PPF waanza kueleweka, kama wewe ni muhanga wa fao la kujitoa fanya hima

tumaini obedi

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
340
190
Ndugu wanaJF,

Mimi jana nifika katika ofisi za PPF kuuliza chochote baada ya kupata tetesi kuwa wameaza kutoa lile fao la kujitoa, ambalo mwanzoni kabisa walisema hawatatoa mpaka ufikishe miaka 55.

Nilifika majira ya saa nne hivi asubuhi, nilionana na afisa mmojawapo nikamuuliza kuhusu jambo hili
akasema ndio na akanitaka nirudi jumatatu na document zangu zote .

Aidha nilikutana na watu wengine wengi sana waliokuwa na bahasha wenye shida na fao la kujitoa na wengine wakiwa tayari wameishajaza fomu za zao walizokuwa wapewa na afisa wa PPF.

Lakini pamoja na haya yote, niligundua bado kuna ka-urasimu maana kuna mmoja alirudishwa. Afisa alimwambia eti hana vigezo, eti yenye aliacha kazi mwenyewe na wanashughulika na walioachishwa kazi, lakini siyo walioacha kazi wenyewe. Aidha walimutaka asubiri hadi watakapopata maelekezo ya serikali.

Wengine walikuwa wakiulizwa "Je ulikuwa kampuni gani?" Yote hayo niliyasikia

Fika ujaribu ikingali mapema.

Asante.
 
Hii mifuko ya hifadhi ya jamii ina mambo ya ajabu sana kwani ukiacha kazi mwenyewe hizo hela si zako pia!
 
Aisee kweli kuna urasimu mwingi sasa kuacha kazi mwenyewe na kufukuzwa kazi kuna cha ajabu kipi maana hela ni zilezile hazina tofauti
 
Huu ni upuuzi mkubwa sana kwani nikiacha kazi ndo nisichukue hela zangu? Hii mifuko haina faida kwa wanachama wake bora tu ikafutwa.
 
Bado kuna tatizo hapo,haiwezekani pesa niliyokatwa kwa "lazima" (kwa mujibu wa sheria)...ninapoihitaji napewa masharti...suala la kuacha kazi lina sababu nyingi,waache urasimu watoe pesa kwa wote!!
 
Back
Top Bottom