiohusika kabisa
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,251
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  umeonaaaa alafu wajanja kama huyu awaondoki mpaka kampuni inakufa
  ONYO
  Pombe si nzuri kwa waliochini ya miaka 18
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ni nzuri tu mi nilianza na miaka tisa lakini hadi leo ni mtu mzima na ninadunda tu
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji kuna hisia kwamba baadhi ya watu waliotoa data walikua revealed somehow and fifty percent are not members of JF nor PP employees

  kaazi kwelikweli

  ukandamizaji kwa hisia
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nilitarajia kuona makali ya kamati ya zitto katika suala kama hili lakini naona kama naye amekuwa legelege.
   
 15. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mh. Zitto (Mb) na Mh L. Utouh (CAG)Hivi PPF Management wanapovuruga ukaguzi kwa kuwaondoa wafanyakazi ni sahihi? Lengo kuu hapa ni kumuondoa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa PPF mwaka 2008 ambaye ndiye muibuaji wa wizi na ufisadi kwa kukataa kuwalipa wakurugenzi milioni 220 kila mmoja ambayo si stahili zao. Wanajua akiondolewa PPF, CAG atapewa majibu na wao wenyewe.

  Kwa hili serikari iliangalie kwa upana wake ili kuokoa huu mfuko. Milioni 520 kwa Mkurugenzi Mkuu kila miaka minne kwa lipi kubwa aliloufanyia mfuko? Ni kiongozi gani hapa nchini mwenye mafao makubwa kama wanayoiba hawa wakurugenzi wa PPF. Nasema wanaiba kwa sababu wao haki yao gratuity tu.

  Kwa Mkurugenzi Mkuu alistahili Milioni 132 za Gratuity lakini kwa kutumia madaraka akavuta Mil 520 za GES plus Mil 132 za gratuity jumla karibu Mil 652. Hii ni sahihi? Wafanyakazi wakihoji, wanasimamishwa kazi kwa kutishia wengine wasijitokeze.Rais J kikwete, hebu ingilia kati uuokoe huu mfuko.
   
 16. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanatakiwa kushtakiwa na Kufungwa kwa uhujumu uchumi. Hivi hii ndio Tanzania kweli watu wanajilipa na kufanya ufisadi wa namna hii. Huku wafanyakazi wa Tanzania tunachangia mifuko hii kwa ajili ya kuwanufaisha wachache huku tukiambulia kiduchu tunapo staafu.

  Hii ni hujuma. Hawa jamaa watakuwa na mtandao unaolindwa na serikali ya JK. Tuachieni Tanzania Yetu Jamani. Hamtaki tutawaondoa kwa nguvu. Kama ni Noma na Iwe Noma. People's Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer!!!!!!!!!!!!!
   
 17. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wana JF, kesho uongozi wa PPF unawapandisha kizimbani wafanyakazi waliosimamishwa kwa kuhisiwa kuchangia na kupost issues za ufisadi wa PPF humu jamvini.

  Zitto Kabwe mbona kimya? Toa mwongozo maana wanaharibu ukaguzi wa CAG uliouagiza.
   
 18. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mengi PPF hayo mbona madogo....Mengine yako Dawasco.
   
 19. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  DAWASCO kunani na maji hawatupi?????   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wana bahati mimi sio mwanachama uko!mnalipana GES mihela yote iyo kwa lipi la maana!
  Alafu JK bwana hawa ndo wanaokuaribia badala ya kuwatimua utawasamehe at the end wananchi watakufa moyo wa kuchangia
  Ivi hii mifuko inafall chini ya wizara ya kazi?hope budget yao baddo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...